Hivi mkuu
Elungata a.k.a chapombe ikipigika vita ya tatu ya dunia hivi kuna kitu kitakacho kuwepo kweli?
Na kama ikitokea basi ndio itakuwa mwisho wa dunia hakuna kitakachobaki
Man cannot destroy the earth, man can only destroy himself, these all mikwaraz and so, are there for scaring innocent people and those who are fighting for their rights, Whites like to demonstrate that are very superior; and are very desirous for the position of the Most High God, they would like to be WORSHIPED as well as God.
Urusi aliwahi kutandikwa kule Afghanstan, Marekani alichakazwa sana Vietnam ili kujiosha wakaanza kutuchezea sinema za uongo eti mmarekani mmoja anaua majeshi yote ya Wavietnam, Italia alipigwa hapo Ethiopia, hizo nyuklia haziwezi simama badala ya muumba eti zikaamua mwisho wa maisha, hata hapo Japani ilipopigwa kwa atomiki ni maeneo fulani tu yalidhurika na bado waliosavaivu walikuwepo. Si wakawamalize boko haram, IS IS, pia usisahau Marekani alikimbia hapo somalia mwaka 1992 kabla ya hawa Al Shabab na kushindwa vibaya.
Wakipigana hali itakuwa mbaya sana ila si mwisho wa maisha. Mkuu, yaani Mungu akiaamua hata leo mwisho unafika maana ana siraha nyingi zipitazo nyuklia, akishusha Mvua ya maana, akilipua Volkano, akiswich on Tetemeko la ardhi, akiwasha Kimbunga, akiamsha Tsunami, akifumua Radi, akazima Pumzi ya kila mwenye nayo anazima kelele za ulimwengu kwa dakika tu. Tena yeye aweza tumia chochote kati ya hayo, hapo nimeacha ukame, Magonjwa na tusiyoyafaham.
Binadamu wenzetu wengi wamepewa uwezo mkubwa sana wa kuiitiisha nchi lakini wasitudanganye kwamba eti kulala na kuamka wanaweza zimisha uhai, na wao wanafahamu hilo ila sisi tuliowapa umungu ndo tunafikiri uongo huo ni ukweli.
Kumbuka taifa mama kama marekani limekuwa na migogoro na uadui na mataifa mengi ambayo ingekuwa chini ya uwezo wake lingeyafuta kabisa, fikiri juu ya uadui wa miaka na korea ya Kaskazini, Cuba, Iran, Iraq, Vietnam, Lybia (uadui ulianza mwaka 1804 lybia ikiitwa tripolitania), nikaragua na China ya enzi hizo, kwa nini wasingewamaliza tuu kama wao na wazungu wenzao wameshika uhai wa dunia?
Kweli tukubali kazi za wazungu pale penye ukweli unaostahili tusikufuru tukawakabidhi mamlaka ya Mungu. Si wazuie kifo basi, mbona kinatutawala wote ili hali kwao kuna kila teknolojia.