Usalama wa Pesa zako unazoweka Benki

Usalama wa Pesa zako unazoweka Benki

mbona tunakua wepesi wa kusahau. Meridian biao bank. Greenland bank hizi zote zimeigia mitini mbele ya macho ya bot. Meridian biao walikua wanatangaza uongo kua wao hutoa interest kila siku mbele ya macho ya bot. Meridian biao ilikua haina kwao lkn bot waliisajili. Mimi huniambii kitu. Pesa yangu inakaa chumbani kwangu kama mkinga. Wahindi wenyewe wanaweka asilimia ndogo sana benki za bongo ila mali zao ziko nje. Hili halina ubishi.
wewe pesa zako ni bilioni?kama milioni mia weka ndani tu.wakinga sikuhizi wanaweka bank ndugu wahindi wanabank zao.uwe na ushaidi.
 
Habari zenu Wadau.

Nimekuwa nikijiuliza kuhusu usalama wa fedha za mtu binafsi au kampuni zinazoekwa kwenye akaunti ktk mabenki tofauti hapa nchini.
Endapo labda benki itafilisika au ikaamua kuhamisha matawi yake yote nchini itakuaje na wakati hakuna mkataba wowote unaoingia na benki wakati wa kufungua akaunti kuhusu hali kama hiyo itakapotokea, tena kwenye mabenki wao ndo wanachukua taarifa zako nyiingi wakati wkt wewe huandikiwi hata mkataba wa kuwa utakua unahifadhi pesa zako pale.
Pia kwenye mabenki unapofungua akaunti huambiwi kuhusu makato ya kila mwezi wala ya atm,we unashangaa tu hela zako zinakatwa kidogo kidogo kwa mwezi na pale unapotoa pesa.
Hili nalo vp halihitaji makubaliano au kupewa taarifa kweli?

Nauliza tuu, kama kuna mwenye majibu afunguke

Kuhusu makato ya mwezi na atm bank nyingi hasa za kimataifa za hapa wanatumia bundle charge unakatwa kila mwezi kiasi kadhaa na unaambiwa ila huduma nyingine km atm,sim banking na internet banking ni free.
 
Nilifungua acc stanbic. nikaweka pesa baadae nikatoa zote ikabaki elfu ishirini. baada ya miezi sita wakaniandikia barua eti nadaiwa. nikauliza kulikoni wakasema elfu ishirini ishatumika kama service chg na hilo deni ni service charge ya account ambayo haina pesa. niliwaambia the choice is yours endeleeni kunicharge lkn mlangoni penu hamnioni tena. Ukiweka pesa nyumbani kwako service charge hakuna

Kila bank ina minimum operating balance uwezi mpa mtu akutunzie pesa bure... Minimum operating bank kwa kila bank lazima waweke ata ukifungua ya account ya akiba (saving) lazima uache elfu kumi au ishirini.. Hua aitoki
 
Tena NBC kama siwaelewi vile, mpaka nimeanza kupunguza pesa yangu kule. CRDB wezi pia, sioni Bank ya kuiamini kwa kifupi.

ACCESS bank wanatangaza hawakati, hata ukiacha buku utaikuta hivyo hivyo. Ila sina uhakika maana sijawahi kuacha zaidi ya elfu 5 hivi karibuni
 
Kuhusu taarifa za account ni uvivu wetu tu watz kufatilia bank zina account tofaut zaidi ya 10 ukienda kichwakichwa utaweza funguliwa acc isiyo type yako...

Kila bank ina tariff guide za aina ya acc na makato na hata fomu za kufungua acc zina terms and condtn ambazo unatakiwa usome ndipo usign...

Ila sasaaa mtu akifika counter anaacha picha na kusign na kupeleka barua basi, aulizii more detail kuwa nini anachotaka matokeo yake bank officer anamfungulia acc yenye makato makubwa kwa faida yao bank na hasara kwake mteja kwa uvivu wake wa kuuliza au kupitia tarrif guide kujua bank ipi ni cheap.
 
