US is sending more defence armies in gulf

Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,327
1,681
Wanajf, kile kinachodhaniwa huenda kikatimia kuwa kweli.
Marekani imetangaza kutuma wanajeshi wengine zaidi ya 1000 huko mashariki ya kati ili kujilinda dhidi ya vitisho vya Iran huko miezi kadha iliyopita US ilituma wanajeshi wengi kwa ajiri ya kujilinda.
Je kuna uwezekano wa kutokea vita?
je tunajiandaaje sisi watanzania kuhusu uchumi wetu?
Je US ataiweza Iran kijeshi?
 
Hamna vita hapo.....vitisho na siasa....
Kuanza kwa vita huwa hakuna kujiandaa au kujiuliza uliza maswali, kutafuta kuungwa mkono kwa kiwango hiki Ukiona hivyo ujue hamna sababu hasa ya vita au sababu ya vita inatafutwa..
Ikitokea incidence ya vita huwa hakuna show games kama hizi...watu wanatangaza huko waliko wanaingia mzigoni
 
Kwa takwimu zilizopo, US na Irani wakiingia vitani wao kama wao, Irani atapigwa.

Tatizo la vita za nchi zenye maslahi ya kidunia huwa hawapigani wenyewe wakatoshelezana, huwa lazima wapatikane viherehere kuonesha kuunga mkono upande moja wapo.

Hapo ndiyo vita hubadilika na kuvaa sura nyingine!

Tunaomba sana balaa kama hilo M/Mungu aliepushe ili maisha ya amani yaendelee.

Kwenye vita kama hizo tunaobeba adha na madhara makubwa ni sisi nchi maskini, ila kwa wenzetu walioendelea wao ni fursa.
 
Wanajf, kile kinachodhaniwa huenda kikatimia kuwa kweli.
Marekani imetangaza kutuma wanajeshi wengine zaidi ya 1000 huko mashariki ya kati ili kujilinda dhidi ya vitisho vya Iran huko miezi kadha iliyopita US ilituma wanajeshi wengi kwa ajiri ya kujilinda.
Je kuna uwezekano wa kutokea vita?
je tunajiandaaje sisi watanzania kuhusu uchumi wetu?
Je US ataiweza Iran kijeshi?
US hawezi kumpiga Irani, atatolewa knock out
 
Kitathimini kama ni special force 1000 hizo ni regment mbili tuu!!
America ni hatarii tuombe Mungu Trump asiwe kichaa kama Bush.
Air Force ya USA ni shida, soma history ya kampein mbali mbali za vita ya USA.
Iran yuko kwenye range ya zana zilizopo Ghuba ni hatari saana!!
 
Sasa wanajeshi 1000 ni kitu?Ulizieni iran ipo kwenye orodha ya nchi kumi ambazo ni ngumu kuzivamia nchi ipo na milima ile


Tukija iran most of people wanasupport serikali yao kwa 100% Wananchi wa Iran ni wazalendo kweli kweli...

Kuipiga iran hata zikiungana nchi 60 bado utakua ni mziki mnene iran yupo na jeshi la akiba kubwa hapo hujaweka mamilioni ya wairan hujaweka Hezbollah ya lebabon,hujaweka hamas,syria army,wahouth,shiite military wa Iraq, Haya wale kule syria wanamgambo wa iran wapo zaidi ya laki mnafikiri hii vita ni simple??Hiyo vita itawasha moto middle east nzima hapo hujaweka wale raia wa saudi arabia wanaotaka kujitenga watapoanza kupambana na saudi kingdom,bahran akishiriki iran atawapa silaha wananchi ambao wengi wao wanaipinga serikali kwa muda mrefu kiujumla hiyo vita inaweza kuvuka mpaka ulaya....
 
... kuna ujinga fulani anafanya Iran wa kushambulia meli hususan za mafuta! Anachokitafuta anaenda kukipata muda sio mrefu. Trump hamalizi muda wake bila kuchapa mtu na mtu huyo ni Ayatollah. Muda uliosubiriwa ni kama umewadia.
 
Back
Top Bottom