Usalama wa nchi hautangazwi kwenye TV wala Magazeti

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,534
Mods nawaomba sana pls huu Uzi muuache ujitegemee wenyewe kwa Sababu una maudhui tofauti.

Waziri Lugola ameita media na kuonya mtu yeyote asije kujaribu kuwaonyesha wawekezaji wala kuwatisha kuwa "eti Tanzania hakuna amani".

Kauli ya Lugola imejaa kichekesho kweli,amani ya Taifa lolote hujiuza yenyewe Duniani.

Leo hii huwezi kumwambia mtu eti Syria kuna amani akawekeze,Dunia nzima inajua kuwa Syria haikaliki.

Tukio la kutekwa MO Dunia nzima inajua,sasa hakuna mtu wa kuwashawishi au kuwatisha wawekezaji kuhusu kuwekeza Tanzania ama la,wao ndo wanaamua kulingana na taswira ya nchi .

Ni vyema Lugola angetuambia serikali imefikia hatua gani ktk kumtafuta MO na siyo kuongea mambo yasiyofanana na uhalisia.
 
Ccm wanadhani hadi leo dunia ni kama ile ya kipindi kile wakati kulikuwa na absolute control ya vyombo vya habari na contents za habari. Wanadhani wanaweza kudhibiti mtu asipate habari na kuwa watu toka nje ya nchi hawana sources za habari tofauti na magazeti ya uhuru, daily news na TBC. Ndio maana hadi leo hii utakuta tangazo linalokataza kupiga picha mahali as if mtu anahitaji kuwepo hapo physically ili apige picha.
 
huu utawala haramu ungedumisha amani ya kweli wanayoihubiri..
Huyu kichwa maji hajui kwamba kutoa vitisho ndio anaizika amani ya nchi iliyopo ICU !?
Kama una rafiki yako anataka kuja kuwekeza Tanzania mwambie..
"MY FRIEND IF YOU MISS KIDNAPPING WELCOME TO TANZANIA"
 
Ccm wanadhani hadi leo dunia ni kama ile ya kipindi kile wakati kulikuwa na absolute control ya vyombo vya habari na contents za habari. Wanadhani wanaweza kudhibiti mtu asipate habari na kuwa watu toka nje ya nchi hawana sources za habari tofauti na magazeti ya uhuru, daily news na TBC. Ndio maana hadi leo hii utakuta tangazo linalokataza kupiga picha mahali as if mtu anahitaji kuwepo hapo physically ili apige picha.
Hakika Shetani hana rafiki ! Mchango wa MO kwa ccm unazidi michango yote ya viongozi wa awamu ya 5 , wakiikusanya pamoja haifiki hata nusu yake ! leo anakejeliwa na Lugola , Koplo asiye na mchango wowote !
 
Back
Top Bottom