Hii vita US anahangaika tu, Trump atakachofanya hapo ni kurusha missiles mbili tatu jangwani , halafu wanakaa mezani huku kama kawaida yake akirusha vijembe mitandaoni kwamba ameipiga Iran hadi imeamua kuitikia wito na kukaa mezani.
Vita ya june kati ya Iran na Israel, US alishindwa kumpa ulinzi mshirika wake Israel, THAAD na interceptors za SM-3 kutoka kwenye destroyers zilizokuwa zinaelea mashariki mwa bahari ya Mediterranean kwa lengo maalumu la kuzuia missiles za Iran ilishindikana.
Israel akaweka Arrow 3 na iron dome, Jordan , France na Britain zikaingia kati kuisaidia Israel kupukutisha missiles za Iran zisiingie Israel ikashindikana pia, Israel ikaanza kutafunwa taratibu, ikaanza kumomonyoka taratibu, SM-3 kutoka kwenye destroyers zilizokuwa zinaelea Mediterranean zikaanza kuisha kwenye stock... hii SM-3 ni interceptors expensive.
ADs nyingi za Israel zikaanza kupungukiwa interceptors, na ikaonekana kwa muda mfupi ujao Israel haitoweza tena kulinda anga lake, ni vita ya siku 12 tu lakini ilikuwa inakwenda kuimaliza Israel. ikabidi waite ceasefire, Iran ikawa ya mwisho kuipiga Israel na vita ikasimama, Israel haikujibu.
Ndio maana Israel hivi sasa haonekani tena kuwa mbele kwenye hii vita, mashambulizi yakianza hawana uwezo kujizuia.
Licha ya kuwepo kwa complex layered air defense ili kuilinda Israel lishindikana...
Israel anakaa nyuma maana kipigo kikianza wenzake wapo maelfu ya maili... japo ni vyema wanavyochukua precautions maana vita haitabiriki.
US hana uwezo kuingia full scale war na Iran tokana na mambo kadhaa ikiwemo sababu za kijiografia, kistratejia na kiuchumi.
Ngoja tusubiri lakini hii ni mikwara na sijui lengo la US ni lipi, kuna kitu kipo nyuma ambaho wengi hatukioni, kuna masuala ya kijasusi yanaendelea nyuma ya pazia.