Usalama barabarani, ukiona bodaboda kaning'iniza sendo na kitambaa kwenye exhaust usipande

Pole. Mimi kuna siku watoto waliachwa na school bus, sasa boda ninaemtumia mimi binafsi akawa hapatikani ila kuna mwingine mtu mzima kiasi nikawa namfwata ili awapeleke watoto kumbe amelewa hataru alikua ameegemea nguzo ile kupiga tu hatua chini amelewa hajiwezi kumbe kugemea ile nguzo ni balance alikua anatafuta nikasema asante Mungu maana nadhani leo ningekua naongea mengine kuhusu watoto
Kumpandisha mtoto boda boda ni kuingilia uhuru wake sababu hajitambui.

Bora bajaji mara 67
 
Kuna siku nilipita kijiweni vijana wakachangamka nikaona hawa wanaochangamka sio, nikachagua dereva aliekuwa kakaa kimya hana neno, nashukuru ilikua ni safari fupi....nishakaa kwa chuma yule dereva akageuka kunisemesha aseeeeeee ndio maana alikua kimya yani nilihisi nimemwagiwa ji-konyagi usoni yule atakua ni mlevi mbwa!!!
! Uandishi huu chumvi chumvi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumpandisha mtoto boda boda ni kuingilia uhuru wake sababu hajitambui.

Bora bajaji mara 67
Ni kweli japo umbali haukua mrefu sana japo haidefine ajali kutotokea. Najua fika nilifanya makosa sema mwenyez Mungu alininusuru
 
Back
Top Bottom