Alwaz
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,115
- 10,822
Ureno kwa nchi za Afrika Mashariki iko pembe ya mbali sana na mbele ya kaskazini magharibi ya Afrika.Hata hivyo eneo hili la Afrika limejaa historia inayofungamana na Ureno kuanzia Kenya mpaka Msumbiji.
Hii nchi inayojulikana rasmi kama Porugal kwa sasa inajinasibu sana na Ukristo wa madhehebu ya kikatoliki.Pamoja na kwamba kwa sasa ni moja ya nchi maskini za Ulaya na yenye watu wachache lakini watu wake hapo mwanzoni mwa karne ya 19 waliweza kusafiri mbali kwa nia tofauti na hatimaye kumudu kuwa na makoloni Afrika kama wenzao wengine wa Ulaya.
Mmoja ya raia wa Ureno anayetajwa kama mvumbuzi ni Vascoda Gama.Lakini ukweli ni kuwa yeye alikuwa na kinyongo sana na waislamu ambao walikuwa wameitawala Ureno na Uhispania kwa karne kadhaa kuanzia mwaka 711 AD wakiwa katika himaya moja ya kiislamu iliyojulikana kama Andalusia.
Katika mwaka huo jeshi la waislamu chini ya Tariq bin Ziad waliweza kupenya ngome za utawala wa Visigoths na kuanzisha utawala ambao ulikuwa neema kubwa kwa ulimwengu mzima na Andalusia ikawa sehemu ambayo maendeleo ya kila aina ya kisayansi kutawanywa kuingia nchi za Ulaya ya leo.
Utawala huo wa waislamu pamoja na kutokuwa na uadui na yoyote lakini kulikuwa na mbinu za kichichini kwa hamasa za kidini.Hii ilipelekea kutokea kwa vita vingi na mauwaji ya waislamu na hata mayahudi .Kila wareno waliposhinda walifanya ukatili mkubwa na kujaribu kujitanua kwenye maeneo ya waislamu mpaka pale mwaka 1578 waliposhindwa vibaya kule Maghrib (Morocco ya leo).
Hata hivyo mbinu hizo hazikusimama moja kwa moja na hatimaye kwa kukua kwa uadui na ushirikiano wa mataifa mbali mbali yaliyokuwa na chuki za kidini mbinu hiyo ilifanikiwa kuungusha utawala wa kiislamu uliojulikana kama Ottoman Empire kipindi cha vita kuu ya mwanzo ya dunia.
Inakisiwa wareno ni miongoni mwa watu wenye ukatili zaidi katika utawala wao na hasa kwa waislamu kati ya wakoloni waliowahi kuzitawala nchi za waislamu.Na hata Vasco da Gama hakuwa mvumbuzi bali alikuwa muwindaji wa maendeleo ya waislamu popote duniani baada ya waislamu kushindwa kule kwao na kuuliwa kwa wingi.Alikusudia kuwanyan'ganya waislamu uchumi na udhibiti wao wa biashara ya viungo kutoka India ambayo ilikuwa imeshamiri sana.
Pamoja na kuongozwa kiteknolojia na nahodha mahiri wa kiislamu Majid kutoka Oman kufika India lakini Vascoda Gama hakuwacha kinyongo chake.Katika moja ya safari yake iliyofuata Vascoda Gama aliweza kuichoma meli ya waislamu iliyokuwa imebeba mahujaji kuwarejesha makwao na kuwauwa wote.
Hii leo kule Ureno waislamu wamebaki asilimia 0.5 tu kati ya watu milioni 10 kutokana na kuuliwa na kulazimishwa kuingia Ukristo.Hali ni tofauti kidogo na eneo la Spain ambayo baadae ilikuwa kitovu cha utawala wa kiislamu enzi hizo,kwani nchini Uhispania waislamu ni wengi zaidi na nembo za kiislamu zimebaki hadi leo na kubaki kuwa fakhari ya dunia yanapotajwa maendeleo ya kisayansi na kielimu kwa ujumla.
Pamoja na yote yaliyotokea siku za nyuma utafiti sasa umegundua lugha ya kireno imejaa maneno yenye asili ya lugha ya kiarabu iliyotumiwa na waislamu wakati wakiwa watawala wa Andalusia kwa karne kadhaa.Vile vile watafiti wa mambo ya kale ambao ni wazaliwa wa Ureno wamegundua majengo mengi na vitu vya kihistoria ambavyo haviwezi kutenganishika na historia ya Uislamu katika nchi hiyo.Historia kama hiyo imekuwa wazi zaidi katika mji wa Mertola. Hata misikiti iliyosalimika kuvunjwa na iliyogeuzwa kuwa makanisa pia imebaki na athari zake za nembo za kiislamu.
The Portuguese rediscovering their country's Muslim past