miss chagga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 57,802
- 49,110
Habari zenu wana JF
Kama kichwa kinavyojieleza nimeona niongelee jambo linaloniumiza kichwa japo bado sijapata mtoto ila naona namna watoto wanavyokosewa na wazazi wao.
Wazazi baadhi yetu tumekuwa wabinafsi kiasi kwamba tunaishi leo tumesahau kesho, nikiwa na maana ya kwamba unapokuwa na mtoto huyo ndiyo kesho yako na zaidi ya miaka hamsini.
Kwa nini urithi wetu duniani tunaucha katika hali ngumu ya majuto na hata kupoteza mwelekeo?
Umeshawahi jiuliza urithi wako unauachaje hapa duniani (nikiongelea urithi namaanisha mtoto), tumekuwa wepesi sana kuwekeza katika ardhi, majumba, mali nyingi tukasahahu kuwa tunatakiwa kuwekeza kwa watoto wetu, tumejifunga zaidi katika kuwapa watoto elimu za darasani ambazo kiuhalisia hazitumiki katika maisha yetu ya kila siku, tukaacha elimu jamii na hata vitendo.
Kwa nini nasema wazazi tumekuwa wabinafsi unakuta mzazi unacheo kikubwa serikalini au kampuni fulani na unalipwa vizuri tu unaamua kumlea mtoto kilege lege ajishughulishi na kazi yeyote ya kijamii kama kupika, kusimamia miradi na hata kulima pale mzazi anapokuwa na uwezo wa kuwa na shamba, wapo ambao wanamashamba lakini uliza ni lini mtoto wako kaenda shamba kuona hata wafanyakazi wako wanafanyaje? Mtoto amekuwa mtu wa kuona vitu ndani bila ya kujua vinapatikanaje. Sina maana tuwatume wakatafute unaweza mfundisha tu namna ya kutumia hata kutunza, si mtoto anaharibu vitu unamwacha tu kwa kuwa unauhakika kesho utapata kingine.
Inahuzunisha sana kuona mzazi anapoondoka duniani future ya mtoto inapotea kabisa na kubaki na historia kuwa baba alikuwa anahela nyingi lakini havioni.
JIULIZE URITHI WAKO UMEURITHISHA NINI?
Labda ni uvivu na unyanyasaji wa wafanyakazi na hata dharau?
Labda ni ni kumpiga mke au kumtukana mume?
Au ni moyo wa hekima na ukarimu?
Au umemrithisha uchapaji kazi wa hali na mali?
Ni vizuri na busara kumkuza mtoto katika njia ambayo hata usipokuwepo duniani leo anaweza kusimama na kutetea haki yake.
Wazazi wengi wamekufa wameondoka na mali zao na kwa kuwa ndugu wametapanya na kupoteza kabisa na kuacha watoto katika hali ngumu ni huzuni kwa kweli, mkuze mtoto hata akiwa na miaka minne unaweza anza kumwambia kama story tu lakini ndiyo ukweli, tuishi kesho tusiishi leo, leo ni wewe kesho ni mwanao.
Nawatakia malezi mema ubarikiwe.