USAHIHI: Kuhusu uvumi wa John Mnyika

USAHIHI: Kuhusu uvumi wa John Mnyika

Nataman kutoa tusiii jipyaaaaa.......................
 
mnyika aje hapa akanushe...vinginevyo tutaanza kuamini kuna ukweli...
Kwa nini Bavicha wamsemee? Msemaji wa Chama Tuma Makene amtafute JJM kusawazisha ombwe hili.
Ukimya wa mnyika kwa siku hizi za karibuni zinaleta mashaka.
 
Issue ya Dr. Slaa ilianzaga hivihivi kwa mikanusho mikali.
 
Watu wenye nia ovu dhidi ya Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John John Mnyika, wamesambaza taarifa ya uongo mitandaoni kwa lengo la kupotosha umma wa Watanzania....

Wasambazaji wa uongo huo ambao ni wazi pia wana nia ovu dhidi ya CHADEMA na wananchi wazalendo wanaounga mkono mapambano ya kutafuta MABADILIKO na UHURU wa kweli nchini, wamesambaza taarifa hiyo wakilenga pamoja na mambo mengine;

1. Kumgobanisha JJ Mnyika na Watanzania wengi ndani na nje ya nchi wenye ambao wana imani nae kubwa kama kiongozi wao.

2. Kumgobanisha Ndugu Mnyika na wananchi wake wa Jimbo la Kibamba ambao walimpigia kura kutokana na imani kubwa waliyonayo juu yake kwa namna anavyowawakilisha bungeni lakini pia wanaoamini katika misingi imara ya CHADEMA katika kupigania mabadiliko na uhuru wa kweli kwa maslahi ya wananchi.

3. Kusababisha taharuki miongoni wa jamii kubwa ya Watanzania yenye mapenzi na matumaini makubwa juu ya CHADEMA na viongozi wake katika kuamua mstakabali wa nchi hii.

4. Wanalenga kuhadaa Watanzania Watanzania kwa kubadili mijadala ili umma uanze kujadili vitu vya kutengenezwa badala ya mijadala mikubwa inayoendelea nchini kwa sasa, kama vile; bajeti inayomuongezea maisha magumu kila Mtanzania, udkiteta uchwara unaovunja katiba na sheria za nchi, kauli tata za viongozi zinazoonesha kuwa Serikali ya CCM iko katika anguko la kisiasa kutokana na kuishiwa busara ya uongozi, hoja, mbinu na mikakati ya kuiongoza nchi.

Katika hatua ya sasa wakati tukitoa wito kwa Watanzania kupuuza taarifa hiyo ambayo pia ina lengo la kutaka kuwaondoa kwenye mjadala muhimu wa kuiondoa CCM madarakani, tunataka Mamlaka za Serikali zinazohusika zichukue hatua za haraka kisheria, hususan kwa mujibu wa Sheri ya Makosa ya Mtandaoni, dhidi ya wote waliohusika kusambaza taarifa hiyo ambayo leo imeibua taharuki kubwa bila sababu za msingi.

Wakati tayari Mnyika amekanusha taarifa hiyo, tunatoa wito kuwa mamlaka hizo zioneshe kuwa zina uwezo wa kuchukua hatua kwa kutumia sheria hiyo kwa wakosaji hasa kama ilivyofanyika leo, kuliko kuonesha umahiri wa kuitumia sheria hiyo kisiasa kuwabambikia kesi wale wanaotumia uhuru wa kikatiba wa kutoa maoni yao kuipinga serikali ya CCM na viongozi wake, hasa pale wanapovunja Katiba na Sheria za Nchi.

Imetolewa leo Jumapili, Julai 3, 2016 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 
Mkuu hizo zote Ni Propaganda, mpaka Leo hii Serikali ingekuwa Na uwezo ingejenga nyumba nyingi tu Na kuwapa wananchi wake bure tu Na sio kwa bei rahisi!
Hizo propaganda wenye akili wanajua hazina tija yoyote, credibility ya Magufuli kuhusiana Na UFISADI huwezi kui-question!! But it is very simple to question Lowasa's credibility when it comes to corruption scandals!!

hahaha! wabongo wanafiki sana. hata la mv dar es salaam!!!! ambalo liko wazi kabisa.
 
