Ally Kombo
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 11,429
- 2,645
Mimi swali langu ni moja ni moja tu, nimeelewa kiasi umuhimu wa mahakama ya kadhi:
kama mtu aliwahi kuwa muislamu, atafanya vipi kama hataki kuhukumiwa na hio sheria, mfano ameamua kuacha dini hio na kubadili dini au kuwa mpagani.
Je familia zenye mchanganyiko wa dini mojawapo ikiwa ya kiislamu, zinahusishwa vipi na hii mahakama
A kama ninaa mzazi mmoja muislamu, mwingine mpagani, ninahusika na hii mahakama?
Yani kwa maneno mengine nauliza hii mahakama inachaguaje watu wa kupokea kesi zao? je hata ndugu, marafiki, maadui wanaweza kuamua kunishtaki katika hii mahakama simply tu kwa kuwa nilishawahi kuwa na historia ya kiislamu? Yani mahakama itafanyaje kazi katika nchi hii ambako tumejichanganya na wengi tumeacha dini zetu?
.........ulipata wapi maelezo kuwa Mahakama hiyo itawashurutisha watu !
Tukisema kuwa 'Mahakama ya kadhi' ni ibada hamuelewi !.............hivi kuna Waislaam wangapi wa kuzaliwa Baba na Mama, Bibi na Babu lakinini hawafanyi 'ibada ya kuswali' !?
Halazimishwi mtu yeyote kujihusisha na Mahakama hiyo kama hataki 'ibada' hiyo kama mtu mwingine anavyokwepa ibada ya kuswali.
Kiislaam ndoa inayotambulika ni ya Muislaam kwa Muislaam mwenziwe, na imefungwa kwa taratibu za Kiislaam.
Muislaam anayesema kaoa asiye Muislaam huyo ni mzinifu period !
Uislaam hauhangaiki (katika taratibu zake) na asiye Muislaam ! Haika
Last edited by a moderator: