Usalama wa Pesa zako unazoweka Benki

Usalama wa Pesa zako unazoweka Benki

Mwamba028

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2013
Posts
4,649
Reaction score
3,817
Habari zenu Wadau.

Nimekuwa nikijiuliza kuhusu usalama wa fedha za mtu binafsi au kampuni zinazoekwa kwenye akaunti ktk mabenki tofauti hapa nchini.
Endapo labda benki itafilisika au ikaamua kuhamisha matawi yake yote nchini itakuaje na wakati hakuna mkataba wowote unaoingia na benki wakati wa kufungua akaunti kuhusu hali kama hiyo itakapotokea, tena kwenye mabenki wao ndo wanachukua taarifa zako nyiingi wakati wkt wewe huandikiwi hata mkataba wa kuwa utakua unahifadhi pesa zako pale.
Pia kwenye mabenki unapofungua akaunti huambiwi kuhusu makato ya kila mwezi wala ya atm,we unashangaa tu hela zako zinakatwa kidogo kidogo kwa mwezi na pale unapotoa pesa.
Hili nalo vp halihitaji makubaliano au kupewa taarifa kweli?

Nauliza tuu, kama kuna mwenye majibu afunguke
 
Kuhusu kufilisika B.O.T inachukuwa jukumu hilo coz mabenk yte ya biashara lazima yawe na account B.O.T na kuna limit katika mtaji wao uliopo B.O.T so ondoa shaka kwa hilo
 
Na huu ujanja ujanja mara siasa kuingia kwenye hiyo taasisi, hivi ni kweli ikitokea bank ikafilisika, serikali yetu hii itarejesha amana zetu kweli? Narejea mambo kama ya EPA, mafao ya wastaafu mbalimbali wakiwemo wa EA, ambao bila shaka fedha zao zilipitia hukohuko BOT na hadi sasa haijulikani lini watalipwa
 
Unajua kwanini wakinga wengi ni matajiri ? MKINGA haweki hela benki mpaka amalize ghorofa kwanza. Pesa yake inakaa kwenye godoro na ila siku anaiona. BOT ni kitu gani ? wenyewe tu ni wezi. mfano ninao kwani Liyumba alifungwa kwa kuiibia benki na kuna wengi tu wanatumia vifungo. BOT imeajiri vitoto vya makanjanja ambavyo ni incompetent. mimi pesa yangu mvunguni.
 
Mkuu uliyosema ni kweli,nakumbuka ilipofungwa benk ya greenland iliyokuwa maeneo ya posta ambako posta wamefungua tawi la metropoltan,fedha yangu ilifungiwa kwa mwaka mmoja,baada ya hapo tuliitwa na kupewa fedha zetu lkn walikata makato kwa kisingizio cha kuwalipa watumishi waliotuhudumia,binafsi nilishangaa kuona hela yangu imefungiwa mwaka mzima afu nikaishia kukatwa,hivyo hizo story za BOT ni kanjanja kama nyinginezo.
 
Jambo la msingi sana limeongelewa na mleta mada, wenye ujuzi wazidi kutupa info. ..
 
Mbona tunakua wepesi wa kusahau. MERIDIAN BIAO BANK. GREENLAND BANK hizi zote zimeigia mitini mbele ya macho ya BOT. Meridian biao walikua wanatangaza uongo kua wao hutoa interest kila siku mbele ya macho ya BOT. Meridian Biao ilikua haina kwao lkn BOT waliisajili. Mimi huniambii kitu. pesa yangu inakaa chumbani kwangu kama mkinga. Wahindi wenyewe wanaweka asilimia ndogo sana benki za bongo ila mali zao ziko nje. hili halina ubishi.
 
Kuhusu kufilisika B.O.T inachukuwa jukumu hilo coz mabenk yte ya biashara lazima yawe na account B.O.T na kuna limit katika mtaji wao uliopo B.O.T so ondoa shaka kwa hilo

Sasa mambo km hayo ww uliyeeka pesa zako inabidi ujulishwe
 
Mabenki yote / Tanzania ni wezi kazi ya Benki ni kuchukua pesa za watu na kuwakopesha wanaohitaji kwahio ni biashara pesa yako yoyote unayoweka wanaizalisha kwa kuikopesha hivyo basi inabidi kila mwezi au hata wakitaka mwaka wakulipe interest ya kuwasaidia kuzalisha pesa na sio kukukata eti service charge ; sijui ni service gani hio. Mimi niliacha pound tano tu kwenye savings yangu na HSBC UK kurudi hata baada ya mwaka au mwezi unakuta hio pound tano imezaa vijjipennies kidogo lakini huku ukiacha elfu tatu baada ya miezi kumi unakuta una sifuri; sasa sijui hio service wanayokupa ni ya kula pesa zako au sijui ni nini
 
