USALITI: Je wewe ni msaliti kwa Mpenzi wako? Unapata faida gani unaposaliti?

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,556
7,085
aa-couple-laying-in-bed.jpg

images

Habari za muda huu wadau wa JF hasa jukwaa hili la MMU? Ni matumaini yangu kuwa wengi wetu ni wazima... Kwa wale mnaoumwa au mnauguza ndugu basi nawapa pole sana najua mda si mrefu mtakuwa katika hali nzuri . Pia nawapa pole wale walioondokewa na ndugu zao wapendwa.... Mungu awape pumziko marehemu wote huko waendapo.

Leo nimeona ni vyema sote kwa pamoja tuzungumzie suala zima la USALITI katika mahusiano ya kimapenzi. Je unafaidika na nini unapomsaliti mwenzi wako?
Hebu Nifuatilie Kwa Makini Sana Na Nina Imani Kuna Kitu Utajifunza...

Kama Kuna Kitu Kinachukiwa Na Wengi Katika Mapenzi, Basi Ni Usaliti. Ni Kilio Cha Wengi. Vijana Kwa Wazee, Wote Hawa Hawataki Kusalitiwa. Usaliti Una Maumivu Makali. Kiukweli Kila Mmoja Huwa Anajisikia Vibaya Sana Anaposalitiwa.
Wengi (Hasa Wanawaume) Baada Ya Kuwasaliti Wapenzi Wao Huwa ...Na Maamuzi Mazito Sana. Wakati Mwingine Hufikia Uamuzi Wa Kukatisha Uhusiano Kwa Sababu Hiyo. Unadhani Ni Kwa Nini Wanachukua Uamuzi Huo Mgumu? Hakuna Kingine Zaidi Ya Maumivu.

Unajua Kuna Watu Ambao Huumia Na Kuchukia Sana Wanaposalitiwa, Lakini Wao Ni Wasaliti Namba Moja. Kwa Nini Wanafanya Hivyo?

Je, Kwa Kufanya Hivyo Wanafaidika Nini? Hebu Nizungumze Na Wewe Rafiki Yangu Ambaye Una Tabia Hiyo Mbaya Ya Kusaliti, Unajisikiaje Unaposaliti? Amani? Kuna Faida Unayoipata Kwa Kusaliti Kwako?

Binadamu Wote ni Sawa
Kuna Mambo Mengi Ambayo Mpenzi Akifanyiwa Na Mwenzake Lazima Ataumia Sana. Ingawa Kuna Mengine Yanafichwa Au Kupasishwa Kama Sahihi, Lakini Ukweli Unabaki Pale Pale Kwamba Yanaumiza.

Kikubwa Ambacho Unatakiwa Kufahamu Ni Kwamba Maumivu Hayo Yapo Sawa Kwa Kila Mmoja. Haijalishi Jinsi, Umri, Kabila Wala Dini, Maumivu Ya Mapenzi Yote Yanafanana. Kufanana Huko Kunasababishwa Na Mioyo Yote Kuwa Na Nyama!
Kwa Sababu Mioyo Yote Ina Nyama Basi Unatakiwa Kufahamu Kwamba, Jinsi Unavyoumia Wewe Moyoni Mwako, Ndivyo Mpenzi Wako Anavyoumia Ikiwa Utamkwaza Kwa Namna Yoyote.

Vipi Ukisalitiwa wewe? Je utajisikiaje?

Unajua Kabisa Una Mpenzi, Tena Inawezekana Wakati Mwingine Mmeshawahi Kuzungumza Juu Ya Kuishi Pamoja, Lakini Bila Haya Wala Aibu, Unamsaliti! Kwa Nini Unafanya Hivyo? Kama Umeona Hana Thamani Tena Kwako, Kwa Nini Unazidi Kumpotezea Muda?
Unafikiri Anafurahia Sana Wewe Kuwa Na Kimada Mwingine Huko Uchochoroni Au Unadhani Atafurahi Siku Akijua Kuwa Una Mtoto Umezaa Nje Ya Ndoa Yako? Nafsi Yako Yenyewe Inakusuta, Inajua Ni Kiasi Gani Unamkosea Mpenzi Wako Lakini Unajifanya Kichwa Ngumu Na Kuendelea Na Uchafu Wako. Kwa Nini Hutaki Kubadilika?

Hebu Jitoe Katika Nafasi Yako, Kisha Mfanye Mpenzi Wako Ndiyo Wewe, Halafu Fikiria Kama Yeye Ndiyo Angekuwa Anakusaliti, Ungejikiaje? Lazima Utaumia! Sasa Kama Utaumia Kwa Nini Unaendelea Kumfanya Mwenzako Akose Raha?

