Usaliti unauma

Usaliti unauma

MKALI W MAMBO

Senior Member
Joined
Aug 9, 2018
Posts
190
Reaction score
135
Mwaka 2010 niliingia katika mahusiano ya kimapenzi na binti mmoja mwanafunzi wa kidato cha 5.

Tulidumu kwa muda mrefu sana kwani alikua akisoma jitegemee sec school nilikua nikimuhudumia vitu mbali mbali vya shuleni mfano pesa ya matumizi na kadharika japo Ada ya shule alikua akilipiwa na wanafamilia yake ususani ndugu zake.

Mpaka alipomaliza kidato cha sita tulikua bado wapenzi na nilikua nikimjali kwa kila hali na kumsaidia shida zake kadri ya uwezo wangu.
Mwaka 2012 akajiunga na chuo cha ualimu kwa ngazi ya sekondary ikambidi akakae huko huko Hosteli lakini bado nilikua karibu nae kwa mawasiliano kwani alienda kusomea mkoani mbeya.

Sikusita kumsaidia japo yupo mbali nilikua nikimsaidia mambo mbali mbali ikiwemo pesa ya matumizi na hata nguo pia n.k.

Mpaka alipomaliza mafunzo yake ya Diploma mwaka 2014 hakubaatika kupata ajira ya moja kwa moja hivyo aliludi kukaa nyumbani kwanza kusubili ajira hapo tulikua karibu saanaa na kupanga mipango mingi ya kimaisha kwa wakati huo na baadae pamoja na kukubaliana kuja kufunga ndoa.

Mwaka 2016 akabaatika kupata nafasi ya kujiunga na JKT kwa kujitolea na yote hilikua ni kwa juhudi zangu kwani nilitafuta mtu wa kumuunganishia si unajua siku hizi ili kupata nafasi JKT ni lazima uwe na mtu wa kukushika mkono hasa ukiwa na elimu ya juu.

Akafanikiwa kumaliza mafunzo ya jkt na kupangiwa kambi kwa ajili ya kujitolea kusubili Ajira kwa kuwa ana elimu ya juu akuchelewa kuchukuliwa na JWTZ na kwenda kupitia Kozi ya JWTZ baada ya kuludi uko na kuapishwa kuwa mwanajeshi rasmi alianza kubadilika kwa upande wangu nilishindwa kuelewa kabisha ni mwaka huu 2018.

Alikua mtu wa tofauti sana simu zangu hapokei kwa wakati msg ajibu yaani niliumia saaana.

Nikamuomba tuonane tuongee kwa kina nini tatizo Alichonijibu sikutegemea.

Nilijibiwa hivi....FANYA YAKO NA MIMI NIFANYE YANGU NASHUKURU KWA UKARIMU WAKO NA KUWA MWEMA KWANGU KWA KIPINDI CHOTE AHSANTE.

Niliumia sana sikuelewa ni kwa nini ameamua kunifanyia hivi au labda nimemkosea lakini cha ajabu aliniblock kila kona
Facebook
Whatsapp
SMS
Call

Yaani sikutegemea inauma sana
Nawaombeni wanawake kuweni na Moyo wa huruma pia mkumbuke fadhira na hutu alio kufanyia mtu Usika...
 
Mimi nimedumu 7 years kwenye mahusiano lakn mwaka huu ameniacha,simu hapokei wala sms hajibu,nilimgharamia kama wew na sasa ni mwalimu kaniacha,ila sina stress mana nimewapanga balaa
1.Kuna nurse 2
2.Kuna mwalimu 1
3.Mfanyabiashara 1
Jumla 4
Ni dhambi kubwa sana kuwa na mwanamke mmoja hapa duniani
 
Pole sana, maisha ni kujifunza pamoja na maumivu aliyokuachia usijali analo deni la kukulipa ipo siku atakukumbuka tu.
 
Mimi nimedumu 7 years kwenye mahusiano lakn mwaka huu ameniacha,simu hapokei wala sms hajibu,nilimgharamia kama wew na sasa ni mwalimu kaniacha,ila sina stress mana nimewapanga balaa
1.Kuna nurse 2
2.Kuna mwalimu 1
3.Mfanyabiashara 1
Jumla 4
Ni dhambi kubwa sana kuwa na mwanamke mmoja hapa duniani
Zambi kivip tena mkuu
 
Pole mkuu ndo maisha ujifunze tu ila naona pia ulikosea kumpeleka huko jkt wanawake wa kijeshi akili zao wanazijuaga wenyewe
 
Ndio huenda kaona hakuna future kati yako na yeye.

Niliwahi kuwepo jkt kipindi fulani nilisikia( japo sina uhakika) kuwa mwanajeshi wa kike haruhusiwi kuolewa na raia ila wa kiume anaruhusiwa kuoa raia.

Yawezekana ni sababu
Mbona wapo wengi wa kike wameolewa na raia
 
Ndio huenda kaona hakuna future kati yako na yeye.

Niliwahi kuwepo jkt kipindi fulani nilisikia( japo sina uhakika) kuwa mwanajeshi wa kike haruhusiwi kuolewa na raia ila wa kiume anaruhusiwa kuoa raia.

Yawezekana ni sababu
Sio kweli mkuu
 
Duuuh zikoje kwani ndugu au wanaaribika
Nijuavyo wote huwa wanatolewa uraia na kuwa tofauti na aria wa kawaida sasa ni wanawake wachache sana wanaoweza kubaki na ile spirit na kike na kujikubali kama mke wengi huwa wanaharibiwa na mazingira ya kazi zao usikute mngeendelea angekuja akuache baadae sana labda kwa kuona hamuendani kitabia
 
Kuna mambo mengi sana ya kufanya katika hii dunia, mapenzi yanauma sana. Ukishindwa kuvumilia maumivu yake, achana nayo.
 
Pole sana rafiki,mwenyewe nilishakumbana na kadhia kama yako,tofauti ni kuwa ilikuwa twende naye wote JKT,lakini mie majina hayakuwa vizuri,hivyo akapata yy nafasi mie nikakosa,mie nikaamua kuendelea na masomo ya juu zaidi.
Mwaka wa mwisho kumaliza chuo ,naye ndio anapata kazi JWTZ,hapo akaanza kunichenjia.
Mie nikasema ,no sweaty,nikaamua pia kumuumiza kisaikolojia..Nikamwambia kuwa nilikuwa sikutaki ndio maana nikakusakizia uende jeshini ili niwe huru kula bata na nimpendaye,maana nilikuwa sikupendi,ila nilikuwa natafuta njia ya kukupiga chini. Alinipigia, nikamchana,sasa ivi analazimisha angalau tupige shoo tu,mie sitaki tena.
 
Back
Top Bottom