US election 2020: Nani kuwa mgombea mwenza wa Joe Biden kati ya hawa?

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,416
7,828
Habari!

Mnamo mwezi Machi, Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden aliahidi kumteua mwanamke kuwa mgombea mwenza iwapo atateuliwa na Chama cha Democratic kuwania kiti cha Urais kwenye uchaguzi ujao wa mwezi Novemba hapo baadaye mwaka huu.

Kwa yule asiyefahamu, Joe Biden hivi sasa ndiye mgombea rasmi wa kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Democratic katika uchaguzi ujao utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu nchini Marekani.

Kitendawili kilichopo hivi sasa ni kuhusiana na huyo mgombea mwenza ambapo kwa mujibu wa Bw. Biden, mgombea mwenza huyo kama nilivyosema hapo awali ni mwanamke.

Joe Biden anatarajiwa kumtangaza mgombea mwenza katika kipindi kifupi kijacho lakini kwa sasa orodha ni ndefu ila wapo ambao wanatajwa na wachambuzi mbalimbali kama kati ya wanawake ambao huenda mmoja wapo kati ya hao akapewa nafasi hiyo.

Hawa hapa:

1. KAMALA HARRIS
Kamala-Harris (1).jpg


Katika wanawake wanaopigiwa upatu zaidi (wengine mnasema "chapuo") kuteuliwa katika nafasi hiyo basi si mwingine bali ni Seneta wa jimbo la California, Kamala Devi Harris. Vyanzo mbalimbali vinamtaja mwanamke huyu kama "front-runner" kuelekea katika uteuzi huo wa mgombea mwenza wa Chama cha Democratic.

Bi Kamala Harris mwenye umri wa miaka 55 ni Mmarekani mweusi (African-American) mwenye asili ya Kijamaika upande wa baba yake na Kihindi upande wa mama yake anayetajwa kama mwanamke wa pili Mmarekani mweusi kushika wadhifa wa Useneta katika historia ya taifa la Marekani. Mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuwa Seneta nitakutajia hapo baadaye!

Kamala Harris anaonekana kupewa nafasi kubwa zaidi kutokana pia na maombi ama shinikizo linalomkabili Joe Biden kwa miezi kadhaa sasa likimtaka kuteua mgombea mwenza Mmarekani mweusi ama Mmarekani mwenye asili ya Afrika, shinikizo ambalo limechagizwa pia na masuala ya haki za Wamarekani weusi kutokana pia na sakata la hivi karibuni kuhusiana na kifo cha George Floyd lililoamsha maandamano ya Black Lives Matter.

Je, Kamala Harris anafaa kuwa mgombea mwenza wa Joe Biden?

2. ELIZABETH WARREN
2682.jpg


Seneta huyu wa Massachusetts mwenye umri wa miaka 71 anatajwa pia kama mwanamke mwenye nafasi kubwa ya kuikamata nafasi hiyo muhimu. Elizabeth Ann Warren ni Mmarekani mweupe na anatajwa kama ndiye mwanamke Mmarekani mweupe pekee mwenye nafasi kubwa zaidi ya kuwashinda wenzake katika kinyanganyiro hicho.

Elizabeth Warren ni msomi wa sheria na mwalimu, profesa wa zamani wa sheria anayejulikana kwa sera zake za maswala ya kiuchumi na kijamii. Kabla ya kuitumikia Seneti alikuwa mshauri wa Ofisi ya Ulinzi wa Fedha za Watumiaji wa Bidhaa na Huduma (CFPB) mnamo mwaka 2010 hadi 2011. Warren alichaguliwa kuwa Seneta mnamo Januari 3 mwaka 2013 kama Seneta wa kwanza wa kike kutokea Massachusetts.

Bi Warren anazungumziwa kama mwanamke mwenye uzoefu wa kiuongozi nchini Marekani hususani katika migogoro ya kiuchumi kutokana pia na mchango wake katika kuanzishwa kwa shirika la CFPB lenye kuzisimamia taasisi za kifedha na zisizo za kifedha, kusimamia ripoti za masoko, na pia kukusanya na kufuatilia malalamiko ya wanunuzi wa bidhaa na huduma katika soko la kibiashara.

Vipi kuhusu Elizabeth Warren; Je, anafaa kuwa mgombea mwenza wa Joe Biden?

3. MICHELLE OBAMA
michelle-obamas-birthday.jpg


Michelle LaVaughn Robinson Obama ni mwanasheria na mwandishi wa vitabu ambaye ni mke wa rais wa 44 wa Marekani Ndugu Barack Obama. Huyu ni mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuwa First Lady nchini Marekani mnamo mwaka 2009 hadi 2017. Michelle Obama anatajwa pia kama mwanamke mwenye nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Bw. Joe Biden kuelekea katika uchaguzi ujao. Usishangae!

