Usalama barabarani, ukiona bodaboda kaning'iniza sendo na kitambaa kwenye exhaust usipande

Kajeba

JF-Expert Member
Oct 15, 2020
826
1,965
Hii ni kwa usalama wako!
Kuna ajali na vifo vingine vinapangwa na wanadamu wenyewe kwa kutokujali na kuangalia usalama wa barabarani

Kiukweli dereva bodaboda wengi ndani ya jiji la Dar es salaam hawajali usalma wao kabisa, hii imepelekea vifo na ulemavu wa kudumu kwa kundi hili na abiria wengi wanaotumia usafiri huu wa haraka ndani ya jiji

Napenda kutoa angalizo kwa wale wanaotumia usafiri wa bodaboda kuwa makini pindi wachaguapo dereva wa kuwasafirisha
Hakika usimchague bodaboda ambaye amevaa sendo zile wanaendesha pikipiki huku wameining'iniza yaani haijafit mguu vizuri
Pia wale boda boda waliofunga vitambaa kwenye exsozi(kitolea moshi) tuwaepuke

Dereva boda wa aina hiyo wako rafu sana hawajiangalii wala kuthamini uhai, wanatembea mwendo hatari

usije kusema hatukukuambia
 
Naongezea

Warning!.....

TAFADHALI SANA WATANZANIA
___________________________
1.msipande boda boda yoyote isiyokuwa na side mirror,

2. Usipande boda yenye Dereva mwenye afya dhaifu kuliko wewe abiria.

3. Kabla ya kupanda muombe umuangalie usoni , km amevaa helmet mwambie avue kwanza umuangalie vizuri, akikataa chukua boda nyingine.

4. Usipande boda ambae dereva wake ni mchafu sana..... it's a warning sign kwamba ni careless.

Mwisho,
...... jaribu kumsemesha maneno mawili matatu kabla hamjaondoka.....kumpima kama hajalewa, siku hizi kuna pombe za kwenye chupa bei km viroba.

Nishukuru siku nyingine.
 
Kuna siku nilipita kijiweni vijana wakachangamka nikaona hawa wanaochangamka sio, nikachagua dereva aliekuwa kakaa kimya hana neno, nashukuru ilikua ni safari fupi....nishakaa kwa chuma yule dereva akageuka kunisemesha aseeeeeee ndio maana alikua kimya yani nilihisi nimemwagiwa ji-konyagi usoni yule atakua ni mlevi mbwa!!!
 
download.jpeg
 
Never judge a book by its cover
 
Hii ni kwa usalama wako!
Kuna ajali na vifo vingine vinapangwa na wanadamu wenyewe kwa kutokujali na kuangalia usalama wa barabarani

Kiukweli dereva bodaboda wengi ndani ya jiji la Dar es salaam hawajali usalma wao kabisa, hii imepelekea vifo na ulemavu wa kudumu kwa kundi hili na abiria wengi wanaotumia usafiri huu wa haraka ndani ya jiji

Napenda kutoa angalizo kwa wale wanaotumia usafiri wa bodaboda kuwa makini pindi wachaguapo dereva wa kuwasafirisha
Hakika usimchague bodaboda ambaye amevaa sendo zile wanaendesha pikipiki huku wameining'iniza yaani haijafit mguu vizuri
Pia wale boda boda waliofunga vitambaa kwenye exsozi(kitolea moshi) tuwaepuke

Dereva boda wa aina hiyo wako rafu sana hawajiangalii wala kuthamini uhai, wanatembea mwendo hatari

usije kusema hatukukuambia
Hakika usimchague bodaboda ambaye amevaa sendo zile wanaendesha pikipiki huku wameining'iniza yaani haijafit mguu vizuri

Hata ukaaji wao kwenye kiti sio mzuri wanakaa uoande uoande! wahuni hawa! sasa jiulize kama kwenye kiti tu hawezi kukaa vizuri je hiyo boda boda ataendesha vizuri?
 
Back
Top Bottom