Usajili wa ‘Kanisa la Neema’ uchunguzwe

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,402
19,070
Siandiki ili kupinga uanzishwaji wa makanisa, naandika jambo ambalo kama halitashughulikiwa mapema, kuna siku litaleta matatizo, tena yawezekana yakawa matatizo makubwa sana.

KANISA LA NEEMA la mume wake na grace zoazoa vipodozi, limekuwa kero, linatukana na kupotosha Biblia na amekuwa akigombana na wachungaji wote Tanzania, sema tu kwasababu hawaji hewani kuongea, ila kuna kitu kinafukuta ndani kwa ndani ambacho kinatakiwa kupewa dawa urgently.

Tanzania kuna uhuru wa kuabudu, as long as umefuata sheria na miongozo iliyowekwa. Jambo hili limekuwa limechukuliwa kama uchochoro kwa matapeli wengi kukusanya watu ili aidha kujipatia utajiri kutoka kwao, au kwa malengo yao yoyote wayajuayo kwa kigezo kwamba Serikali haitakiwi kuingilia kati.

Majority ya victims, ni wanawake na watu masikini na wasiosoma...those people who have been stricken with problems na wanaenda kwao kama njia ya kutafuta msaada, badala yake wao wanatake advatage kuwafanya kitega uchumi.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI
1. Kanisa la Kibwetele lilianza hivihivi, mwisho wa siku aliua watu zaidi ya 100 Uganda

2. Tuhakikishe Makanisa yanafunguliwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria. asiyefuata huo utaratibu, ashughulikiwe.

3. hata yale makanisa ambayo tayari yameshapewa vibali, yachunguzwe kuona kama wanacomply.

4. Viongozi wengine wa dini kwenye kamati zao wahusishwe katika kila kada. mfn. Wapentecost wanao umoja wao, waprotestant wengine wanao umoja wao, katholic etc, kama mtu hayupo kwenye aina hizo zote za Makanisa, basi aeleze yeye kanisa lake ni la aina gani ili asije kuleta migogoro isiyo ya lazima.

5. Kuna uzembe na rushwa nyingi sana zinafanyika kwenye ofisi ya usajili wa haya makanisa. mfn. haiji kichwani Nabii Suguye, amekuwa na kanisa miaka kadhaa yote hiyo, hadi ameanza kuomba nywele za utosini, kucha kidole kidogo n.k ilikuwa bado kidogo aagize walete nywele za sehemu za siri manake alishaanza kufundisha namna ya kufanya ngono madhabahuni. hapo ndio wakashtuka, muda wote huo kumbe kanisa lake halikuwa na usajili. INAKUWAJE MIAKA YOTE HIYO MTU ANAOPERATE KANISA BILA USAJILI?

6. kuna kanisa moja linaitwa KANISA LA NEEMA, ni la mzee wa Neema. huyu ni mme wake yule grace zoazoa anayetengeneza sabuni na vipodozi bila kuwa na elimu yeyote ya kemikali. Wakristo karibia wote Tanzania wamekuwa wakimlalamikia huyu mtu kwasababu mahubiri yake yote, ni kupindua Biblia hadi haijulikani kama yeye ni Mkristo au wa dini gani. amefungua pia tv, na anayo night club kama kanisa. ni wazi yeye anasema sio mpentecost, sio mkatoliki, sio wa dhehemu lolote, SASA HATUJUI AMEJISAJILI KWENU KAMA NANI. mtu huyu anakwaza ukristo, ana potosha mengi ambayo tunaogopa kuna siku isijetokea watu wasio na Mungu moyoni wakamdhuru, na pia anakosesha sana amani katikati ya watu kwasababu ya mafundisho yake. tunaomba chunguzwe ili kuona kama ana elimu yeyote ya dini, ametumwa na nani manake hadi anamiliki television ya TOP PLUS anagarimia vipi n.k. ni ushauri tu.