Ukiachana na nafasi yake kama First Lady wa zamani, Michelle Obama mwenye umri wa miaka 56 amejizolea umaarufu mkubwa na kuwa mfano wa kuigwa hasa kwa wanawake na amekwisha fanya kazi kama mtetezi na mhamasishaji wa masuala mbalimbali ya kijamii yakiwemo elimu, lishe bora, mazoezi ya mwili pamoja na mitindo ya mavazi.

Hayo ni machache tu kumuhusu Michelle Obama lakini ikoje ama iko vipi nafasi yake katika kinyang'anyiro hiki cha mgombea mwenza wa Urais kutoka Chama cha Democratic?

4. STACEY ABRAMS
8709806de9aea4f08c252170d1241c2a1d-02-abrams.rsquare.w1200.jpg


Stacey Yvonne Abrams kwa majina yake kamili ni mwanasiasa, mwanasheria, mwanaharakati wa haki za upigaji kura, na mwandishi wa vitabu aliyewahi kutumikia Baraza la Wawakilishi la jimbo la Georgia kwa miaka takribani 10 kuanzia mwaka 2007 hadi 2017.

Stacey Abrams mwenye umri wa miaka 46 ni Mmarekani mweusi mwingine aliyejizolea umaarufu kutokana na harakati zake kuhusu haki za upigaji kura. Tofauti na wapinzani wake katika kinyang'anyiro hiki, Stacey Abrams amekuwa akifanya kampeni ya kuwa makamu wa rais wa Biden na anatajwa kama nyota mpya inayoibuka ndani ya Chama cha Democratic. Je, nyota hii itaweza kung'aa katika kinyanganyiro hiki cha kumpata mgombea mwenza wa chama chake?

Hao niliowataja ni wachache tu lakini wako wengine kadhaa wakiwemo pia:
  • Meya wa jiji la Atalanta, Georgia Keisha Lance Bottoms
  • Gavana wa Michigan Gretchen Whitmer
  • Seneta wa Illinois Tammy Duckworth
  • Gavana wa New Mexico Michelle Lujan Grisham
  • Seneta wa Arizona Kyrsten Sinema

Bila kuwasahau wanawake wengine akiwemo mwana Congress kutoka California Karen Bass, mwana Congress kutoka Florida Val Demings, Seneta wa Wisconsin Tammy Baldwin pamoja na Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa zamani Susan Rice.

Mchakato huu wa kumpata mgombea mwenza wa Joe Biden unaendelea kufanywa chini ya usiri mkubwa au unaweza pia kusema usiri uliokithiri, hata washauri wengi wa juu wa kampeni za Biden wako gizani kama tu wengi wetu humu jukwaani katika kujua kile kinachoendelea kuhusiana na mgombea mwenza mahususi anayekusudiwa.

Tuendelee ama tuzidi kuvuta subira wakati mchakato ukiendelea na muda si mrefu tutaweza kulipokea jawabu la kitendawili hiki kigumu kilichopo hivi sasa.

Tukutane hapo baadaye, asante kwa sasa!


SASISHO: Agosti 11; Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Democratic Bw. Joe Biden amemchagua Seneta wa California Bi Kamala Devi Harris kuwa mgombea mwenza katika kinyanganyiro cha Uchaguzi wa Rais utakaofanyika panapo mwezi Novemba mwaka huu.

Endapo chama chake kitashinda kiti cha Urais katika Uchaguzi huo, Kamala Harris atakuwa ni mwanamke wa kwanza, pia mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Afrika na Asia Kusini kuwahi kushika wadhifa wa Umakamu wa Rais katika historia ya taifa la Marekani.


FRANC THE GREAT,
Semper magnas.
 
Wahenga walisema: "Ahadi ni deni."

Mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kushika wadhifa wa Useneta katika bunge la Senate nchini Marekani anaitwa Carol Moseley Braun ambaye alitumikia nafasi hiyo mnamo mwaka 1993 hadi mwaka 1999 akiliwakilisha jimbo la Illinois.
 
Susan Rice. Ila yule Congress Woman kutoka California, Karen Bass anapigiwa chapuo kweli kweli. Anaweza kuibuka kidedea yule.
 
1. KAMALA HARRIS
View attachment 1525364


Bi Kamala Harris mwenye umri wa miaka 55 ni Mmarekani mweusi (African-American) mwenye asili ya Kijamaika upande wa baba yake na Kihindi upande wa mama yake anayetajwa kama mwanamke wa pili Mmarekani mweusi kushika wadhifa wa Useneta katika historia ya taifa la Marekani.
Mbona anatajwa kama African-American lakini Uhindi wake hautajwi?
Ndiyo yale yale ya kuaminishwa kuwa barack Obama alikua ni Mwafrika mwenzenu wakati ni nusu mwafrika na nusu mzungu, halafu huko Afrika alikuja tu kusalimia wakati kiuhalisia alilelewa kizungu na kusomeshwa expensive university lakini ninyi mkam dominate ni mwafrika mwenzenu.
 