Nilifungua acc stanbic. nikaweka pesa baadae nikatoa zote ikabaki elfu ishirini. baada ya miezi sita wakaniandikia barua eti nadaiwa. nikauliza kulikoni wakasema elfu ishirini ishatumika kama service chg na hilo deni ni service charge ya account ambayo haina pesa. niliwaambia the choice is yours endeleeni kunicharge lkn mlangoni penu hamnioni tena. Ukiweka pesa nyumbani kwako service charge hakuna
 
Yalinikuta exactly. Nikawaambia mnipeleke mahakamani. sijaona upuuzi huo tena. mpango mzima kibubu. Sisi bongo hatujafika stage tuamini benki zetu kiviiiile.
 
Habari zenu Wadau.

Nimekuwa nikijiuliza kuhusu usalama wa fedha za mtu binafsi au kampuni zinazoekwa kwenye akaunti ktk mabenki tofauti hapa nchini.
Endapo labda benki itafilisika au ikaamua kuhamisha matawi yake yote nchini itakuaje na wakati hakuna mkataba wowote unaoingia na benki wakati wa kufungua akaunti kuhusu hali kama hiyo itakapotokea, tena kwenye mabenki wao ndo wanachukua taarifa zako nyiingi wakati wkt wewe huandikiwi hata mkataba wa kuwa utakua unahifadhi pesa zako pale.
Pia kwenye mabenki unapofungua akaunti huambiwi kuhusu makato ya kila mwezi wala ya atm,we unashangaa tu hela zako zinakatwa kidogo kidogo kwa mwezi na pale unapotoa pesa.
Hili nalo vp halihitaji makubaliano au kupewa taarifa kweli?

Nauliza tuu, kama kuna mwenye majibu afunguke

Tena NBC kama siwaelewi vile, mpaka nimeanza kupunguza pesa yangu kule. CRDB wezi pia, sioni Bank ya kuiamini kwa kifupi.
 
Habari zenu Wadau.

Nimekuwa nikijiuliza kuhusu usalama wa fedha za mtu binafsi au kampuni zinazoekwa kwenye akaunti ktk mabenki tofauti hapa nchini.
Endapo labda benki itafilisika au ikaamua kuhamisha matawi yake yote nchini itakuaje na wakati hakuna mkataba wowote unaoingia na benki wakati wa kufungua akaunti kuhusu hali kama hiyo itakapotokea, tena kwenye mabenki wao ndo wanachukua taarifa zako nyiingi wakati wkt wewe huandikiwi hata mkataba wa kuwa utakua unahifadhi pesa zako pale.
Pia kwenye mabenki unapofungua akaunti huambiwi kuhusu makato ya kila mwezi wala ya atm,we unashangaa tu hela zako zinakatwa kidogo kidogo kwa mwezi na pale unapotoa pesa.
Hili nalo vp halihitaji makubaliano au kupewa taarifa kweli?

Nauliza tuu, kama kuna mwenye majibu afunguke
ndugu HII AINA YA MIKATABA KAMA YA BIMA,BANK BAINA YA MTEJA NA BANKI NI STANDARD CONTRACT YAANI WEWE UNAAMUA KUKUBALI AU LA.UNAPOPEWA FOMU ILE NI OFFER YA MKATABA,UKIJAZA NA KURUDISHA NA KUSAINI BASI UNAKUWA MKATABA SASA YAANI OFFER+AGREEMENT.
KUHUSU USALAMA WA PESA ZAKO KUNA MFUKO WA BIMA ZA MABENKI,PIA KUNA MFUKO BOT UNAOSHUGULIKIA KWAMBA KUNA MINIMUM BALANCE INAWEKWA BOT ,NA BOT NDIO WANAOPERATE KILA KITU NA MABENKI NDIO WANAWEKA HELA KULE .INAMAANA BANKI IKIFILISIKA BASI KUNA INSURANCE ALAFU KUNA PROCEDURE ZA KUFILISI ILI WAWEZE KULIPA MADENI YA NJE NA NDANI..WANAHISA KAZI KWAO SASA...
NDOJA WENGINE WATOE MAONI ZAIDI
 
Back
Top Bottom