7. Tunaomba Serikali pamoja na kuwapa vibali/usajili, iwaangalie kwa jicho la karibu hao mitume na manabii wa kisasa, hao wanaouza mafuta, maji nk. wanafanya biashara kama biashara zingine tu kwa Jina la dini. iangalie usajili wao, hao kina mwamposa, ngurumo ya upako wanaogawa pesa hata hazijulikani zinatoka wapi, mzee wa upako na wengine wengi. HIVI KWELI HAWA WAMESAJILIWA?

8. kama Nabii Suguye, mzee wa ibada za nywele na kucha, amefungiwa kanisa hadi arekebishe usajili wake, ni kwali kwamba hao mitume wengine ambao ni contraversual wamesajili makanisa yao? au kwasababu wana pesa kama kina mwamposa?.

9. kama suguye aliexist miaka yote hiyo, tunajuaje kama hawapo wengine ambao anaamka tu asubuhi anaanzisha kanisa na kukusanya hela kwa maskini? bila hata kupitia serikalini.

Mambo haya nimeandika wengine wanaweza kufikiri nina bifu nao, sina, ila ni alart tu kwa serikali, isijekuja kushtuka shuka kukiwa kumekucha.

Wasalaam!
 
imagine leo mtu anasimama anaasema, BIBLIA NI KITABU TU kama vitabu vingine. anachukua kil akilicho kwenye Biblia, anageuza kuongea kinyume chake na anasambaza kwa tv. haya mambo yanakwaza sana Wakristo, kupita kiasi. hadi wamemtungia jina kuwa anaitwa MPINGA KRISTO. lakini serikali bado tu inamwangalia mtu aliyejifanya anamhubiri Kristo lakini anahubiri upinga Kristo.
 
Utapeli upo kila kona hata huko unako sali kuna utapeli pia,achakuteseka na watu mind your our business.

Waumini wakianza kuyakimbia makanisa yenu yaliyopoa kiroho na kwenda kwenye makanisa yenye upako sadaka zenu zina pungua na kuanzisha bifu. Hizo conflict of interest baina yenu pambaneni nazo wenyewe.
 
hamkatazwi kufungua makanisa hayo ya ajabu, hoja yangu ipo kwenye usajili, muwe mmefuata taratibu. hata kibwetele alikuwa na waumini ila serikali ya uganda ilipolalaa ilikuja kufukua tu maiti. mwenye akili ameshaona hili jambo ninaloongea kama la mantiki au la, na ni kwaajili ya kuokoa watu masikini wanaodanganywa na kutapeliwa, nabii anachorwa hadi tatoo, nabii anaendesha gari ya mil.300 kwa sadaka za mtua mbaye amekopa nauli aje kanisani. kumbe pamoja na yote hayo, hajasajili wala nini iyo cult yake. si bore msajili tu ili mjulikane kisheria?
 
Utapeli upo kila kona hata huko unako sali kuna utapeli pia,achakuteseka na watu mind your our business.

Waumini wakianza kuyakimbia makanisa yenu yaliyopoa kiroho na kwenda kwenye makanisa yenye upako sadaka zenu zina pungua na kuanzisha bifu. Hizo conflict of interest baina yenu pambaneni nazo wenyewe.

"Waumini wakianza kuyakimbia makanisa yenu yaliyopoa kiroho na kwenda kwenye makanisa yenye upako sadaka zenu zina pungua na kuanzisha bifu. Hizo conflict of interest baina yenu pambaneni nazo wenyewe." 😀😀
 
Mwenye kanisa, elimu ya chini ni degree ya Theology kutoka chuo kinachotambulika, ikiwezekana na somo la falsafa. Tuige mfano wa Rwanda.
hilo limeshawekwa, hapa unatakiwa tu kuwa na cheti kinachoonyesha umesomea hiyo dini, lakini kuna ufisadi mwingi hata kwenye vyuo vya dini, wanauza vyeti sana. though hapa ni walau diploma kama sikosei. ninachowaasa hao watu wa usajili, VYUO VYOTE VYA BIBLIA viingizwe TCU, na mtu akileta cheti, wakichunguze kuona kama kweli alifika chuo au amenunua cheti. wana pesa nyingi sana walizokusanya toka kwa waumini masikini, ndio maana wanaishi maisha ya kifahari.ni nabii gani maarufu ambaye hana nyumba masaki au mbezi beach n.k? wakati waumini wamepauka hawana kitu, na anawahubiria nywele na kucha. kuna siku tu hiyo ofisi ya usajili itafumuliwa na kuna watu watawajibishwa. ni suala la muda tu.
 
