Urais 2015: UKAWA waanza safari

Urais 2015: UKAWA waanza safari

Kitu ambacho CCM hawataki kitokee ni kuona Dr.Slaa anasimama kama mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA.

Mtahangaika sana mwaka huu. Lipumba anachukua jimbo huko kusini, Mbatia anachukua Vunjo.

Imeshapangwa, dua zenu zimefeli.
 
Last edited by a moderator:
Kitu ambacho CCM hawataki kitokee ni kuona Dr.Slaa anasimama kama mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA.

Mtahangaika sana mwaka huu. Lipumba anachukua jimbo huko kusini, Mbatia anachukua Vunjo.

Imeshapangwa, dua zenu zimefeli.
Mleta mada anapendekeza LIPUMBA , haya ya SLAA na CCM yanatoka wapi?
 
Hila na mbinu chafu za ukoo wa panya zimeshang'amuliwa ni kwa sasa kuwagonasha wana wa UKAWA hamtaweza ng'o kuivunja ukawa kwa mbinu nyepesi namna hii/LOWASSA FOR PRESIDENCY 2015
 
Wanaopandikiza udini kwa wananchi ni viongozi wa vyama vya kisiasa kwa manufaa yao wenyewe kama mtoa hoja ana vyojaribu kuwashawishi UKAWA wamsimamishe mgombea kulingana na dini yake na siyo kwa kukubalika kwake na kwa uwezo wake Kama UKAWA walivyokubaliana.

Waanzilishi wa kuwatenganisha wananchi kwa dini zao ni CCM ndio walionza kusema kuwa vyama vya upinzani ni vya kidini.

Lakini ukija mitaani kwa mwananchi mmoja mmoja mambo ya udini huyasikii zaidi ya kuyasikia kwa viongozi wa kisiasa,wananchi wanaishi kwa kupendana bila kujali dini ya mtu.
 
CCM kwanini mnahangaika?CCM wanamwogopa sana Dr.Slaa
 
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU; LIPUMBA ATAIFAA UKAWA KULIKO SLAA.

