USAHIHI wa taarifa za Lwakatare; Mkutano wa hadhara na Press Conference

asante mkuu, ila kwenye Facebook wall ya Rwakatale leo amefunguka mwenyewe kuwa atazungumza, labda kama ipo hacked na akina Mwigulu.

Hilo halina tatizo mkuu kuzungumza lazima atazungumuza ila juu ya wakati gani ndo hilo Makene amesema muda utaelelezwa ni lini
 
Hivi hii inakuwaje kama jamaa na support yote ya TISS wanapanga mission zinafeli ? Kweli CHADEMA ni mpango wa Mungu
 
Makene,

You are such a good Information Officer. Good Clarification kwa kweli nilikuwa na doubt hayo yaliyokuwa yakisemwa juu ya Kamanda Lwakatare kuitisha Press Conference na kushiriki katika kampeni. Huku nikiendelea kuamini kuwa tutaibuka na ushindi mkubwa katika jiji la Arusha bado naamini Kamanda Lwakatare ni muhimu Strategically akaenda Ama Arusha ama Mbeya ama Songea kuongeza nguvu

Regards
 
Hilo halina tatizo mkuu kuzungumza lazima atazungumuza ila juu ya wakati gani ndo hilo Makene amesema muda utaelelezwa ni lini

mkuu hii ilikuwa taarifa yake ya kwanza leo.
PEOPLEEEEEEEEEEEEEEEEEES!
Salaam MAKAMANDA, namshukuru sana Mwenyeenzi Mungu kwa kunipa fursa nyingine tena kurejea kwenye mapamabano ya pamoja na MAKAMANDA wenzangu. Tuwe pamoja leo tarehe 13/06/2013 saa 4:00 asubuhi CHADEMA Makao Makuu Kinondoni Manyanya kutakuwa na Press Coference. Pia unaweza fuatilia kwa karibu kwenye blog yangu ya wilfredlwakatare.blogspot.com yenye updates ya matukio muhimu yanayoendelea hivi sasa. TULIANZA NA MUNGU, TUKO NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU.
PEOPLEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEES!

baadae ndo akaja na hii taarifa.
Makamanda,habari ya asubuhi.
Leo budget ya taifa inasomwa,hivyo basi ni busara kuhairisha press Conference iliyokuwa ifanyike leo ili tuelekeze nguvu yetu wote katika budget yetu hii. Nitawapatia updates kupitia blog yangu na ukurasa wangu huu.
Ahsanteni sana kwa support na concern yenu makamanda.
PEOPLEEEEEEEEEEEE's!!
Nawatakia siku njema Makamanda!

pamoja sana.
 
Kumekuwepo na taarifa zinazosambazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari tangu jana juu ya vitu viwili ambavyo vyote vinamhusu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Ndugu Wilfred Mganyizi Lwakatare.1. Kwamba atafanya press conference leo, (watu wale wa upande wa pili wameenda mbali hata wametaja muda eti ni saa 4 asubuhi)2. Atakuwa kwenye mizunguko ya mikutano ya kampeni katika chaguzi ndogo za udiwani zinazoendelea katika hatua ya lala salama maeneo mbalimbali nchini.Usahihi.Kwa kuzingatia masuala kadhaa hasa mikakati ya kitaalam katika mapambano ya kisiasa, hususan katika suala hili, press conferense iliahirishwa tangu jana mapema asubuhi, baada tu ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa vimetangaza kuwa itafanyika leo, Alhamis. Tuliviarifu vyombo vya habari hivyo. Imesogezwa mbele na taarifa zitatolewa tena.Suala la mizunguko kwenye kampeni za uchaguzi mdogo...hakuna kitu kama hicho kwa sasa. Pamoja na kwamba kuna watu wenye mapenzi mema kabisa na vuguvugu la mabadiliko wamekuwa na hamu ya kutaka kumsikia kamanda mwenzao, ndugu Lwakatare akizungumza majukwaani baada ya miezi mitatu ya 'ukatili' mkubwa, pia tumebaini kuwa watu wa upande wa pili, wanataka sana kujua CHADEMA sasa inajua kiasi gani juu ya njama za kuibambikia ugaidi, utekaji na mauaji.Hivyo upande huo wa pili, ambao unaonekana dhahiri kuwa under pressure ya kutojua kiasi gani mipango yao inajulikana na itaumbuliwa kwa kiwango kipi, umekuwa ukieneza habari za Lwakatare kufanya mikutano ya hadhara kwenye kampeni za uchaguzi wa madiwani, kitu ambacho si kweli.Baada ya hila na uovu wa watawala na vibaraka wao kushindwa katika jaribio lingine kubwa kabisa wao kuwahi kupanga dhidi ya wimbi la mabadiliko na kutaka kuzuia kasi ya CHADEMA kuwaondoa madarakani, tumwache ndugu Lwakatare apumzike na familia, wakati mipango makini ikifanywa kwa ajili ya matukio yote mawili ambayo Watanzania wanategemea na kuyasubiri kwa hamu yafanyike; mkutano na press conference.Kitu kimoja cha uhakika ni kwamba, watu wa upande wa pili, ambao tayari hofu yao inajulikana, hawataweza kumchagulia Lwakatare wala kuichagulia CHADEMA kitu gani cha kusema, kama ambavyo wameanza kufanya kupitia forums mbalimbali. Let tthem cool down, wasiwasi wa nini! Yote yakayosemwa itakuwa ni kwa ajili ya maslahi ya Watanzania, haitakuwa kwa ajili ya kuifurahisha 'status quo'.Ukweli haujawahi kushindwa na uongo, wala dhuluma haijawahi kuishinda haki. Vyote viwili, ukweli na haki, vinaweza kuchelewa tu, lakini hatimaye huwadia. Kwa sababu Lila na Fila havitangamani.Makene0752 691569
Naunga mkono hoja.
 