Kuhusu makato ya mwezi na atm bank nyingi hasa za kimataifa za hapa wanatumia bundle charge unakatwa kila mwezi kiasi kadhaa na unaambiwa ila huduma nyingine km atm,sim banking na internet banking ni free.

Sikubaliani na wewe, atm unakatwa mia tano na kupitia simu unakatwa mia tatu. Hiyo ni benki ya taifa ya makabwela, NMB
 
Sikubaliani na wewe, atm unakatwa mia tano na kupitia simu unakatwa mia tatu. Hiyo ni benki ya taifa ya makabwela, NMB

Soma vizuri ni bank za kimataifa Stanbic,Standard charter, Barclays n.k hizo bank zenu za waalimu nmb sijui mtajua wenyewe na wanaiba vizuri maana hawasemi ukweli kuhusu makato yao.. Nilisha ziacha muda sasa
 
u
Habari zenu Wadau.

Nimekuwa nikijiuliza kuhusu usalama wa fedha za mtu binafsi au kampuni zinazoekwa kwenye akaunti ktk mabenki tofauti hapa nchini.
Endapo labda benki itafilisika au ikaamua kuhamisha matawi yake yote nchini itakuaje na wakati hakuna mkataba wowote unaoingia na benki wakati wa kufungua akaunti kuhusu hali kama hiyo itakapotokea, tena kwenye mabenki wao ndo wanachukua taarifa zako nyiingi wakati wkt wewe huandikiwi hata mkataba wa kuwa utakua unahifadhi pesa zako pale.
Pia kwenye mabenki unapofungua akaunti huambiwi kuhusu makato ya kila mwezi wala ya atm,we unashangaa tu hela zako zinakatwa kidogo kidogo kwa mwezi na pale unapotoa pesa.
Hili nalo vp halihitaji makubaliano au kupewa taarifa kweli?

Nauliza tuu, kama kuna mwenye majibu afunguke

cha msingi huwe unatunza vizuri LISITI
 
Mabenki yote / Tanzania ni wezi kazi ya Benki ni kuchukua pesa za watu na kuwakopesha wanaohitaji kwahio ni biashara pesa yako yoyote unayoweka wanaizalisha kwa kuikopesha hivyo basi inabidi kila mwezi au hata wakitaka mwaka wakulipe interest ya kuwasaidia kuzalisha pesa na sio kukukata eti service charge ; sijui ni service gani hio. Mimi niliacha pound tano tu kwenye savings yangu na HSBC UK kurudi hata baada ya mwaka au mwezi unakuta hio pound tano imezaa vijjipennies kidogo lakini huku ukiacha elfu tatu baada ya miezi kumi unakuta una sifuri; sasa sijui hio service wanayokupa ni ya kula pesa zako au sijui ni nini

Jamaa wanatuibia sana,,mi natafuta njia ya kuwakwepa aisee,,hao HSBC ni benki pia au?
 
Jamaa wanatuibia sana,,mi natafuta njia ya kuwakwepa aisee,,hao HSBC ni benki pia au?

Yes HSBC ni Banki ila ipo UK point yangu ilikuwa kwamba huu wizi wa mchana kweupe haupo nchi nyingine mfano England hakuna huu upuuzi wa Service Charges.., ila kuna mdau aliniambia hata FBME nao hawakati
 
Kuhusu makato ya mwezi na atm bank nyingi hasa za kimataifa za hapa wanatumia bundle charge unakatwa kila mwezi kiasi kadhaa na unaambiwa ila huduma nyingine km atm,sim banking na internet banking ni free.

Simbanking sio free mama, nlifanya transaction na makato yao yanakaribiana na hiz m pesa
 
Have you ever think of Mpesa,Tigo pesa usalama wake? Kuna tofaut gan na bank.. Na utakuta mtu anaweka hata 5mil like serious??????
 
Mke wangu aliibiwa laki 2 tumefatilia mpaka bas,,ni hii bank ya wafanyakazi wa umma.
 
