Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Baadhi ya madereva wa usafiri huu wanatajwa kuwa ni miongoni mwa wale wasiozijua au wanaozivunja sheria za usalama barabarani hata kusababisha maafa kwa abiria na watumiaji wengineo wa barabara.
Limekuwa kama ni jambo la kawaida, kuwakuta baadhi ya dereva wa bodaboda wanaendesha chombo hicho cha moto huku wakiwa wamevaa kandambili mguuni au malapa jambo ambalo si salama kwao na abiria aliyembeba hata kidogo.
Ukweli ni kwamba, uvaaji wa kandambili unaweza kusababisha ajali kwa muhusika kuteleza bila ya kutarajia, kwa sababu muda wowote yaweza kuvuka au kukwama katika pikipiki na kuchangia ajali isiyotarajiwa.
Ikumbukwe kuwa, sheria na kanuni za usalama barabarani, zinakataza kabisa waendesha bodaboda kuvaa kandambili badala yake wavae viatu ili kuwafaya wamudu kukabiliana na changamoto yoyote ikijitokeza.
Si kandambili pekee, utakuta dereva huyohuyo kavaa koti jepesi, lililochanika, lisilo na vifungo wala zipu, upepo ukija kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka nalo, nayo hii ni hatari.
Ni hatari kivipi, wakati dereva anaendesha bodaboda ni kwamba upepo mkali unapovuma kwa namna yoyote ile unaweza kusababisha koti kumfunika usoni hivyo kukosa uelekeo na matokeo yake ni ajali ambayo ingeweza kuepukika kama tu dereva huyo angekuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Si hayo tu, hata mavazi ya baadhi yao hayaridhishi aslani. Ni machafu, tena katika kipindi hiki cha mvua abiria ujiandae kulowesha nguo zako pale tu utakapopanda pikipiki na kugusana na dereva huyu. Kimsingi ni kwamba hawajali mteja kuwa ni mfalme hata wao hawajijali. Yaani kwao palipo na mvua yeye kuloana wanachukulia kuwa ni kawaida.
Achilia mbali kupuuza sheria za usalama barabarani, kwani inaweza kuwa hatari hasa kwa abiria na dereva mwenyewe.
Madereva wanapuuza kanuni na sheria za usalama barabarani. Yaani ni kwamba palipowaka taa nyekundu za kuongozea magari wao hupita, pembeni au katikati ya barabara kwa kupenya katika namna ya hatari, pia huvuka kwenye kivuko cha watembea kwa mguu iwapo magari yamesimama kupisha watu wavuke wao hawajali, hupita kwa kasi.
Tena usipokuwa makini barabarani, bodaboda zinaweza kukusababishia ajali kuliko hata magari ambayo yanaogopwa na wengi. Hii ndiyo hali halisi ya usafiri wa bodaboda katika zama hizi.
Ukienda katika Taasisi ya Mifupa (MOI), takwimu za ajali zote za barabarani, bodaboda zinaongoza kwa kusababisha ulemavu wa kudumu kwa watu wengi ikiwa pamoja na vifo.
Baadhi ya madereva hawa, hawatii sheria, hawavai kofia ngumu, wachafu, kandambili mguuni pia hodari kuwachomekea madereva wa gari na kuondoka katika namna ya hatari. Wanacheza na hatari bila ya hofu yoyote ile.
Mtaani stori za vijiweni au katika daladala ni pale wanaposhuhudia dereva wa bodaboda kafanya makosa barabarani, wengine huthubutu kutamka ya kwamba ‘MOI kumejaa na vyuma vimeisha, saa hizi ni kukata tu viungo vya mwili ’.
Ni kauli zisizo nzuri, lakini zinatokana na baadhi ya madereva wa bodaboda wasio na chembe ya woga kwa yeyote wawapo barabarani. Yaani, hawamuogopi askari wa usalama barabarani wala sheria. Cha ajabu, hata abiria aliyempakia hamuogopi, bila kujua abiria huyo atakuwa anafanya kazi gani? Yawezekana hata anaweza akamchukulia hatua kali kwa mujibu wa kisheria.
Wao muda wote ni kama wana haraka na kutaka kuwahi kufika waendako, bila kujali usalama wake, abiria, watembea kwa miguu au watumiaji wengineo wa barabara.
Nimekuwa nikijiuliza kuhusu madereva hawa, wanamuogopa nani? Hii ni kwa sababu wanaongezeka kwa kasi mijini na wengi wao ni vijana wengi waliokosa ajira rasmi ambao wamejiajiri katika kazi hii ambayo kwa sasa inazalisha walemavu na vifo vingi.
Inavyoonekana ni kwamba, askari wa usalama barabarani inawawia vigumu kuwakamata madereva hawa, kwani wakijua wameharibu mbele ya askari, ni kwamba wako radhi kubadili mwelekeo na kukimbia ili asikamatwe.
Ama sivyo, wakitaka kuwakamata wawe askari zaidi ya mmoja. Madereva wa bodaboda kinachotakiwa kwao ni kutii sheria na kuipenda kazi yao kwa kujiweka safi ikiwamo kuvaa viatu ikiwezekana hata sare kama inavyofanyika kwa baadhi ya vijiwe mnavyovitambua.
Niwape pongezi madereva kama hawa, ambao katika baadhi ya vituo wamejitambua na kuvaa viakisi mwanga hali inayofanya hata kama ni usiku au akiwa mbali mtumiaji barabara mwingine humuona na kuondoa hatari yeyote.
Tunafahamu umuhimu wa usafiri huu kwamba ni ajira nzuri kwa vijana, ambao zamani walikaa kijiweni bure, iheshimiwe.
Kwa namna yoyote ile, madereva wa bodaboda wanatakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani, ili kuhakikisha kuwa maisha yanakuwa hayana mashaka hata chembe.
Chanzo: Nipashe