Usaliti katika mapenzi, hali gani unakuwanayo baada ya hapo!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usaliti katika mapenzi, hali gani unakuwanayo baada ya hapo!?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Uncle Jei Jei, Mar 23, 2012.

 1. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  Siku hizi limekuwa jambo la kawaida watu kuongelea jinsi wanavyo wasaliti wenza wao! Wengine hutoa hata mbinu wanazotumia kutembea na wake/waume au wapenzi wa wenzao! Hivi ukishamaliza kufanya tendo la ndoa na mtu asiye wako hasa kwa wanawake! Hivi, hujisikii aibu?? Unapokutana naye au mnapokuwa nyumbani siku hiyo unamuonaje mwenzako!?, humuonei aibu kweli?? Au ndo unamdharau! Na je ikitokea akataka gemu, unafanyaje??
   
 2. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Ni mambo machafu na ya aibu ambayo sehemu ya jamii ya Kitanzania imedumbukia ktk dimbwi la matendo haya! Ukosefu wa maadili, malezi mabaya, utandawazi, kukuso utu na ubinadamu, kutokumuogopa na kumheshimu Mungu na kukosa mapenzi ya dhati baina ya wapenzi wawili ni sehemu ndogo ya sababu ambazo zinawafanya watu kuyatenda mambo haya bila aibu!

  Nashauri ifike wakati, watoto wetu wafunzwe yafuatayo kusaidia kupunguza matatizo kama haya ktk vizazi vijavyo.
  1. Tuwalee watoto ktk imani ya kufahamu kuwa Mungu yupo, then tuwafunze wamuogope na kumheshimu,
  2. Tuwape watoto Malezi bora ya kijamii tukiowaonya juu ya tabia mbaya na madhara yake kwa jamii. Watawezi kubaini na kukataa maovu ukubwani maana tayari watakuwa na msingi mzuri wa malezi
  3. Waelimishwe juu ya matumizi sahihi ya teknolojia na madhara yake ktk jamii kujenga na kukuza ufahamu wao

  Kwa kizazi cha sasa, kila mwenye uelewa anatakiwa kupinga hali ya namna hii, najua ni kitu kigumu na kitachukua muda ila ipo siku itafika na jamii kubadilika. Tusipochukua hatua na kuendelea kukupambatia stori za namna hii tutakuwa tunaendelea kuwakumbatia watu wenye tabia hizi na kuwatia moyo waendelee na tabia hizi.


  Mungu okoa kizazi chetu,

  Amin.
   
 3. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  Ubarikiwe sana mtumishi!! Maombi yako ni dhati! Ki ukweli inatia maudhi, ndo maana nikiwauli wahusika hawaonagi aibu mbele ya watu wao?? Afadhali umeongezea, basi waƶne aibu hata kwa Mungu aonae sirini!!
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  The world is roten everywhere!
   
 5. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  haya sasa,.....
   
 6. Mc Tilly Chizenga

  Mc Tilly Chizenga JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 3,718
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  HorsePower katoa ufumbuzi wote,hakuna cha kuchangia hapa zaidi ya kumuunga mkono na kuhimizana ktk kufuata na kutekeleza ushauri wake
   
 7. P

  Paul mathew JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nakuunga mkono horse power.
   
 8. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mpaka ameweza gonoka na mwengine tayari kashakudharau....so ata akija back home ni kawaida tuu
   
Loading...