Taarifa njema hii maana ningeshangaa kuona kamanda hapewi muda wa kupumzika na familia.
 
Kumekuwepo na taarifa zinazosambazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari tangu jana juu ya vitu viwili ambavyo vyote vinamhusu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Ndugu Wilfred Mganyizi Lwakatare.

1. Kwamba atafanya press conference leo, (watu wale wa upande wa pili wameenda mbali hata wametaja muda eti ni saa 4 asubuhi)

2. Atakuwa kwenye mizunguko ya mikutano ya kampeni katika chaguzi ndogo za udiwani zinazoendelea katika hatua ya lala salama maeneo mbalimbali nchini.

Usahihi.

Kwa kuzingatia masuala kadhaa hasa mikakati ya kitaalam katika mapambano ya kisiasa, hususan katika suala hili, press conferense iliahirishwa tangu jana mapema asubuhi, baada tu ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa vimetangaza kuwa itafanyika leo, Alhamis. Tuliviarifu vyombo vya habari hivyo. Imesogezwa mbele na taarifa zitatolewa tena.

Suala la mizunguko kwenye kampeni za uchaguzi mdogo...hakuna kitu kama hicho kwa sasa.

Pamoja na kwamba kuna watu wenye mapenzi mema kabisa na vuguvugu la mabadiliko wamekuwa na hamu ya kutaka kumsikia kamanda mwenzao, ndugu Lwakatare akizungumza majukwaani baada ya miezi mitatu ya 'ukatili' mkubwa, pia tumebaini kuwa watu wa upande wa pili, wanataka sana kujua CHADEMA sasa inajua kiasi gani juu ya njama za kuibambikia ugaidi, utekaji na mauaji.

Hivyo upande huo wa pili, ambao unaonekana dhahiri kuwa under pressure ya kutojua kiasi gani mipango yao inajulikana na itaumbuliwa kwa kiwango kipi, umekuwa ukieneza habari za Lwakatare kufanya mikutano ya hadhara kwenye kampeni za uchaguzi wa madiwani, kitu ambacho si kweli.

Baada ya hila na uovu wa watawala na vibaraka wao kushindwa katika jaribio lingine kubwa kabisa wao kuwahi kupanga dhidi ya wimbi la mabadiliko na kutaka kuzuia kasi ya CHADEMA kuwaondoa madarakani, tumwache ndugu Lwakatare apumzike na familia, wakati mipango makini ikifanywa kwa ajili ya matukio yote mawili ambayo Watanzania wanategemea na kuyasubiri kwa hamu yafanyike; mkutano na press conference.

Kitu kimoja cha uhakika ni kwamba, watu wa upande wa pili, ambao tayari hofu yao inajulikana, hawataweza kumchagulia Lwakatare wala kuichagulia CHADEMA kitu gani cha kusema, kama ambavyo wameanza kufanya kupitia forums mbalimbali. Let tthem cool down, wasiwasi wa nini! Yote yakayosemwa itakuwa ni kwa ajili ya maslahi ya Watanzania, haitakuwa kwa ajili ya kuifurahisha 'status quo'.

