Urais wetu usitafutwe kwa njia za panya

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
Wanaotaka Urais wajitokeze tuwajue.
Wakijitokeza tutawauliza wanataka kwenda Ikulu kuifanyia nini Tanzania.
Tutawauliza wana uwezo wa kupambana na ufisadi na uhujumu uchumi unaotikisa nchi?
Tutawauliza wanajua ndugu zetu vijijini wanakabiliwa na umasikini uliopindukia na mipango ya maendeleo iliyoanzishwa na Nyerere imekufa?
Je, wanajua kwamba huduma za kijamii upatikanaji wake umekuwa ni mgumu na wa gharama?
Watapaswa kusema wanawezaje kukabiliana na ujangili wa kutisha unaoangamiza utajiri wa wanyama pori nchini.
Nataka kujua Wanaotaka Urais wa watawezaje kutaifisha nyumba za serikali zilizouzwa na Akina John magufuli na watawezaje kutaifisha maeneo muhimu kiuchumi ambayo mikataba Yao iliingiwa kifisadi? Ipo migodi ya madini, mashirika nyeti kama NBC, TANESCO na TTCL.
Kwa mantiki hiyo, naona kwamba Sasa si wakati wa kutafuta Urais kwa njia za panya.
Mipango mikakati ya chini kwa chini yenye kufuata njia haramu za kutumia fedha, haiwezi kupatia Taifa Rais mwadilifu, mzalendo na mwaminifu.
Wakati ndo huu wanaotaka Urais wetu wajitokeze umma uwapime kwamba wanataka kuifanyia Tanzania na si kuutafuta kwa njia za panya.
 
Back
Top Bottom