Sasa Kifupi ni kwamba mkuu Pundit kaandika mapungufu ya rais wetu (BLACK) ambayo nayakubali lakini wakati huo huo mimi nimewakumbusha mazuri ya rais Kikwete (WHITE) hivyo tunapoweka vitu hivi ktk mzani ni rahisi kwetu kuona huo mzani umeelemea upande gani ili tupate kuona hiyo Grey color ktk kupata balance!..
Bulesi,
Mkuu wangu nawe umechanganya.. Mimi huwa nafuatilia sana habari zilizopita hapa JF na kwa bahati nzuri Mungu kanijalia kukumbuka yaliyopita ingawa sii yote..
Rostam Aziz alikuwa mweka hazina wa CCM toka kipindi cha Mkapa na hasa wakati fedha zile za EPA zikichotwa..Record ya utumishi wake kama mweka hazina wa chama imebadilishwa ktk site ya CCM kiasi kwamba huwezi kumfunga Rostam na EPA lakini nakuhakikishia kwamba Rostam alikuwa mweka hazina na kuna moja ya mada humu ndani niliwahi kuweka hyperlink..nakumbuka sana ilikuwa ikihusu uchaguzi baada ya FMES kutushtua kuhusu mtu huyu ajulikanaye kama Rostam. Hizi habari za kusema Solome Mbatia ndiye alikuwa mweka hazina wakati wa EPA zimepigwa ubatizo na RA mwenyewe na pengine yawezekana kabisa kuwa ni sababu ya kifo chake!.. Mimi natilia mashaka sana ajali ile hasa wakati swala hili limefikia hapa..
Huwa najiuliza hivi ingekuwa vipi kamam marehemu angekuwa hai kwa sababu ktk record ya leo ndiye anayeonyeshwa kuwa mweka hazina wa chama.!
The fact ni kwamba hatukuwa tukifahamu nguvu na uwezo wa RA hadi mambo yalipoanza kujitokeza kulingana na maelezo ya FMES, huyu mtu hakupanda ngazi zote hivi hivi tu...
Sasa nirudie neno moja kwamba fedha za EPA zimechotwa wakati Mkapa ambaye ndiye alikuwa rais wetu na fungu kubwa (ambalo halizungumziwi) limetumika ktk kampeni za uchaguzi. Viongozi wote wa awamu ya nne wanaohusika wote walikuwa na nafasi ndani ya Utawala wa Mkapa. Na wengine bado wapo nje wala sintashangaa kusikia kama Sumaye pia kahusika...Kwa mshahara gani aliweza kutajirika ghafla kiasi hicho!
Inasemekana, (kulingana na habari za Mtaani) CCM walikubaliana kuchukua robo tu ya fedha zilizochukuliwa..Sasa kwanza ni swala la kujiuliza nani aliyepitisha fedha hizo zitoke kwa mashirika ya niaba yaa..kwa sababu haiwezekani mashirika kuundwa haraka kiasi kile na kupewa fedha bila kipenga cha la mgambo...
Kwa maana nyingine nachukulia kichwa cha mada hii - Urithi wa Kikwete na haiba iso sababu ina maji marefu zaidi ya dimbwi la fikra.. kwani ukitazama 1. Urithi na 2. Haiba, tunaweza kuona kina kirefu cha ya maji haya ktk kujenga sababu.
Wakati huu tunapoelekea uchaguzi nikaona niirudishe hii masterpiece ya kaka yangu "Pundit" tuendelee kuichambua.
Ha ha ha,
Nasubiri kuona ukitoa conclusion kuwa .. Kikwete amethibitisha kuwa hafai kwa sasa, tuchague mtu mwingine kuwa raisi wa Tanzania
Duh,
Pundit kapotelea wapi?
Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza, ulishapata kulinganisha maoni ya kaka yangu "Pundit" na maoni yangu?
Mbona nilishasema vote CHADEMA ku close the gap na ili tusirudi kwenye single party system? Au ulitaka nisemeje ?
Kiranga said:Huwezi kujua hili kwa hakika bila kuwapa muda wa kutosha kujionyesha true nature yao ndani ya upinzani. Inawezekana wamekuwa mzigo hata CCM ndiyo maana wakatoswa.
Ndiyo maana wengine tunapendekeza wapewe muda mpaka 2015 waangaliwe.
Last time niliangalia, ulisema hivi:
Mbona una comprehension ndogo? Au unataka ku distort mambo? Angalia nilikuwa naongelea nani wapewe muda mpaka 2015, mamluki kina Shibuda wanaotaka kuingia CHADEMA kwa sababu wamenyimwa nafasi ya kugombea ubunge CCM wasipewe nafasi kugombea ubunge CHADEMA, wapewe muda wa kuji prove mpaka 2015 ili tuone kama CHADEMA wamefuata chama na sera zake au wanataka kutumia CHADEMA kama ngazi ya kupatia ubunge bila kujali chochote kuhusu chama hiki.
Jaribu kusoma posts kabla ya kukurupuka na kuona contradiction sehemu ambayo hata hamna a whiff of contradiction. Unatuonyesha usivyo na comprehension.
Kiranga said:Mazee ningependa watu wengi zaidi wa vote CHADEMA, only because naamini tunahitaji mabadiliko.
Lakini at the same time siamini kwamba CHADEMA watashinda urais au kuwa na majority ya viti vya bunge. Nisingependa kuona CHADEMA wanashuka chini kutoka asilimia za kura za urais walizopata 2005 (11%) wala kupunguza viti vya bunge.
Lakini for sure CHADEMA nao bado hawako ready for prime time, ndiyo maana naona ni bora kuwe na gradual change, wapate tough love hapa, kama wana moyo wa kujifunza waweze kujifunza, labda 2015 au 2020 wataweza kuchukua nchi with confidence.
Kweli hapa nakubali makosa nimeleta wrong quote (kwa msemo wako nimekurupuka). Quote niliyotaka kuleta ni hii hapa:
Ha ha ha,
Nasubiri kuona ukitoa conclusion kuwa .. Kikwete amethibitisha kuwa hafai kwa sasa, tuchague mtu mwingine kuwa raisi wa Tanzania
Originally Posted by Kiranga
Mazee ningependa watu wengi zaidi wa vote CHADEMA, only because naamini tunahitaji mabadiliko.
Lakini at the same time siamini kwamba CHADEMA watashinda urais au kuwa na majority ya viti vya bunge. Nisingependa kuona CHADEMA wanashuka chini kutoka asilimia za kura za urais walizopata 2005 (11%) wala kupunguza viti vya bunge.
Lakini for sure CHADEMA nao bado hawako ready for prime time, ndiyo maana naona ni bora kuwe na gradual change, wapate tough love hapa, kama wana moyo wa kujifunza waweze kujifunza, labda 2015 au 2020 wataweza kuchukua nchi with confidence.
Unataka nini zaidi kiumbe mwenye husda wewe ? Kijicho gani hiki?
What's going on here?
hicho ulichoweka hapa ni a qualified statement....
I would like ....BUT
Ungependa...LAKINI
Lakini hiyo imepinga kupenda kwako. Wewe ni mtaalamu wa lugha (kwa mtizamo and gawd you are so goood) na unajua vyema kabisa matumizi ya neno LAKINI (BUT)