USAHIHI: Kuhusu uvumi wa John Mnyika

Acha Jeshi la polisi lishughulike na mambo ya maana huu upuuzi mbaki nao wenyewe na taratibu zipo wazi aende mwenyewe post. Msipende kulinganisha mbingu na ardhi.
 
Nadhani ingekuwa Ni wakati wa Mnyika kujitokeza na kukanusha, na yeye ukimya wake wa muda mrefu umezaa yote hayo.

Kuhusu cyber crime sikubaliani na Ile sheria na mambo yakee yote.....
Katika dunia ya kidemokrasia hayo Ni mambo ya kawaida Sana, hasa Kati ushindani huru wa vyama vingi.....jibu Ni kukanusha tu
 
Hata vyama vyote vya siasa vifutwe au wote viongoz wa upinzan warud ccm kamwe siwez kuunga mkono serikali chin ya ccm wala kukipenda chama kinachoitwa ccm. Miaka 50 wametufikisha hapa sion jipya kwao
 
TAARIFA KWA UMMA

Ipo hoja nyepesi mno iliyopikwa na Vijana wa Lumumba juu ya Mbunge wa Kibamba na Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika kuwa alimkataa Lowassa

Hoja hiyo ni ya kupuuzwa kwa kuwa haina ukweli wowote ule, na nitalishangaa Jeshi la Polisi kuendelea kukaa kimya,na kumuacha aliepotosha Umma kwa kiwango kikubwa kiasi hicho,jambo ambalo limempa Usumbufu mkubwa Naibu Katibu mkuu kwa chama na Wananchi wake katika jimbo lake.

Nataka kuona nguvu ya Cyber Crime kama kweli sheria hiyo ni dhahiri ni msumeno au huwa inakata upande mmoja tu!.Mnyika ni Kiongozi mkubwa na katika Taasisi kubwa sana nchini CHADEMA,hapaswi kunenewa uongo kwa nia ya kuupotosha Umma naliomba jeshi la Polisi liingie kazini Mara moja kutimiza majukumu yake.

Imetolewa July 03

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa
Edward Simbeye, atembelee
bandiko hili na aseme kama anawajua ni kina nani waliozungumzwa humo!.

Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa,.
Pasco
 
Hay a wanaCDM hebu tujalieni ukweli wa hiyo statement kama iko sawaa ama laaa..inaenezwa kwenye magroup ya wassap. Angalizo mpaka iwe imehakikiwa na wahusika ndo tuanze yale maneno yetu yasiyo na busara kama nijuavyo JF. Kwa yenye busara yaanze sasa hivi....
Uzushi usipate tatizo. Buku 7 za Lumumba zinafanya kazi. Mnyika kashakanusha
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mtakumbuka ni muda sasa sijaonekana wala kusikika katika harakati za kisiasa. Leo nimependa kuweka bayana ili umma wa watanzania ufahamu kwani kumekuwa na upotoshwaji mkubwa juu ya ukimya wangu.

Napenda umma wa watanzania ufahamu yafuatayo:-

1. Msimamo wangu wa kuitaka serikali imkamate Mh Edward Lowassa, imhoji na imchukulie hatua kwa mujibu wa sheria kutokana na ushiriki wake katika kashfa ya RICHMOND haujabadilika kama ambavyo niliwahi kusema nikiwa mkurugenzi wa vijana wa CHADEMA tar 25 Februari 2008 na kipindi chote nikiwa Mbunge wa Ubungo.

Hivyo nategemea kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi Lowassa ndiyo atakuwa wa kwa. Siwezi kusaliti msimamo wangu bora nipoteze ubunge wangu.

2. Sikukubaliana na utaratibu uliotumika kumpata mgombea urais ndani ya Chama changu hususani ujio wa Mh Edward Lowassa mmoja wa watu ambao ni mizizi ya ufisadi hapa nchini. Hali hii ilinilazimu nikae kimya kutokana na kutokuamini kilichokuwa kinatokea hususani kwa Chama kama CHADEMA kilichojijenga na kujipatia umaarufu kwa kuongoza mapambamo dhidi ya rushwa, ubadhirifu, ufisadi na uwajibikaji mbovu wa serikali halafu tukasaliti msimamo wetu kwa uharaka wa kuipata dola! Sikukubaliana na sijakubaliana hata sasa.

3. Napenda kuzungumzia utendaji wa serikali ya Dkt Magufuli. Naomba Ifahamike nimekuwa mara zote nikisema matatizo ya msingi ya nchi yetu hayasababishwi na mapungufu ya sheria ila Kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na kulegea kwa misingi ya utawala wa sheria na uwajibikaji miongoni mwa viongozi. Hivyo kwa asilimia kubwa naona Dkt Magufuli ameweza kujibu nilichokuwa nikikilalamikia kwa muda sasa. Haya mengine yanazungumzika.

