Urafiki wa Afrika na China hauna maslahi kwa Wananchi. Una maslahi kwa watawala Madikteta

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
Popote pale China ilipo inaweka mazingira mazuri kwa ajili ya watu wake. Hivyo hujitahidi sana kukamata Serikali iliyopo Madarakani kwa kui support kwa hali na mali ili Serikali hiyo iendelee kuwanyonya wananchi na China ifaidike kwa maslahi ya nchi yake.

China ya sasa siyo China ya Ujamaa. Hii ni China ya Utamaa. Inayoangalia namna ya kujitanua zaidi kiuchumi. Angalia mikataba ya ki Chief Mangungo wa Msovero ambayo China imeingia na mataifa mengi ya kiafrika. Nenda kafuatilie kinachowapata Zambia sasa.

Waulize Kenya. Kaulize mkataba ambao ilikuwa tuingie kuhusiana na Bandari ya Bagamoyo. Ni Mkataba wa kihuni kupata kuwekwa na hili sina budi kumpongeza Magufuli.

Lakini kuna madudu mengi ambayo bado China inayafanya kwa nchi zetu za Kiafrika.

Mi sijui.
 
Kweli tupu.

Wachina wanasaidia wale watawala madikteta, ili waendelee kupewa Nafasi za kuwafilisi Waafrika.
 
Ujanja mwingine wa moderators ni kuhamisha uzi jukwaa ambalo lina watu wengi na kwenda ficha jukwaa ambalo limepoa. Huu uzi ulitumwa jukwaa la Siasa. Wameupeleka International Forum wakati uzi ni wa tanzania na Kiswahili, ila wameogopa serikali itaudhika.
 
Ujanja mwingine wa moderators ni kuhamisha uzi jukwaa ambalo lina watu wengi na kwenda ficha jukwaa ambalo limepoa. Huu uzi ulitumwa jukwaa la Siasa. Wameupeleka International Forum wakati uzi ni wa Tanzania na Kiswahili, ila wameogopa serikali itaudhika.
 
Wachina ni wamekuwa zaidi ya mabeberu wa kale wa kizungu. Wakati mabeberu wa magharibi wanachota tu rasilimali zetu hawa Wachina wametugeuza dampo la bidhaa zao hafifu na kufifisha kabisa ndoto za kuwa na uchumi imara wa viwanda barani Africa.
Ukitaka kujua asili na tabia za china. Angalia movie ya Jumong
 
Wachina ni wamekuwa zaidi ya mabeberu wa kale wa kizungu. Wakati mabeberu wa magharibi wanachota tu rasilimali zetu hawa Wachina wametugeuza dampo la bidhaa zao hafifu na kufifisha kabisa ndoto za kuwa na uchumi imara wa viwanda barani Africa.
Utakuta kuna Chama kinawapigia chapuo mpaka kusema wataweka rehani madini yetu. Hovyo kabisa.
 
Usichokijua baadh walishalipwa fidia ya maeneo yatakayotumika na huo mrad huko Bagamoyo
 
Kweli kabisa wanakera sana
Ujanja mwingine wa moderators ni kuhamisha uzi jukwaa ambalo lina watu wengi na kwenda ficha jukwaa ambalo limepoa. Huu uzi ulitumwa jukwaa la Siasa. Wameupeleka International Forum wakati uzi ni wa tanzania na Kiswahili, ila wameogopa serikali itaudhika.
 
Chinese are the worst of all colonisers and to make it worse, the racists too.
 
Waulize Zambia, ndio wanajua urafiki wa China upo vipi.

Wahoji hao ungrateful Zambians, Wachina waliwajenga reli ya Tazara kwa mabillion US Dollars, wakajengewa very modern Worshops pale Mpika Zambia vile vile na Depots za locomotive na rolling stock pale Kapiri Mposhi na kuifanya Zambia ionekañe ya kileo - - wote huo ulikuwa ni mpoko wa walipa kodi wa China, sasa Wazambia/Serikali iseme kama imewahi kulipa hata senti tano ya mkopo wa Wachina.
 
Back
Top Bottom