Ni wivu tuu.
ni wivu gani sasa, kweli kuna mtu hajaona kwa macho yake namna watanzania masikini wanavyopelekeshwa kama mang'ombe kwa nabii, nabii mwenyewe anatembelea v8 na anatandikiwa nguo apite asikanyage chini, kwenda kwa nabii tu wamekopa nauli, alafu yeye anafanya kazi ya kuwakamua tu. serikali inatakiwa kudhibiti utapeli uwe wa kanisani, msikiniti au popote, haiwezi kukaa kimya wakati hata mjinga anajua kuwa raia wake wanatapeliwa.
 
ukijua kuwa kamata wajinga kwenye imani ata ukiwaambia fanyeni hivi mtafanya hivi
imagine mtu anaambiwa akalete nywele za utosini na kucha za kidole kidogo, na anaaminishwa hilo ni kanisa. sipingi kufanya hivyo kama ni usajili wa mganga wa kienyeji, ni pale anaposajili kama kanisa lakini anafanya shughuli za mganga wa kienyeji. usajili uwe wazi.
 
Nakubaliana na mtoa mada mia kwa mia. Makanisa yamechipuka kama uyoga katika nchi hii. Nimekuwa nikifuatilia na kuona ni biashara tu ya kujipatia utajiri kwa hao wanaojiita manabii. Hakuna masomo ya dini wala masomo ya biblia. Lete sadaka ili tungarishe nyota yako na utajirike, tena sadaka za mamilioni. Nabii moja anasema ukitoa hela nyingi utapata huduma ya VIP !!! Upako wa VIP!!! Uko wapi ule usemi wa ulipata bure toa bure? Je serikali/TRA inachunguza mahesabu yao na kuona kama wanalipa kodi kwa mujibu wa sheria?
 
huyo ni nabii Mkenya, ana tv ya utajirisho, yaani mkenya kaja kupiga pesa hapa Tanzania anaitwa Peter Nyaga. na serikali kweli iendelee kuangalia tu? kweli?
 
Siandiki ili kupinga uanzishwaji wa makanisa, naandika jambo ambalo kama halitashughulikiwa mapema, kuna siku litaleta matatizo, tena yawezekana yakawa matatizo makubwa sana.

KANISA LA NEEMA la mume wake na grace zoazoa vipodozi, limekuwa kero, linatukana na kupotosha Biblia na amekuwa akigombana na wachungaji wote Tanzania, sema tu kwasababu hawaji hewani kuongea, ila kuna kitu kinafukuta ndani kwa ndani ambacho kinatakiwa kupewa dawa urgently.

Tanzania kuna uhuru wa kuabudu, as long as umefuata sheria na miongozo iliyowekwa. Jambo hili limekuwa limechukuliwa kama uchochoro kwa matapeli wengi kukusanya watu ili aidha kujipatia utajiri kutoka kwao, au kwa malengo yao yoyote wayajuayo kwa kigezo kwamba Serikali haitakiwi kuingilia kati.

Majority ya victims, ni wanawake na watu masikini na wasiosoma...those people who have been stricken with problems na wanaenda kwao kama njia ya kutafuta msaada, badala yake wao wanatake advatage kuwafanya kitega uchumi.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI
1. Kanisa la Kibwetele lilianza hivihivi, mwisho wa siku aliua watu zaidi ya 100 Uganda

2. Tuhakikishe Makanisa yanafunguliwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria. asiyefuata huo utaratibu, ashughulikiwe.

3. hata yale makanisa ambayo tayari yameshapewa vibali, yachunguzwe kuona kama wanacomply.

4. Viongozi wengine wa dini kwenye kamati zao wahusishwe katika kila kada. mfn. Wapentecost wanao umoja wao, waprotestant wengine wanao umoja wao, katholic etc, kama mtu hayupo kwenye aina hizo zote za Makanisa, basi aeleze yeye kanisa lake ni la aina gani ili asije kuleta migogoro isiyo ya lazima.

