Uropokaji huu wa Membe utaibua upya mzozo wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Tanzania


kitu kama kweli M23 ni wanyarwanda taabu ipo wapi? Kama alichosema Membe ni uongo uuthibitishe uongo wake. Na hawa wapinzani hamjawajua bado, wanatafuta umaarufu na kutetea wananchi waliowapeleka bungeni. Think Big.
 
Membe karefer report ya UN sasa sijui tatizo liko wapi.Halafu uwe unapenda pia kujisomea ili ujue kuliko kutumia mawazo ya watu maana nina uhakika ungesoma kuhusu march 23 nadhani ungewaelewa sana
 
Repory ya UN ndio inasema M23 ni watusi,sasa wewe una mwandama membe kwa vile ni shemeji yako
 
You know nothing about Americans attitude toward Rwanda, They are much closer than you think!You can't separate France from the DRC conflict too!!
 
Mnacho kosea Chadema ni kutaka kupinga kila kitu! Kuna siku mtapinga kuwa Boko Haram sio Wanigeria!
That's absurd,Really! I hope you also noticed how foolish you sound with such stupid remarks if you have any brain left in your pumpkin like head! Didn't you?
 
Jamani tuwe waangalifu wakati wa kuishi na majirani na Wah MaRais Kikwete na Kagame wanaendelea vizuri katika maongezi yao na kidiplomasia bado wako vizuri. Hayo ya Membe it's totally uncalled for ni vema tukawa waangalifu na jinsi tutumiavyo ndimi zetu ulimi wa membe utatuponza sie watu wa chini....hakina kitu kibaya kama vita.....bado hatujafungua mikanda tangu ya Idd Amin...mwenye macho haambiwi tazama KARAGABAHO.
 
Niliwahi kuandika hapa juu ya maovu ya ndugu Kagame, ni mvivu pekee wa kusoma ambaye hatoamini kua M23 walnafadhiliwa na Kagame na kaka yake Museven, CIA ambao ndo walijifanya waandishi wa habari walilifanya hili kwa ustadi mkubwa sana na baadhi ya mawasiliano ya Kagame na viongozi wa M23 ylinaswa muda mrefu na vikao vya Kagame na ndugu zake vingi vilifanyika Gisenyi nyakati za usiku au katika wilaya ya Nyagatare ndo walifanyia vikao vyao.
 
Weka hiyo ripoti tuione
 
Suala la Chadema kumfagilia Kagame ni kutaka ufadhili wa uchaguzi mkuu kama walivoanza mazungumzo na maafisa usalama wa Rwanda na hili linafahamika wazi, hakuna diplomasia tena kwa mtu anaewatesa Watanzania wanatumia mpaka wake au waishio kwake tena huku wakijisifu kukomesha na janja yake ya maafisa wake kutumia Passport za Uganda ili kuingia TZ kirahisi ilishagunduliwa asidhani haifahamiki vyema, lazima ukweli usemwe na usibembeleze urafiki na adui asiependa muafaka na wewe huo ni utumwa.
 
Huyu Membe ningemshauri ajaribu kufanya mawasiliano na kina Joshua Arap Sang na wenzake wampe mwongozo wa kinachoendelea pande za THE HEGUE ili walau apate tips za kinachojili huko kwani ulimi ni kiungo kidogo sana ila kisivyotumika sawa sawa kinaweza kukuletea majanga.
 
Naipenda CHADEMA, ila hapa nimekuwa na wasiwasi mkubwa. Kauli si ya Membe ni ya UN. Alichosema Membe hata Lipumba (team UKAWA) aliunga Mkono MUNUSCO. Nimeionea huruma CDM
 
Hapa sasa naona kwa mbaaaaali vita kamili vya nchi na nchi na ukizingatia ile mikwara ya juzi kati kwenye sherehe za Muungano!. Nahisi kitu.
 
Everybody knows kwamba wale ni wanyarwanda swali la msingi:kulikuwa na haja ya kutaja jana bungeni kwamba m23 ni wanyarwanda?
 
mtoa mada naona una ushabiki wa kisiasa maana umeamua kuchagua ya kuandika. cha kushangaza zaidi unaleta mada kwa kusikia hotuba ya membe bila ya kufanya uchambuzi wa kutosha. gazeti la serikali la rwanda linaisema tanzania na familia ya rais vibaya kwa makala zisizo na miguu wala kichwa. tanzania na rais anatukanwa halafu unaleta ushabiki maandazi. haya ni mambo ya kitaifa hayana chama. rais ni taasisi na tanzania ni yetu sote. watu kama wewe + upinzani maandazi = janga la tiafa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…