Urais uanzie miaka 60

Urais uanzie miaka 60

Mleta uzi umeona mbali hata Nyerere alishawahi kumwambia mgombea mmoja subiri ukiwa rais katika umri huu mdogo unaweza kua dikteta ukataka ubadili katiba

Nyerere aliingia Ikulu akiwa na umri gani? Je, aling'ang'ania madaraka?
 
Kwa nini wananchi wa Afrika hatujiamini?Hizi ni zama za demokrasia,utawala wa watu kwa ajili ya watu. Zama za madikiteta zimeshapitwa na wakati.Katiba ndio nchi na nchi ndio katiba,sasa Rais alieapa kwa katiba hiyo kisha akaigeukia na wananchi wanamwangalia tu hiyo siyo nchi.Kuanzia miaka 40 kuchukuwa madaraka ni sahihi kabisa kwani ndio miaka ya kuanza kukomaa kiakili,na uwongozi unahitaji stamina na stamina ya akili na kimwili tutaipata kuanzia miaka 40.Hiyo miaka 60 tunawaona wabunge wa umri huo wakilala bungeni sembuse leo Rais,ututaki kutawaliwa kwa niaba na wake zao na waramba viatu vyao.Waafrika inabidi tujiamini madaraka ni dhamana na wala sio mali ya mtu binafsi.
 
Kuna rais wa Filipino Glory Aroyo baada ya urais alirudi kugombea ubunge ila sikumbuki kama alishinda. Bahati mbaya pia baada ya kustaafu urais alipata misukosuko ya kesi za ufisadi. Kwa upande wangu naona miaka 50 ndio yafaa kuanzia.
 
Hakuna tofauti ya waafrika na wazungu tukiacha tamaa mtu aweza kuwa raisi hata @40 years na akaongoza vyema na muda ukifika wa kutoka ataachia ngazi.
 
Kwa nini wananchi wa Afrika hatujiamini?Hizi ni zama za demokrasia,utawala wa watu kwa ajili ya watu. Zama za madikiteta zimeshapitwa na wakati.Katiba ndio nchi na nchi ndio katiba,sasa Rais alieapa kwa katiba hiyo kisha akaigeukia na wananchi wanamwangalia tu hiyo siyo nchi.Kuanzia miaka 40 kuchukuwa madaraka ni sahihi kabisa kwani ndio miaka ya kuanza kukomaa kiakili,na uwongozi unahitaji stamina na stamina ya akili na kimwili tutaipata kuanzia miaka 40.Hiyo miaka 60 tunawaona wabunge wa umri huo wakilala bungeni sembuse leo Rais,ututaki kutawaliwa kwa niaba na wake zao na waramba viatu vyao.Waafrika inabidi tujiamini madaraka ni dhamana na wala sio mali ya mtu binafsi.

viongozi ndio hawajiamini. kwa nini mtu apindue katiba aliyoapa kuisimamia? hilo hauoni unaona tu udhaifu wa wananchi. miaka 60 bado mtu yuko katika kiwango cha kumtosha kiafya na kiakili na kihekima ndugu
 
Robert Mugabe na ICC??tatizo watu wengi hawajui ICC inahusika na nin.

ICC inahusika na kesi za mauaji ya kimbari na sio vinginevyo.Kukaa madarakani muda mrefu ata kama ikiwa ni kinyume cha katiba haihusiani kabisa na ICC, ICC inahusika tu kama kuna mauaji ya kupangwa dhidi ya halaiki ya watu.Hakuna kitu chochote juu ya Mugabe kwenye angle hiyo.

Hivyo hawezi kabisa kupelekwa huko ata akijiuzulu kesho.
 
Kulikuwa na mjadala mkali hapa nchini kundi fulani likitaka rais ajaye awe ni yule aliyezaliwa baada ya 1961 huku kundi hilo likisema ni zamu ya vijana. Rais mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema ataiacha nchi mikononi mwa kijana. Wapo pia waliopinga wazo hilo, kuna kiongozi wa dini aliwahi kusema nchi haijafikia kiwango cha kuongozwa na wanyoa vipara na wafunga milegezo.

