US Gendermerie 1 - 1 Simba Sc| CAF Confederation Cup | Stade General Seyni Kountche

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,714
45,099
Muda mchache ujao, wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Caf Confederation Cup, Simba SC atashuka dimbani ugenini nchini Niger, kumenyana na wenyeji wao, US Gendermerie katika dimba la General Seyni Kountche ambaye alikuwa kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo na kiongozi wa mapinduzi ya 1974.

Huu ni mchezo wa pili kwa Simba, baada ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Asec katoka uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam

Mtanange huu utawajia saa 1:00 usiku kwa saa za afrika mashariki, kupitia AzamTv, Dstv, Star times.

=======

Dakika 17 zimetosha kwa mshambuliaji wa Simba Bernad Morrison kusawazisha bao lililodumu kwa dakika 71.

Ni furaha kwa Wanamsimbazi baada ya kupata pointi moja ugenini katika mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika ugenini dhidi ya USGN ya Niger.


Union Sportive de la Gendarmerie Nationale ni klabu ya soka ya Niger yenye makao yake mjini Niamey. Iliasisiwa mwaka 1996.

Union Sportive de la Gendarmerie Nationale is a Nigerien football club based in Niamey.

Kwa upande wa Simba SC Yusuf Valentine Mhilu na Erasto Nyoni pia wamo katika kikosi cha wana Msimbazi

GOAL 11' Wilfred wa US Gendarmerie Nationale

Dakika 26' US Gendarmerie Nationale 1 - 0 SIMBA SC timu zinapata dakika za kunywa maji.

Dakika 29' Z. Adebayo wa US Gendarmerie Nationale ana wakosa SSC

Dakika 37' mchezaji anayesumbua sana Z.Abebadeyo anafanyiwa foul na walinzi wa Simba SC

Dakika 45' : HALF-TIME
US Gendarmerie Nationale 1- 0 SSC

Dakika ya 52' Abebayo analazimisha kona, air Manula anakamata mpira

Dakika 60' Sheik Abdul Nassir nahodha wa Union Sportive de la Gendarmerie Nationale akosa bao la wazi kabisa, kweli Mungu Mkubwa yupo na Simba SC

Dakika 65' John Bocco kuchukua nafasi ya Peter Banda

Dakika 68' Kapombe anachonga adhabu karibu na kibendera cha kona upande wa US Gendarmerie

Dakika 71' kuna matumaini baada ya ujio wa John Bocco Papaa', Simba SC kama timu inaingia sana katika eneo la miguu 18 ya lango la US Gendarmerie Nationale ya Niger

Dakika 75' Sergie Wawa ana mzuia mchezaji wa US Gendarmerie na wanapata free kick, adhabu mpira unakwenda juu na kuwa goal kick .

DAKIKA 80 ' US GENDARMERIE 0 - SIMBA SC

Dakika ya 82' Jimson Mwanuke anaemia

GOAL : Dakika 83' Bernard Morisson anasawazisha kufuatia mpira wa kona ktk lango la US Gendarmerie



Dakika ya 83 : US Gendarmerie 1 - 1 Simba SC

Dakika 90' + 4

Dakika nne za nyogeza mpira unaendelea
Dakika 93' nafasi kwa Johnny John Bocco papaa anapaisha mpira
DAKIKA 94' MPIRA UMEKWISHA
FULL-TIME :
US Gendarmerie 1 - 1 Simba SC

Msimamo wa kundi

667147C9-82E5-49FF-A2D5-66B3BBFB1D1C.jpeg
 
Back
Top Bottom