Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,636
- 25,617
Mkuu JMushi,
Huyu Sam Bacile inaelezwa kwamba ni "property developer" na hajawahi kutengeneza filamu zozote na iweje leo hii atengeneze filamu kwa haraka hivyo na kufanya "timing" kuitoa wakati huu wa kampeni?
Inabidi tufikirie maana "foreign policy" ya USA siku zote imekuwa ni kusaidia kutingisha tawala za maeneo mengi ya mashariki ya kati ingawa kwa mahesabu makali sana.
Obama amepunguza majeshi nchini Iraq kiasi cha kuiacha nchi hiyo kwenye wimbi kubwa la vurugu za hapa na pale. Pia kuna mpango kwamba ifikapo mwaka 2013 majeshi yote yatakuwa yameondoka nchini Afghanstan.
Lakini Juzi kule Cairo Ubalozi wa US ulitoa taarifa kushutumu shambulio kwenye jengo la ubalozi huo kitendo ambacho kilipondwa na Romney kwa sababu ambazo bado sijazielewa.
Halafu Romney pia amesema kwamba "foreign policy" ya US ni "hit and miss" yaani akimaanisha kwamba kuna wakati inakuwa sawa na wakati inakosea malengo yake. Lakini juzi kwenye hotuba yake ya kupokea kupewa ugombea uraisi , Obama aligusia kwamba ni lazima US ijiondoe kwenye utegemezi wa mafuta kutoka nje akimaanisha mafuta kutoka mashariki ya kati, jambo linaokinzana na mawazo ya Republicans kwamba ni lazima ubeberu ukomae mizizi katika eneo hilo.
Wamarekani inabidi wafikirie upya hii foreign policy yao pamoja na uchumi wa ndani kwani ndivyo vitu vya msingi kabisa kuwaeleza wamarekani tofauti ya sera za Romney na zile za Obama.
Kwahio mimi nafikiri kwamba kwa sasa Obama atajaribu kuwatafuta waliohusika na mauaji ya Balozi Stevens maana ni tukio lililokuja bila kutarajiwa. Na wakipatikana watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na wamarekani watataarifiwa na Obama kupata sifa kama alivyofanya kwa Osama BIn Laden, na hayo yote yatafanyika kabla ya uchaguzi mwezi November.