Kama watanzania sasa tunaweza kujadili kwa upana baada ya matukio ya Burundi, watu wanasema kinachomsukuma Nkurunziza kung'ang'ania madaraka ni umri wake. Ana miaka 51, rafiki yangu mmoja akaniambia ukisha kuwa rais huwezi kuomba kazi nyingine wala kufanya biashara. Akaniuliza sasa kwa umri wa Nkurunziza unadhani ataenda kufanya nini? Akaniuliza unaona Congo? Kabila anajaribu kukatalia madarakani kwa sababu zile zile.

Je, watanzania tumepata funzo? Tuko tayari kumkabidhi nchi yetu kijana? Je bwana mkubwa amebadili mawazo ya kumuachia nchi kijana baada ya kuona swaiba wake alichofanya Burundi?
 
Hoja yako haina mashiko. Sio vijana wote wanaoshika nafasi ya urais kwa umri mdogo wanaleta matatizo. Mifano ipo mingi sana.

Lakini pia, tukiongelea wazee, Mugabe alishika dola akiwa na umri gani? Mbona hizo sijui busara, hekima mara hofu ya Mungu hatuioni kwa mtu kama Mugabe?

Vijana wapatiwe fursa sawa na tunapaswa kuaminiana.

Wazee kama Mbowe na Slaa huko CHADEMA mbona wanafanya hayo hayo ya Nkurunziza?

Undetoa mifano ya hao waliotawala wakiwa na umri mdogo na kuondoka kiustarabu ingekuwa vizuri Sana.
 
Kulikuwa na mjadala mkali hapa nchini kundi fulani likitaka rais ajaye awe ni yule aliyezaliwa baada ya 1961 huku kundi hilo likisema ni zamu ya vijana. Rais mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema ataiacha nchi mikononi mwa kijana. Wapo pia waliopinga wazo hilo, kuna kiongozi wa dini aliwahi kusema nchi haijafikia kiwango cha kuongozwa na wanyoa vipara na wafunga milegezo.

Kama watanzania sasa tunaweza kujadili kwa upana baada ya matukio ya Burundi, watu wanasema kinachomsukuma Nkurunziza kung'ang'ania madaraka ni umri wake. Ana miaka 51, rafiki yangu mmoja akaniambia ukisha kuwa rais huwezi kuomba kazi nyingine wala kufanya biashara. Akaniuliza sasa kwa umri wa Nkurunziza unadhani ataenda kufanya nini? Akaniuliza unaona Congo? Kabila anajaribu kukatalia madarakani kwa sababu zile zile.

Je, watanzania tumepata funzo? Tuko tayari kumkabidhi nchi yetu kijana? Je bwana mkubwa amebadili mawazo ya kumuachia nchi kijana baada ya kuona swaiba wake alichofanya Burundi?
JK inabidi afikiri upya kauli mbiu yake ya kuwaachia vijana. Hata Mwalimu aliona mbali sana hadi kutengeneza mazingira ya kumwengua jk mwaka 1995
 
Robert Mugabe na ICC??tatizo watu wengi hawajui ICC inahusika na nin.

ICC inahusika na kesi za mauaji ya kimbari na sio vinginevyo.Kukaa madarakani muda mrefu ata kama ikiwa ni kinyume cha katiba haihusiani kabisa na ICC, ICC inahusika tu kama kuna mauaji ya kupangwa dhidi ya halaiki ya watu.Hakuna kitu chochote juu ya Mugabe kwenye angle hiyo.

Hivyo hawezi kabisa kupelekwa huko ata akijiuzulu kesho.
Asante kwa taarifa. Unadhani ni kwa nini Mugabe hataki kuondoka madarakani?
 