5. Kuna uzembe na rushwa nyingi sana zinafanyika kwenye ofisi ya usajili wa haya makanisa. mfn. haiji kichwani Nabii Suguye, amekuwa na kanisa miaka kadhaa yote hiyo, hadi ameanza kuomba nywele za utosini, kucha kidole kidogo n.k ilikuwa bado kidogo aagize walete nywele za sehemu za siri manake alishaanza kufundisha namna ya kufanya ngono madhabahuni. hapo ndio wakashtuka, muda wote huo kumbe kanisa lake halikuwa na usajili. INAKUWAJE MIAKA YOTE HIYO MTU ANAOPERATE KANISA BILA USAJILI?

6. kuna kanisa moja linaitwa KANISA LA NEEMA, ni la mzee wa Neema. huyu ni mme wake yule grace zoazoa anayetengeneza sabuni na vipodozi bila kuwa na elimu yeyote ya kemikali. Wakristo karibia wote Tanzania wamekuwa wakimlalamikia huyu mtu kwasababu mahubiri yake yote, ni kupindua Biblia hadi haijulikani kama yeye ni Mkristo au wa dini gani. amefungua pia tv, na anayo night club kama kanisa. ni wazi yeye anasema sio mpentecost, sio mkatoliki, sio wa dhehemu lolote, SASA HATUJUI AMEJISAJILI KWENU KAMA NANI. mtu huyu anakwaza ukristo, ana potosha mengi ambayo tunaogopa kuna siku isijetokea watu wasio na Mungu moyoni wakamdhuru, na pia anakosesha sana amani katikati ya watu kwasababu ya mafundisho yake. tunaomba chunguzwe ili kuona kama ana elimu yeyote ya dini, ametumwa na nani manake hadi anamiliki television ya TOP PLUS anagarimia vipi n.k. ni ushauri tu.

7. Tunaomba Serikali pamoja na kuwapa vibali/usajili, iwaangalie kwa jicho la karibu hao mitume na manabii wa kisasa, hao wanaouza mafuta, maji nk. wanafanya biashara kama biashara zingine tu kwa Jina la dini. iangalie usajili wao, hao kina mwamposa, ngurumo ya upako wanaogawa pesa hata hazijulikani zinatoka wapi, mzee wa upako na wengine wengi. HIVI KWELI HAWA WAMESAJILIWA?

8. kama Nabii Suguye, mzee wa ibada za nywele na kucha, amefungiwa kanisa hadi arekebishe usajili wake, ni kwali kwamba hao mitume wengine ambao ni contraversual wamesajili makanisa yao? au kwasababu wana pesa kama kina mwamposa?.

9. kama suguye aliexist miaka yote hiyo, tunajuaje kama hawapo wengine ambao anaamka tu asubuhi anaanzisha kanisa na kukusanya hela kwa maskini? bila hata kupitia serikalini.

Mambo haya nimeandika wengine wanaweza kufikiri nina bifu nao, sina, ila ni alart tu kwa serikali, isijekuja kushtuka shuka kukiwa kumekucha.

Wasalaam!
makanisa ni haki yake kuwepo tatizo kelele vilio miziki mchana kutwa na usiku kucha watu hatulali wala atupumziki majumbani mwetu serikali sijui inaogopa nini kwa haya makanisa kuyapiga faini ya uchafuzi wa mzingira

jambo baya kabisa ni kuruhusu makanisa ni misikitu kuwa sehemu 1 kisa heti waisilamu na wakirito wana vumiliana hakuna uvumilivu hapa kuna siku sirikali itavuna inacho kipanda

mfano ifakara watu waaridhi wameruhusu kujengwa kanisa karibu na msikiti wa muhajirina kinachotenganisha baina ya msikiti na kanisa ni mita 5

mkuu wawilaya kaambiwa akufatilia kapuuza mkuu wamkoa nae kapuuza serikali za mitaa ndio kabisa kelele mtindo 1 msikiti huo umekuwepo miaka 25 iliopita mkuu wawilaya anawaogopa wachungaji na mkuu wa mkoa morogoro nae anawaogopa wanaona bora watu wauane kuliko kukata mzizi wa fitina

wanawadharau sana waisilam kisa hawana uwezo wa kuweka wakili tunsema hivi mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya watabue kuwa hata sisi waisilamu tunahaki nchii kwa sababu kodi tunalipa kama wakirito wanavio lipa kodi hiyo ndio inayo walipa mishahara na hayo magali wanayo tembelea na malipo yao baada ya kusitafu iweje wetudharau wawe upande wa kanisa?
 