Mbona anatajwa kama African-American lakini Uhindi wake hautajwi?
Ndiyo yale yale ya kuaminishwa kuwa barack Obama alikua ni Mwafrika mwenzenu wakati ni nusu mwafrika na nusu mzungu, halafu huko Afrika alikuja tu kusalimia wakati kiuhalisia alilelewa kizungu na kusomeshwa expensive university lakini ninyi mkam dominate ni mwafrika mwenzenu.
Ukisema hivi kule marekani watakuita Racist,Wakati ni Fact kabisa.
 
Susan Rice. Ila yule Congress Woman kutoka California, Karen Bass anapigiwa chapuo kweli kweli. Anaweza kuibuka kidedea yule.
Karen Bass ameingia katika shortlist na kuonekana kukubalika hivi karibuni kutokana pia ni kiongozi wa kundi la muungano wa Wabunge weusi (Congressional Black Caucus), Democrats wengi wanaamini ushawishi wake na CBC kwa ujumla utamsaidia Biden kujipatia kura nyingi kutoka kwa jamii ya Wamarekani weusi.

Kumekuwa na shinikizo kubwa ndani ya Chama cha Democratic linalopendekeza kusimamishwa kwa mgombea mwenza kutoka katika jamii za Wamarekani wasio weupe.
 
Mbona anatajwa kama African-American lakini Uhindi wake hautajwi?
Ndiyo yale yale ya kuaminishwa kuwa barack Obama alikua ni Mwafrika mwenzenu wakati ni nusu mwafrika na nusu mzungu, halafu huko Afrika alikuja tu kusalimia wakati kiuhalisia alilelewa kizungu na kusomeshwa expensive university lakini ninyi mkam dominate ni mwafrika mwenzenu.
Fikiria zaidi ya hapo mkuu!
Angekuwa muafrika angepataje uraisi marekani?
 
Mbona anatajwa kama African-American lakini Uhindi wake hautajwi?
Ndiyo yale yale ya kuaminishwa kuwa barack Obama alikua ni Mwafrika mwenzenu wakati ni nusu mwafrika na nusu mzungu, halafu huko Afrika alikuja tu kusalimia wakati kiuhalisia alilelewa kizungu na kusomeshwa expensive university lakini ninyi mkam dominate ni mwafrika mwenzenu.
Watu wengi wana misinterpret hili neno "African-American".

African-American ni Mmarekani mwenye asili ya Afrika. Hilo halina mjadala ila kuna baadhi yao wamechanganya asili zaidi ya moja kama huyo Kamala Harris. Nafikiri shida hapo iko katika ukamilifu wa utambulisho wake kwa sababu amekuwa akitajwa pia kama South Asian American.

Kwa upande wa Barack Obama, kusema kuwa alikuwa Mwafrika au kusema ni Mwafrika hivi sasa si sahihi. Obama ni African-American kwa maana ya kwamba ana asili tu ya Africa hata kama hakuwahi kuishi wala kulelewa Afrika ila si Mwafrika.
 
Kete iko kati ya Kamala Harris na Karen Bass! Sintashangaa kama Bass ataibuka mshndi! Ili Democrats wawe na majority kwenye senate; akiondoka Kamala kazi ya kuwa na senate majority inakuwa ngumu !! Kamala could as well become the next Attorney General.
 
Nawapenda sana Stacey Abraham, Mayor wa Atlanta, wa DC na San Francisco, ila nadhani atamteua Susan Rice au Kamala Harris.
 
Mbona anatajwa kama African-American lakini Uhindi wake hautajwi?
Ndiyo yale yale ya kuaminishwa kuwa barack Obama alikua ni Mwafrika mwenzenu wakati ni nusu mwafrika na nusu mzungu, halafu huko Afrika alikuja tu kusalimia wakati kiuhalisia alilelewa kizungu na kusomeshwa expensive university lakini ninyi mkam dominate ni mwafrika mwenzenu.
Tangu enzi za utumwa America, watu chotara huhesabiwa kama weusi. Mzungu akizaa na mweusi mtoto anaegemea Sana upande mweusi.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kulingana na taarifa za chini kwa chini: Kamala Harris pamoja na Susan Rice wanatajwa 'kuingia fainali' katika kinyanganyiro hiki kulingana na mchakato ulipofikia.

Nimesema: "taarifa za chini kwa chini".
 
Back
Top Bottom