Ukweli haujawahi kushindwa na uongo, wala dhuluma haijawahi kuishinda haki. Vyote viwili, ukweli na haki, vinaweza kuchelewa tu, lakini hatimaye huwadia. Kwa sababu Lila na Fila havitangamani.

Makene

0752 691569
Mkuu Tumaini Makene naomba ukipata nafasi umfundishe Nape Jinsi ya kuandika habari kama Nyinyi iliyoenda shule badala ya Utumbo anao ongea na kuandika
 
Hizi taarifa ndizo tulizokuwa tunazisubiri, Ahsante kamanda.
Kuweni watulivu wekeni mikakati sisi watingaji tuko pamoja nanyi!
 
Mtuhumiwa mkuu wa kupanga njama kuteka na kutesa wahandishi leo anakuwa mtu muhimu katika jamii ya watanzania wapenda amani,haki na ustaarabu? ama kweli Tanzania ni zaidi uijuavyo.
 
Hivi hii inakuwaje kama jamaa na support yote ya TISS wanapanga mission zinafeli ? Kweli CHADEMA ni mpango wa Mungu

Mkuu!

Mwanafalsafa wa kale aliyeitwa Niccol Machiaavelli aliyewahi kuandika kitabu maarufu duniani ambacho kinapenda kutumiwa na watawala madikteta kinacho itwa "The Prince" aliwahi kusema.

"Kuna njia nyingi za kupima uwezo wa kufikiri wa watawala. Njia ya kwanza kubwa na bora zaidi kupima ubora wa akili ya mtawala yeyote ni kuangalia aina na hulka ya washauri wanao mzunguka"

Kwa kauli hiyo hapo juu, kusanya na unganisha nukta kwenye masuala matatu ya mfano.

1. Lugha zinazo tumika kwenye matamko ya kurugenzi ya mawasiliano ambapo baba wa Taifa aliwahi kusema "Ikulu ni mahali patakatifu"

2. Sakata la Lwekatare lililo itwa la kigaidi na miongoni mwa washauri wa raisi ambaye ni naibu katibu mkuu wa ccm na namna UWT ilivyo husishwa.

3. Sakata la Mtwara, madai ya wana Mtwara yanapotoshwa na bado washauri wa mkuu hawamuelezi ukweli.

Kwa mifano hiyo mitatu hapo juu dadavua fikra zako na kakavua ubongo wako uone kama kama mizani inapima.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
  • Thanks
Reactions: Pai
MwandishiP. HAMY-D, umejizalilisha sana kwa kuja kutupotosha hapa jamvini, kwa kuanzisha thread ya uongo. shame on you.

Safi sana kamanda Tumaini Makene upande wa pili wanahangaika sana.

CC Pasco

Nichukue fursa hii kusafisha hansard, kwani nimegundua una juhudi kubwa za kutaka kunichafua.

Taarifa yangu haikuwa ya uongo, ila kilicho tokea ni 'ukigeu geu' wa CHADEMA, wao wenyewe ndio hawana msimamo.

Nilivyo itoa ile taarifa hapa niliipata sehemu rasmi na kwa mtu rasmi (Lwakatare mwenyewe), sasa kubadili muda wa hiyo press conference, sio suala langu mimi, kwani wao ndio walipanga press conference ifanyike leo tar 13/06/2013 saa 4:00 asubuhi, makao makuu CHADEMA.

Tumaini Makene, PERFECT, Buchanan.
 
Last edited by a moderator:
Hiz ndzo habar za kuleta hapa jamvin,habar inanyama imejitosheleza sn.Mwachen apumzike na family yake akili ikae sawa,kutengwa na family yako co kitu kidogo
 
mkuu hii ilikuwa taarifa yake ya kwanza leo.


baadae ndo akaja na hii taarifa.


pamoja sana.

Kiongozi wetu apinga, anadai hizi ni habari za kupikwa na 'upande wa pili' Kuropoka turopoe sie, kuongea tuongee sie, tusingizie upande wa pili. Majangaaaaa
 
Kiongozi wetu apinga, anadai hizi ni habari za kupikwa na 'upande wa pili' Kuropoka turopoe sie, kuongea tuongee sie, tusingizie upande wa pili. Majangaaaaa
unless waseme hiyo account imekuwa hacked, vinginevyo hii taarifa ya Makene ina walakini.
 
Back
Top Bottom