Wakuu,
leo naanza siku kwa tafakari muhimu hasa juu ya utata naojitokeza hasa juu ya mgombea gani upinzani anapaswa kupeperusha bendera ya UKAWA. Binafsi siamini kabisa kuwa ukawa wataingia uchaguzi mkuu wakiwa pamoja. uchambuzi huu ni kwa manufaa ya wale wanaoamini hilo. chadema na cuf tayari wamekinzana vya kutosha juu ya swala hili japo mengi hayajulikani hadharani lakini inaonekana kuna ubishani mkali sana juu ya nani hasa kati ya hawa gwiji wa siasa za tanzania.
tatizo la kwanza litakuwa nani kati yao ama chao kina wafuasi wengi. ni vigumu sana kutumia kigezo hiki maana leo siyo juzi katika siasa. isitoshe kila chama chaweza kufoji wachama ili kipitishe mgombea wake. kwa hiyo kuna mtihani mgumu kwelikweli kwa ukawa. tujuavyo wanachadema hawaiamini kabisa cuf na hii imetokana na wafuasi wa chadema kulishwa kasumba hiyo na viongozi wao. lakini wana chadema wanaweza kumpigia lipumba cuf ikiwa atakuwa mgombea wa ukawa, wakati wana cuf hawawezi kumpigia kura slaa ikiwa atapitishwa na ukawa. kwa wana cuf wengi ni afadhali kuchagua ccm kuliko mtu kutoka chadema na hasa mtu wanayemuona kuwa ni padiri. pia wana cuf hawafuati kila wanachoambiwa na viongozi wao kama ilivyo kwwana chadema. na kwao porofesa lipumba ameshakuwa kama dogma ambayo huwezi kuitoa vichwani mwao.
sasa kwa mazingira yalivyo nje ya upinzani, ccm inaonekana watasimamisha mgombea urais ambaye ni mkristo. vyovyote vile udini utatumika kwenye uchaguzi wa mwaka huu japo kwa unafiki wetu tunajifanya jambo hilo halipo. uchaguzi mitaa uliopita tayari wakristo walikuwa na kauli mbiu ya chini kwa chini ya chagua mkristo popote pale hata kama hana vigezo vya uongozi. na wamefanya hivyo. ndiyo kusema wakristo wa chadema wanaweza baadhi yao wengi kutosha wakapiga kura ccm kwa kuvutwa na dini ya mgombea lakini pia mawazo kuwa mgombea wa upinzani hatashinda.
wakati huo waislamu wa ccm wengi hawatampigia mgombea wa ccm ambaye ni mkristo. malalamiko juu ya mfumo kirisito hayajaisha, na uchaguzi huu ni sehemu ya kutafuta jibu hasa. ikumbukwe waislamu wa aina ya Rais Kikwete inasemwa na waislamu kuwa ni wakatoliki waliojiita waislamu. kwa hiyo lipumba ambaye amewahi kutamka msikitini kuwa waislamu wachague waislamu ili kupigania maslahi yao ( sijui kama amewahi kukanusha ama kuomba radhi), lama wabebwe na siasa za udini za mwaka huu.
ninachojaribu kusema hapa ni kuwa , waislamu wa ccm wengi watampigia kura lipumba, na cuf wote, then wanachama wengi wa ukawa kwa sababu ya vyama vyao watampigia kura pia. tofauti na mgombea akiwa slaa, wakristo baadhi watapiga kwa kufuata dhehebu. mfano ikiwa mgombea wa ccm atakuwa lowassa, walutheri hata wa upinzani watampatia kura hivyo kura za wapinzani za wakristu kugawanyika na hapohapo waislamu wa cuf na wana cuf wote hawatampigia kura slaa. ikiwa mgombea wa ccm atakuwa membe, kura za wakatoliki zitagawanyika baina ya slaa na membe.
hitimisho langu ni kuwa UKAWA kama utakuwepo na kusimamisha mgombea, basi wamsimamishe lipumba. japo hatashinda urais, lakini atapata kura nyingi zaidi kuliko kama angekuwa dokta slaa.
my submission.

Sheikh Yahya si ameshakufa?mtashangaika sana kuwachonganisha ukawa sindano imeshawachoma subirini dawa taratiibu iwaingie.
 
Mleta mada anapendekeza LIPUMBA , haya ya SLAA na CCM yanatoka wapi?

utata unakuja kwanini pro ccm ndio wapiga zumari kwenye mada hii?? Ni lini ccm mmekuwa wapiga debe wa wagombea wa upinzani?....................?????????????????????????? Sielewi????....????
 
mwandishi bila kujitambulisha anaonekana ni muislam alosheheneshwa udini na kutojiamini.kaul kuwa lipumba alitamka misikitini kuwa waislam wachague waislam wenzao naomba uto uthibitisho hapa alitoa msikiti gani na tar.ngapi kuhusu wakristo kuwa waliaswa na viongozi wao kwenye chaguzi ndogo kuwapigia kura wakristo wenzao hata kama hawana sifa hizi nazo ni porojo tu pia kusema kuwa ccm lazima wamsimamishe mkristo huku pia ni kuweweseka!ulosema cha kweli na nakiunga mkono ni kuwa waislamu kweli tunaamini kuwa waislam sampuli ya kikwete,muft simba,kina al,hadi mussa salumu ni wakatoliki tena watiifu kwa sheria na taratibu za kanisa
 
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU; LIPUMBA ATAIFAA UKAWA KULIKO SLAA.

