Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,289
- 2,472
Hii ina mantiki sana. hapa kwetu katiba inasema ni miaka 40. laiti kama katiba ingesema ni miaka 60 basi hali isingekuwa shwari.Lakini kuna mambo huenda bila kusemwa.Hili liwe mojawapo.Rais wa nchi achaguliwe alifikisha miaka 60 ili akimaliza muhula wake apumzike maana atakuwa na miaka 70 kama atajaliwa afya na mihula miwili.
Hivi mtu anachagiliwa kuwa rais akiwa na miaka 40.Baada ya miaka kumi anamaliza mihula yake na ana miaka 50.Sote tunaujua ulevi na ukuu wa Urais. Hivi huyu kijana wa miaka 50 ambaye kamaliza mihula yake miwili na anakabidhi kijiti kwa mwingine kweli ana amani?
Baada ya kuwa Rais na una miaka 50 utakuwa unafanya nini?Hivi alishawahi ulimwenguni humu mtu kuwa Rais na baadae akawa aidha waziri na akaishi kama waziri?Msiniambie kuhusu Putin.Huyu ambaye damu inachemka atakuwa kero.
Mtazameni Nkurunzinza wa Burundi.Mtazameni kabila wa Congo.Msiniambie kuhusu Mugabe maana anajua the Hague inamhitaji akiachia Urais.Mugabe atafia madarakani.
Hebu mtazameni Kagame,same kwa Museveni alikuwa Rais akiwa na umri mdogona leo ana zaidi ya miaka 20 madarakani.Hawa vijana kina Kabila na Nkurunzinza wanawatazama hawa watu kama role models wao.Wanaamini dola itawahakikishia hitaji lao kama inavyoelekea kwa Nkurunzinza.
Hapa kwetu nasikia kuna vijana wanautaka urais, nasema hizi kamati kuu za vyama iwe CCM au UKAWA wasikubaliane na haka kawimbi kanachotaka kupandikizwa vichwani mwa watanzania.Afrika si ulaya,kwetu haya mambo makubwa kama utawala wa nchi tuwaachie wazee.
Nawaambia hivi, hakuna kitu kama hicho kwa kijana wa miaka 40 kushika dola. Tafuteni umri kwanza, kipindi hiki cha ujana bado ni cha kujifunza, hasa igusiwapo taasisi ya Urais.