TAARIFA KWA UMMA

Ipo hoja nyepesi mno iliyopikwa na Vijana wa Lumumba juu ya Mbunge wa Kibamba na Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika kuwa alimkataa Lowassa

Hoja hiyo ni ya kupuuzwa kwa kuwa haina ukweli wowote ule, na nitalishangaa Jeshi la Polisi kuendelea kukaa kimya,na kumuacha aliepotosha Umma kwa kiwango kikubwa kiasi hicho,jambo ambalo limempa Usumbufu mkubwa Naibu Katibu mkuu kwa chama na Wananchi wake katika jimbo lake.

Nataka kuona nguvu ya Cyber Crime kama kweli sheria hiyo ni dhahiri ni msumeno au huwa inakata upande mmoja tu!.Mnyika ni Kiongozi mkubwa na katika Taasisi kubwa sana nchini CHADEMA,hapaswi kunenewa uongo kwa nia ya kuupotosha Umma naliomba jeshi la Polisi liingie kazini Mara moja kutimiza majukumu yake.

Imetolewa July 03

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa
Mufilisi mufilisi! ProfF Mkumbo rudi uwaokoe hawa jamaa....wanatia huruma wanakosa cha kuandika...hawana mission wala vision.... Agenda kuu ni Sukari, Vilaza wa vyuoni, Mahafali, Kuziba midomo, na Mitusi minene minene! Usichezee Kubadilishia GIA angani!
 
Kuna vitu vya ajabu sana, kama vijana wa Lumumba wanalipwa kwa mambo kama haya basi naona anguko la chama tawala miaka mitano au kumi ijayo, hapa dola labda ndio itasaidia! Huwezi kuwa na vijana type ya Lizaboni, Msemaji ukweli, Ruttashobolwa, 1954,YODAYA and co utegemee kuwa chama kinaweza kuwa na uhai wa kudumu, wanashindwa kushauri serekali ihangaike kuwaletea wananchi maendeleo wao wanakazana na kufanya propaganda za ovyo ambazo hata mtoto wa chekechea hawezi fanya. Unasambaza ujumbe ambao unajua mhusika yupo na anauwezo wa kukana na ikaeleweka sasa hapa sio kuwa na akili fupi? Hapa si sawa na kujaza maji kwenye gunia? Chama tawala kinakumbwa na matatizo ya Kuwa na vijana wenye mawazo mgando, vyeo vyao vinaangalia zaidi undugu na ushkaji bila Kuangalia akili ya mtu matokeo yake ndio haya vijana hawajui hata wanafanya nini kwa ajili ya chama, ukienda kwenye bunge ambako vijana walitakiwa wawe ndio wanaoikosoa na kuisema serekali ili ifanye ilioyaahidi huko tena ndio kumekuwa kama sokoni wabunge vijana wamepatikana kwa njia ya rambirambi uwezo wao umebaki kuongelea madera, sanamu la diamond, mara kanivua barakashia, mara ujengwe mnara sehemu fulani alipopigia push up, mara natamani kulia, mara wabunge fulani wana sura mbaya, hapo hamna wa kuishauri serekali na wala chama sasa wanakuja kufikiri umaarufu wa chama na Serekali kwa wananchi umepungua sababu ya UKAWA. Ingekuwa wana akili kidogo tu wangejuaje mchawi ni wao wenyewe kwa kutokuwa na uwezo uwezo mzuri wa kushauri chama na Serekali. Mtu kama Lizaboni na co keshokutwa ni mbunge Unategemea nini mbeleni kama sio chama kujifia kifo cha ajabu.
 
Leo hii Mnyika kawa mtu wa kusemewa?

Kutoka kwenye usemaji hadi usemewaji?

Nakumbuka alivyokuwa ameishupalia issue ya ZZK kila leo press conference.
 
...hao watu watafutwe,kwani kumsemea mtu vibaya lazima umtusi?!,
 
Du ! Yaani tamko la katibu mwenezi lipo kirahisi rahisi namna hii, hivi mbona hawa hawa BAVICHA waliweza kufanya kazi nzuri sana huko nyuma, ni nini tatizo la BAVICHA ya sasa hadi wamekuwa hasara hivi.
 
Back
Top Bottom