Coach Slamah Hamad
JF-Expert Member
- Nov 12, 2014
- 3,430
- 4,336
Inatakiwa busara itumike. Mazingira ya huko vijijini hakuna elimu na uelewa hivyo maisha kama haya ndiyo kawaida yao. Hawajui hata kama wanavunja sheria. Hivyo naishauri serikali isi-over react kwa kufunga watu miaka 30. Japo kutojua sheria siyo utetezi lakini itakuwa siyo vizuri kufunga watu miaka 30 kwa mazingira ya aina hiyo.
Seriously?!
Yaani tunalalamika kila kukicha kuitaka serikali na vyombo vyenye mamlaka kusimamia katiba, kufuata sheria na ku- exercise utawala bora na hapo hapo kati yetu wapo watu wanaowaza Kama wewe!
Kutokujua sheria sio kinga ya kuwajibika kisheria, na sheria haina macho ila ina mikono yenye mizani na upanga.
Watanzania ni wanafiki sana!