Lazima Uwe Na Moyo Wa Huruma, Akili Yako Ifanye Kazi Ipasavyo Na Kugundua Makosa Unayoyafanya Kisha Kufanya Mabadiliko Ya Haraka. Amini Jinsi Utakavyoumia Kwa Kufanyiwa Mabaya Na Mwenzako Ndivyo Mpenzio Anavyoumia Kwa Mabaya Unayoyafanya.
Wengi Wamekuwa Wakiwasaliti Wapenzi Wao Wakiwa Hawafikirii Siku Ya Wao Kufanyiwa Hivyo Itakavyokuwa. Hebu Vuta Picha, Unakwenda Nyumbani Kwa Mpenzi Wako, Unagonga Mlango Haufunguliwi!

Lakini Baadaye Unahisi Kama Ndani Kuna Watu, Hilo Linaingia Akilini Mwako Baada Ya Kuona Viatu Vya Mpenzi Wako Pamoja Na Viatu Vingine Vya Jinsi Tofauti Ya Mpenzi Wako. Unaamua Kusukuma Mlango Na Kuingia Ndani, Hamadi! Unakuta Mpenzio Akiwa Anafanya Mapenzi Na Patna Mwingine...Utajisikiaje?
Mapenzi Ya Kweli Hayaambatani Na Usaliti. Penzi La Kweli Lina Uaminifu Wa Dhati, Kuchukuliana, Kupendana, Kusaidiana, Ukarimu, Huruma Na Mengine Mengi Ambayo Huyafanya Mapenzi Yazidi Kuwa Imara Kila Siku.

Hakuna Mwenye Haki Ya Kusaliti, Kwa nini wamsaliti mwenzako?

Acha Kujiwazia Mwenyewe, Kujiona Wewe Pekee Ndiye Mwenye Haki Ya Kuwa Salama Katika Penzi Lako. Chunga Nafsi Yako Lakini Wakati Huo Huo Ukiangalia Kwa Jicho La Tatu, Nafsi Ya Mwenzako.

Kila Mmoja Anaumia Anapohisi Anasalitiwa, Hivi Unafikiri Ni Nani, Anayependa Kushea Mapenzi? Nani Mwenye Haki Ya Kumsaliti Mwenzake? Kimsingi Hakuna. Utakuta Mwingine Simu Ya Mpenzi Wake Ikiita Yeye Anakuwa Wa Kwanza Kuichukua Na Kutaka Kupokea Au Kusoma Sms, Lakini Subiri Sasa Simu Yake Iite; Anakuwa Mkali Huyo! Acha Kujifikiria Peke Yako.

USHAURI
Je wewe ni msaliti? Hapa Nakusisitiza Ufanye Mabadiliko Ya Haraka Ili Mwisho Wa Siku Uweze Kuishi Maisha Mapya, Mazuri, Yenye Mapenzi Ya Kweli Huku Moyo Wako Ukiwa Huru.

Hutakuwa Na Hukumu Moyoni Mwako, Maana Utakuwa Unamtendea Haki Mpenzi Wako. Lakini Kama Ukiendelea Kumsaliti, Ujue Wazi Kwamba Utakuwa Unajizidishia Maumivu Katika Moyo Wako.

no-cheating.gif

haya mafundisho tuyabadili maana kwa direction hii ni magumu sana, cheating will never end in this world. So tuwafunze watu kuwa na roho zisizoumia wapenzi wao wanapo cheat, yaani wasichukulie very serious. Believe me or not everyone cheats na kama kuna asiye cheat basi hajapata hiyo opportunity tu either kabanwa. kuna watu wana take relations very seriously but doesnt mean kwamba they dont cheat, they do. My advise is: dont take relationships very seriuosly, otherwise life wont be easy.
 
Usaliti ni ushetani tu.
Samtym ni tabia ya mtu tu.
Na hyo tabia ikikomaa itakua sugu tu.
Usaliti btw unamfanya mtu kuwa Mtumwa wa nafsi na kukosa uhuru ktk mahusiano yake.
Usaliti ni Sumu ya mapenzi coz unaumiza na kusababisha mahausiano kuvunjika.. So usaliti hauna faida
 
Last edited by a moderator:
Ahhhhhhhhhhhh wap!

1.Kwanini ule chakula kile kile for the rest of your life wakati vingine vipo tena vyataka vyenyewe kuliwa! Unless umeambiwa na Dr. Usile kwa afya yako au huna uwezo mkeo anakutunzia siri.

2.What you dont know cant kill you! So asipojua there is no harm!

3.Haramu ni tamu siku zote, hata kitimoto ni haramu ila mtamu balaaaaa!

4.Cheatting ina utility kubwa kuliko home ndo maana nyumba mmepanga ila bi mdogo anafungiwa lenter. Ingekuwa utility hakuna wala wasingerudia rudia.

5. Huwezi kwenda na wakati na kuwa technologicaly inovetive bila kucheat. Kila siku matole mapya ya nini unganganie TV la chogo wakati kuna Kitu ya LCD na LED hadi zile extraa slim za kutundika ukutani. WE LIVE ONLY ONCE! AND WE MUST LIVE TO THE FULLEST. Vitu zinazaliwa laiiiini kama una nawa! Mtoto anabonyea bonyeeeeeeeeeeeee! Wkt home umeacha kitu kimezoea kushuka milima, na kulima.