Wakuu,
leo naanza siku kwa tafakari muhimu hasa juu ya utata naojitokeza hasa juu ya mgombea gani upinzani anapaswa kupeperusha bendera ya UKAWA. Binafsi siamini kabisa kuwa ukawa wataingia uchaguzi mkuu wakiwa pamoja. uchambuzi huu ni kwa manufaa ya wale wanaoamini hilo. chadema na cuf tayari wamekinzana vya kutosha juu ya swala hili japo mengi hayajulikani hadharani lakini inaonekana kuna ubishani mkali sana juu ya nani hasa kati ya hawa gwiji wa siasa za tanzania.
tatizo la kwanza litakuwa nani kati yao ama chao kina wafuasi wengi. ni vigumu sana kutumia kigezo hiki maana leo siyo juzi katika siasa. isitoshe kila chama chaweza kufoji wachama ili kipitishe mgombea wake. kwa hiyo kuna mtihani mgumu kwelikweli kwa ukawa. tujuavyo wanachadema hawaiamini kabisa cuf na hii imetokana na wafuasi wa chadema kulishwa kasumba hiyo na viongozi wao. lakini wana chadema wanaweza kumpigia lipumba cuf ikiwa atakuwa mgombea wa ukawa, wakati wana cuf hawawezi kumpigia kura slaa ikiwa atapitishwa na ukawa. kwa wana cuf wengi ni afadhali kuchagua ccm kuliko mtu kutoka chadema na hasa mtu wanayemuona kuwa ni padiri. pia wana cuf hawafuati kila wanachoambiwa na viongozi wao kama ilivyo kwwana chadema. na kwao porofesa lipumba ameshakuwa kama dogma ambayo huwezi kuitoa vichwani mwao.
sasa kwa mazingira yalivyo nje ya upinzani, ccm inaonekana watasimamisha mgombea urais ambaye ni mkristo. vyovyote vile udini utatumika kwenye uchaguzi wa mwaka huu japo kwa unafiki wetu tunajifanya jambo hilo halipo. uchaguzi mitaa uliopita tayari wakristo walikuwa na kauli mbiu ya chini kwa chini ya chagua mkristo popote pale hata kama hana vigezo vya uongozi. na wamefanya hivyo. ndiyo kusema wakristo wa chadema wanaweza baadhi yao wengi kutosha wakapiga kura ccm kwa kuvutwa na dini ya mgombea lakini pia mawazo kuwa mgombea wa upinzani hatashinda.
wakati huo waislamu wa ccm wengi hawatampigia mgombea wa ccm ambaye ni mkristo. malalamiko juu ya mfumo kirisito hayajaisha, na uchaguzi huu ni sehemu ya kutafuta jibu hasa. ikumbukwe waislamu wa aina ya Rais Kikwete inasemwa na waislamu kuwa ni wakatoliki waliojiita waislamu. kwa hiyo lipumba ambaye amewahi kutamka msikitini kuwa waislamu wachague waislamu ili kupigania maslahi yao ( sijui kama amewahi kukanusha ama kuomba radhi), lama wabebwe na siasa za udini za mwaka huu.
ninachojaribu kusema hapa ni kuwa , waislamu wa ccm wengi watampigia kura lipumba, na cuf wote, then wanachama wengi wa ukawa kwa sababu ya vyama vyao watampigia kura pia. tofauti na mgombea akiwa slaa, wakristo baadhi watapiga kwa kufuata dhehebu. mfano ikiwa mgombea wa ccm atakuwa lowassa, walutheri hata wa upinzani watampatia kura hivyo kura za wapinzani za wakristu kugawanyika na hapohapo waislamu wa cuf na wana cuf wote hawatampigia kura slaa. ikiwa mgombea wa ccm atakuwa membe, kura za wakatoliki zitagawanyika baina ya slaa na membe.
hitimisho langu ni kuwa UKAWA kama utakuwepo na kusimamisha mgombea, basi wamsimamishe lipumba. japo hatashinda urais, lakini atapata kura nyingi zaidi kuliko kama angekuwa dokta slaa.
my submission.
acha propagana za kijinga,umetumwa na magamba!
 
Mtoa mada kaonyesha kana kwamba watanzania walio wengi wanachagua wagombea kwa kufuata dini zao jambo ambali halina ukweli saana! Tukiendekeza jambo hili litavuruga taifa letu! Watanzania wanachagua kiongozi kwa kufuata sera zake na si dini.
 
Ili mpite kirahisi iiiii.... Endeleeni kuota haki yenu
 
Back
Top Bottom