Urgent message for Vodacom...

Urgent message for Vodacom...

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,252
Reaction score
11,648
Naomba kama kuna mtu yuko karibu na Vodacom anifikishie ujumbe kwamba mtandao wao sasa unazidi kukera wateja.

Nimeweka pesa muda mfupi uliopita na kununua bundle ya Tsh 4200 kwa ajili ya kupiga mitandao yote. Jambo la kusikitisha ni kwamba siwezi kupiga simu kwa sababu naambiwa sina salio wakati nikiangalia balance ya bundle ninazo sekunde 10,035, SMS 9255 na MB 3294.

Nikijaribu kupiga customer care simu yao haipatikani.

Ahsante sana kwa yeyote atakayeweza kunisaidia.
 
Kweli jamaa kwasasa wako vibaya

But why?

Kwa nini hawatoi taarifa au hawafungi hizo huduma ili pesa za wateja zisichukuliwe?

Naona kama ni utapeli huu...

Kama kuna mtu ana namba ya watendaji wao basi anisaidie niwapigie....
 
But why?

Kwa nini hawatoi taarifa au hawafungi hizo huduma ili pesa za wateja zisichukuliwe?

Naona kama ni utapeli huu...

Kama kuna mtu ana namba ya watendaji wao basi anisaidie niwapigie....

Babu ni kwamba hakuna wa kutetea wanyonge hao viongozi wengi wanatumia voda kwa hiyo hii tabu wanaipata ila ndo no one real cares!!!!!

Internet yenyewe imekuwa pangu pakavu tia mchuzi
 
nenda kwenye page yao Facebook!! Wanasaidia sana Watu Kule
 
Babu ni kwamba hakuna wa kutetea wanyonge hao viongozi wengi wanatumia voda kwa hiyo hii tabu wanaipata ila ndo no one real cares!!!!!

Internet yenyewe imekuwa pangu pakavu tia mchuzi

Hata kama hatuna wa kututetea, hatuwezi kujitetea?

Kwa nini tusitumie social media na outlets nyingine kupiga kelele?

We need to do something...
 
kwa kweli tigo wanajitahidi sana kuhusu bundles. nimekua nikitumia kabaang toka ilipoanzishwa na hakuna hata siku moja imesumbua. unapiga hong kong, usa, nk. internet ta kweli kwa wiki bila usumbufu. sijui baadae kama watabadilika. ila kwa sasa wanajitahidi.
 
Ahsante Amina Thomas,

Ila kama mimi siyo mtumiaji wa Tigo na hawa Vodacom tayari wamekwapua pesa zangu..

Hawa jamaa tukiendelea kuwaendekeza watatumaliza kabisa...
 
Last edited by a moderator:
kwa kweli tigo wanajitahidi sana kuhusu bundles. nimekua nikitumia kabaang toka ilipoanzishwa na hakuna hata siku moja imesumbua. unapiga hong kong, usa, nk. internet ta kweli kwa wiki bila usumbufu. sijui baadae kama watabadilika. ila kwa sasa wanajitahidi.

hongkong Kwa kabang?
 
Kuwapata voacom fasta piga customer care ya VIP namba 15366 ila watakukata sh 50

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hamia Airport. Ah samahani Airwing, mmh sijui mtandao gani ule wanaita. Hebu nadhani Airforce. Hahahaha Airtel Bwana.
 
mi nshahama zangu...haya mauza uza sijui net hamna mara network hakuna sijui txt haziend...acha niende airtel bana!!
 
nimejiunga blakberrry service ya mwezi na inaisha tarehe 28 kesho ila tokea tarehe 24 sipati huduma nikiwapigia kila siku wananiambia inashughulikiwa na siku zinaisha bila service yeyote sipati net sipati chochote
 
Back
Top Bottom