6.Lazima uonje uonje ili ujue ipi tamu! Huwezi kuwa unasifia maharage matamu kuliko vyakula vyote wakati hujawahi onja Lobster na Caviar! Nasisitiza WE LIVE ONLY ONCE! IF YOU LIVE IT WELL ONCE IS ENOUGH!

DISCLAIMER!!!!!!!!!

SI MANENO YANGU MIMI (Akuuuuuuuuuu! Simo kabisaaaaaaaaaa! Tena mnitue mwana wa mwenzenu!) NI MANENO YAKE SHETANI HAYO KATIKA KUWALAGAHI ILI AKUCHOMENI UZURI SIKU YA MWISHO.

Katika kipindi hiki cha Kwaresma napenda kuwakumbusheni MTU HATOISHI KWA MKATE TU ILA NENO LILETALO UZIMAAAA! Mbarikiwe sanaaaaa!
 
Unadhani ni rahisi sana kufanya hicho ulichoandika hapo kwenye red?
 
Usaliti ni ushetani tu.
Samtym ni tabia ya mtu tu.
Na hyo tabia ikikomaa itakua sugu tu.
Usaliti btw unamfanya mtu kuwa Mtumwa wa nafsi na kukosa uhuru ktk mahusiano yake.
Usaliti ni Sumu ya mapenzi coz unaumiza na kusababisha mahausiano kuvunjika.. So usaliti hauna faida

point.... nadhani wenye tabia wamekusoma
 
Ahhhhhhhhhhhh wap!

1.Kwanini ule chakula kile kile for the rest of your life wakati vingine vipo tena vyataka vyenyewe kuliwa! Unless umeambiwa na Dr. Usile kwa afya yako au huna uwezo mkeo anakutunzia siri.

2.What you dont know cant kill you! So asipojua there is no harm!

3.Haramu ni tamu siku zote, hata kitimoto ni haramu ila mtamu balaaaaa!

4.Cheatting ina utility kubwa kuliko home ndo maana nyumba mmepanga ila bi mdogo anafungiwa lenter. Ingekuwa utility hakuna wala wasingerudia rudia.

5. Huwezi kwenda na wakati na kuwa technologicaly inovetive bila kucheat. Kila siku matole mapya ya nini unganganie TV la chogo wakati kuna Kitu ya LCD na LED hadi zile extraa slim za kutundika ukutani. WE LIVE ONLY ONCE! AND WE MUST LIVE TO THE FULLEST. Vitu zinazaliwa laiiiini kama una nawa! Mtoto anabonyea bonyeeeeeeeeeeeee! Wkt home umeacha kitu kimezoea kushuka milima, na kulima.

6.Lazima uonje uonje ili ujue ipi tamu! Huwezi kuwa unasifia maharage matamu kuliko vyakula vyote wakati hujawahi onja Lobster na Caviar! Nasisitiza WE LIVE ONLY ONCE! IF YOU LIVE IT WELL ONCE IS ENOUGH!

DISCLAIMER!!!!!!!!!

SI MANENO YANGU MIMI (Akuuuuuuuuuu! Simo kabisaaaaaaaaaa! Tena mnitue mwana wa mwenzenu!) NI MANENO YAKE SHETANI HAYO KATIKA KUWALAGAHI ILI AKUCHOMENI UZURI SIKU YA MWISHO.

Katika kipindi hiki cha Kwaresma napenda kuwakumbusheni MTU HATOISHI KWA MKATE TU ILA NENO LILETALO UZIMAAAA! Mbarikiwe sanaaaaa!

Je faida za kusaliti ni nini? unapata nini?
 
haya mafundisho tuyabadili maana kwa direction hii ni magumu sana, cheating will never end in this world. So tuwafunze watu kuwa na roho zisizoumia wapenzi wao wanapo cheat, yaani wasichukulie very serious. Believe me or not everyone cheats na kama kuna asiye cheat basi hajapata hiyo opportunity tu either kabanwa. kuna watu wana take relations very seriously but doesnt mean kwamba they dont cheat, they do. My advise is: dont take relationships very seriuosly, otherwise life wont be easy.

Thanks!
 
Je faida za kusaliti ni nini? unapata nini?

GOOD TIMES MEIN! ITS ALL ABOUT THE GOOD TIMES!!!!!!!!!!!!! Whe we reach 70 memories will be all that is remaining with us!!!!!!!

We gota make them enjoyable by the time we are 70 !!!!!!
 
GOOD TIMES MEIN! ITS ALL ABOUT THE GOOD TIMES!!!!!!!!!!!!! Whe we reach 70 memories will be all that is remaining with us!!!!!!!

We gota make them enjoyable by the time we are 70 !!!!!!

Hauwezi kuwa na good time na mpenzi wako mmoja? je itakuaje wewe ukisalitiwa?
 
Kwa leo naogopa kuchangia, ni wakati wa Kwaresma... Tuonane baada ya kipindi hiki kuisha.
 
Back
Top Bottom