4. Sikubaliani pia na mtazamo wa baadhi ya viongozi wakiwemo wa Chama changu wanaotaka fedha za walipa kodi ziendelee kuteketea kwa ufisadi na ubadhirifu huku wahusika ambao ni wachache wakilindwa kwa kisingizio cha haki za binadamu. Kwa hili nampongeza Mh Rais kwa msimamo na hatua anazochukua japo apanue wigo ili watanzania maskini wanufaike na utajiri wa rasilimali walizojaliwa.

5. Vile vile naomba kuzungumzia mwenendo wetu kambi rasmi ya upinzani bungeni au UKAWA binafsi sifurahishwi na maagizo na maelekezo ya viongozi wetu juu ya kuingia na kutoka bungeni kwa hoja ambazo haziwagusi wananchi moja kwa moja kiasi cha kutufanya tushindwe kutimiza majukumu yetu kama wabunge kwa mujibu wa Ibara ya 63 (2) na (3) katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutunga sheria, kuisimamia serikali, kuwawakilisha wananchi na kupitisha mipango ya maendeleo. Sifurahishwi sababu kutoka Kwetu hakuna la msingi tunalofanya kwa ajili ya wananchi waliotutuma huko bungeni. Tusipobadilika itatugharimu!

Mwisho nawatakia waumini wote wa kiislamu mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Imetolewa leo tar 3 Julai 2016.

John Mnyika (Mb)
0754 694 553


Huyo ndiyo Super Mnyika!
 
Hapo sawa naona kitengo cha propaganda kwa upande wa CDM wanataka kuharibu mambo...source haikuwa nzuri wajua makundi ya wassap na yenyewe. Nadhani atafika hapa Mnyika akanushe au kina Makene nk...
Taarifa ilishafika ya kukanusha.. Mufisiemu isikuumize kuchwa
 
Ukweli Ni kwamba Hakuna mpinga UFISADI ambaye anaweza kumpinga Magufuli Na kumuunga mkono Lowasa, Ila Anayetaka mafisadi Atakuwa upande wa kumuunga mkono Lowasa Na kumpinga Mafuli, hiyo Ni fact!!
Aliyeuza na kudalalia kuuza nyumba za serikali na zingine kuwagawia mahawara zake, aliyenunua kivuko kibovu kwa cha mwaka 1978 kwa bei ya kivuko kikubwa cha kisasa cha mwaka 2015 na kisha kuzuia wabunge wa upinzani wasiijadili bungeni ni nani we mkilaza?
 
Mkuu Pasco, unarudisha mkanda nyuma na je ilikuwa kweli au zilikuwa habari za kusadikika
 
Mnyika ameamua kuwatolea uvivu ufipa .

Safi sana Mnyika, naona wanahaha kukuziba mdomo.


Chadema chama la madikteta lisiloruhusu MTU kutoa mawazo yake
 
TAARIFA KWA UMMA

Ipo hoja nyepesi mno iliyopikwa na Vijana wa Lumumba juu ya Mbunge wa Kibamba na Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika kuwa alimkataa Lowassa

Hoja hiyo ni ya kumanaged twa kwa kuwa haina ukweli wowote ule, na nitalishangaa Jeshi la Polisi kuendelea kukaa kimya,na kumuacha aliepotosha Umma kwa kiwango kikubwa kiasi hicho,jambo ambalo limempa Usumbufu mkubwa Naibu Katibu mkuu kwa chama na Wananchi wake katika jimbo lake.

Nataka kuona nguvu ya Cyber Crime kama kweli sheria hiyo ni dhahiri ni msumeno au huwa inakata upande mmoja tu!.Mnyika ni Kiongozi mkubwa na katika Taasisi kubwa sana nchini CHADEMA,hapaswi kunenewa uongo kwa nia ya kuupotosha Umma naliomba jeshi la Polisi liingie kazini Mara moja kutimiza majukumu yake.

Imetolewa July 03

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa
Kijana unatakiwa ujue kwamba post yako hii haisomwi na vijana wa aina yako pekee, watu wengi wenye uwezo wa kufikiri vizuri watausoma pia. Jiulize, Kwani watu ambao hawakumtaka lowasa pale cdm ni mnyika peke yake? Siyo lazima waseme hadharani lakini nyuso na matendo yao yalitosha kuionesha jamii walivyokuwa wakimpinga Lowasa. Kama ambavyo waliokuwa hawamtaki magufuli wengi wao waliendelea kubaki ccm na hawako tayari kusema lolote hadharani, vivyo hivyo na kwa upande wa pili inaapply.
 
Back
Top Bottom