Nakubaliana na umri was urais ili kuepuka watu kutamani madaraka makubwa wakiwa back ni mabachalor na ukijana unawasumbua
 
Tunatakiwa tujiamini,
Miaka 40 ndio umri mzuri kabisa kwa mtu kufikiria na hatimaye kugombea urais
Miaka 60,tunayo mabunge mengi sana yanayoanzia miaka 60 yapo bungeni yanalala tu na sisi wenyewe ndio walalamikaji na tunataka vijana wapewe majukumu,leo rais aanzie 60,miaka 40-50 ndio umri ambao akili iko very active,huko 60 imeshachoka japo hatukatai ndio umri uliojaa busara lakini hata vijana wana busara pia,swala la rais kugoma kutoka madarakani likifanyika wa kulaumu ni wananchi na sio Rais,angalieni Obama miaka 55 tu keshamaliza Terms zake 2,waafrika tubadilike ila kikubwa tuache Uoga.
 
Hiyo miaka 40 ni kweli akili iko active kwa mengi. Mojawapo ni kupindua katiba. uzuri ni kuwa urais ni taasisi hivyo akizungukwa na mawazo ya vijana sio mbaya, kwani vijana nao wanajifunza kwa huyu mtu mzima. Unataka kusema wananchi wa Burundi walaumiwe kwa Nkurunzinza kupindua katiba? kwa nini wananchi walaumiwe?
 
1.Ndugu sipingi Rais kuwa na miaka 60 ila napinga kumzuia rais kuanzia miaka 40,siamini kama ujana kuwa ndio sababu ya mtu kutaka kubadili katiba kuendelea kutawala,ni hulka ya mtu tu katika kuheshimu katiba,hata akiwa na miaka 70 kama atataka aendelee kutawala atabadili tu.
2.Umeuliza kwa nini wananchi walaumiwe?
Jibu: Uliona kilichotokea Burkina Faso?-Ndio sababu nasema wananchi walaumiwe wakikubali mtu kujiongezea muda,Wabukinabe hawakukubali na iliwezekana.Ukweli ambao kila nikiufikiria huwa unaniuma ni kuwa Watanzania tuwaoga sana sidhani kama tunaweza kuthubutu kufanya walichofanya wananchi wa Burkina Faso.
 
Unapointi. Ila ukweli rais mzee anafanya bora liende as has nothing to lose. Pili life span inasema miaka 47 kwa 52, sasa wewe hiyo 60 unaitoa wapi, au unaangalia maisha ya mtu mmoja mmoja unafanya maamuzi ya jumla?
 
Kwa hiyo ndo tunakubaliana kuwa Dkt. Bilali anafaa kupema Urais (2015-2025)?
 
1.Ndugu sipingi Rais kuwa na miaka 60 ila napinga kumzuia rais kuanzia miaka 40,siamini kama ujana kuwa ndio sababu ya mtu kutaka kubadili katiba kuendelea kutawala,ni hulka ya mtu tu katika kuheshimu katiba,hata akiwa na miaka 70 kama atataka aendelee kutawala atabadili tu.
2.Umeuliza kwa nini wananchi walaumiwe?
Jibu: Uliona kilichotokea Burkina Faso?-Ndio sababu nasema wananchi walaumiwe wakikubali mtu kujiongezea muda,Wabukinabe hawakukubali na iliwezekana.Ukweli ambao kila nikiufikiria huwa unaniuma ni kuwa Watanzania tuwaoga sana sidhani kama tunaweza kuthubutu kufanya walichofanya wananchi wa Burkina Faso.

bado nauliza. warundi si wa kupigiwa mfano? mfano makamba kawa rais oktoba. hope ana 41or 42. akimaliza term zake mbili ana 52. around age ya nkurunzinza. unsdhami makamba atajishughulisha tena na nini baada ya urais? we are creating dormant intellectuals
 
Unapointi. Ila ukweli rais mzee anafanya bora liende as has nothing to lose. Pili life span inasema miaka 47 kwa 52, sasa wewe hiyo 60 unaitoa wapi, au unaangalia maisha ya mtu mmoja mmoja unafanya maamuzi ya jumla?

we ndio unaangalia maisha ya jumla na kufanya maamuzi ya mtu mmoja mmoja. ina maana kuwa idadi ya wanaofariki wakufikisha miaka 50 ni kubwa kuliko wanaovuka? na kwa nini tuamini hizo hoja?
 
Back
Top Bottom