Kanisa na musikiti haviwezi kukaa pamoja, kama kuna sehemu vimekaa pamoja basi hao waliotoa vibali vya ujenzi walikosea. ila hoja kuu ni kwamba, pamoja na kwamba kila mtu ana haki ya kuabudu apendavyo, hatuwezi kuishi kama wanyama kila mtu anajiamulia apendacho, kuna sheria na miongozo, lazima ifuatwe, inakuwaje watu wanaanzisha makanisa yanadumu miaka mingi tu bila kusajiliwa, na ofisi ya usajili na ukaguzi ipo? watatuaminishaje kwamba hawakupewa rushwa na hao waliyoyafungua?
 
makanisa ni haki yake kuwepo tatizo kelele vilio miziki mchana kutwa na usiku kucha watu hatulali wala atupumziki majumbani mwetu serikali sijui inaogopa nini kwa haya makanisa kuyapiga faini ya uchafuzi wa mzingira

jambo baya kabisa ni kuruhusu makanisa ni misikitu kuwa sehemu 1 kisa heti waisilamu na wakirito wana vumiliana hakuna uvumilivu hapa kuna siku sirikali itavuna inacho kipanda

mfano ifakara watu waaridhi wameruhusu kujengwa kanisa karibu na msikiti wa muhajirina kinachotenganisha baina ya msikiti na kanisa ni mita 5

mkuu wawilaya kaambiwa akufatilia kapuuza mkuu wamkoa nae kapuuza serikali za mitaa ndio kabisa kelele mtindo 1 msikiti huo umekuwepo miaka 25 iliopita mkuu wawilaya anawaogopa wachungaji na mkuu wa mkoa morogoro nae anawaogopa wanaona bora watu wauane kuliko kukata mzizi wa fitina

wanawadharau sana waisilam kisa hawana uwezo wa kuweka wakili tunsema hivi mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya watabue kuwa hata sisi waisilamu tunahaki nchii kwa sababu kodi tunalipa kama wakirito wanavio lipa kodi hiyo ndio inayo walipa mishahara na hayo magali wanayo tembelea na malipo yao baada ya kusitafu iweje wetudharau wawe upande wa kanisa?
Pale Kongowe Mbagala Mpakani mwa Dar na Mkuranga Pana she'll pembeni Pana Kanisa na Msikiti vimedumu kwa miaka mingi sana bila mgogoro wowote! So long sio ardhi ya Msikiti kanisa linatumia au Msikiti unatumia ardhi ya kanisa hakuna tatizo wewe ndio una tatizo!

Ukifika KAMATA makutano ya barabara ya Nyerere na Ile ya chang'ombe kama unaenda mjini kabla ya daraja upande wa kulia Pana Kanisa na Msikiti na vimetenganishwa na ukuta tu miaka mingi sana sana na hukujawahi kutokea mgogoro au mtafaruku.

Msikiti wa Kichangani na kanisa la kilutheri magomeni vimetenganishwa na morogoro road na Wala hakuna shida Ibada unaendelea huku na kule bila shida.

Huku mitaani tumewekeana mipaka wakristo na waislamu Wala hakuna shida!
Maofisini na sehemu za mikusanyiko tunakaa pamoja bila shida yoyote na kubwa zaidi tunazikana kama ndugu!

Kuna Sehemu Moja Huko Rombo Kilimanjaro waislamu walitoa sehemu ya eneo lao Ili pajengwe kanisa katoliki na likajengwa!

Punguza chuki kama hakuna chochote mnaingiliana au kuhitilafiana wakati wa Ibada !
Asalam
 
Back
Top Bottom