Simbanking sio free mama, nlifanya transaction na makato yao yanakaribiana na hiz m pesa

Tena kama sio mfuatiliaji kuna siku utashangaa huna pesa kwenye akaunti. Ila ukiwa unapiga piga simu mara kadhaa kuulizia transactions zinaendaje wanakuwa waogo kucheza na akaunti yako.
 
Soma vizuri ni bank za kimataifa Stanbic,Standard charter, Barclays n.k hizo bank zenu za waalimu nmb sijui mtajua wenyewe na wanaiba vizuri maana hawasemi ukweli kuhusu makato yao.. Nilisha ziacha muda sasa

Kumbe nami ni mwalimu? Waniingiziage na hako ka laki moja na nusu kangu kama mshahara basi. By the way kuweka pesa ndogo benki hasara ni kubwa kuliko faida, na kama pesa ni nyingi basi ziweke katika fixed deposit accounts na uweke katika benki mbalimbali
 
Tena NBC kama siwaelewi vile, mpaka nimeanza kupunguza pesa yangu kule. CRDB wezi pia, sioni Bank ya kuiamini kwa kifupi.

Kwanza nimpongeze mtoa mada kwa mada nzuri,kwakweli sijui ni benki gani ambayo hakuna wizi nimeibiwa pesa kwenue a/c yangu benki ya Posta mwezi August mwaka jana pamoja na kuripoti wamenisumbua sana hadi ninapoandika hapa sina matumaini ya kupata pesa zangu!kwa hali hiyo bora nijiwekee nyumbani kwangu!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ninachokiona hapa watu wengi bado hawana uelewa wa benki zinaendeshwaje
1. Benki yoyote ya biashara lazima isajiliwe BOT
2. Kila benki iliyosajiliwa lazima iwe na kiwango cha chini cha mtaji (minimum capital balance) BOT ambacho kwa sasa ni ni shilingi bilioni 15.
3. BOT ndio wanaosimamia benki zote Tanzania
4. Kila benki ina aina za akaunti zake (account products) kulingana na mahitaji mbalimbali ya wateja.
5. Kuna akaunti zisizo na makato kabisa, akaunti zenye riba, akaunti zenye makato, akaunti za muda maalamu n.k
6. Mteja anatakiwa kuuliza masharti ya kila akaunti ili aweze kuridhika na akaunti anayoitaka.
7. Kila benki ina kipeperushi cha gharama/makato/ada/riba ya kila huduma inayotoa, hivyo mteja anapaswa kusoma na kuelewa.
8. Benki zote zinatakiwa na kuwa na sehemu mbadala ya taarifa zao (Disaster recovery site) pindi ikitokea janga lolote taarifa zipatikane.

NB:
Kuna watu ambao wanafanya biashara ya kuweka pesa benki na kupata faida kupitia akaunti za muda maalum (fixed deposit account). Mfano mtu anaweza kuweka milioni 200 kwa miezi 12 kwa riba ya 14%. Ikiisha miezi 12 anapata faida ya milioni 28. Kwa hiyo kikubwa ni kujitahidi kupata taarifa za kutosha pindi tunapoenda kufungua akaunti ili tujue nini tutafaidika na hiyo akaunti. Wengi wetu tunazijua akaunti za akiba tu (saving account) ambazo mara nyingi zinakuwa na makato makubwa na ndiyo yanayotuumiza.
 
Tena kama sio mfuatiliaji kuna siku utashangaa huna pesa kwenye akaunti. Ila ukiwa unapiga piga simu mara kadhaa kuulizia transactions zinaendaje wanakuwa waogo kucheza na akaunti yako.

Sio bank zote kuna bank zinatoa sms alert za salio lako kila mwisho wa wiki na mwezi na wanatuma bank statement kwa e-statement kwenye email kama unayo.. Hiyo issue ka kupiga simu ili uambiwe salio ni impossible and i wont happen.. How sure kuwa uliyepiga ni mhusika wa acc ndo maana ukitaka balance kuna vifomu vidogo pale bank unajaza ac number uangaliziwe salio la unaenda ATM na kwa wale wanao pata sms alert pia zinaonyesha namba za mwisho tu za acc sio yote, yote hii ni kwa security reason.
 
Back
Top Bottom