Upotoshwaji Kuhusu ya Mahakama za Kadhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upotoshwaji Kuhusu ya Mahakama za Kadhi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Buchanan, Dec 28, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  1. Zimekuwa zikitolewa kauli mara kwa mara kwamba kuna watu wasiowatakia mema waislamu kiasi kwamba hawataki wawe na Mahakama za Kadhi ambazo ni sehemu ya Ibada zao! Kauli hizo zimekuwa zikipotosha ukweli ama kwa makusudi au kwa kutokujua juu ya jambo hilo.
  2. Mara kwa mara linapotokea suala la Kadhi utasikia suala la Ubalozi wa Vatican likijitokeza kama vile Ubalozi huo unagharimiwa na Serikali ya Tanzania. Hata hivyo suala la Balozi nyingine ambazo nchi zao au Serikali zao ni za Kidini halizungumzwi kabisa, it is a one sided story!
  3. Suala kubwa toka kwa watu wasio Waislamu ni kwamba Mahakama hizo ziruhusiwe, kwa kuwa ni haki kwa Waislamu kuwa nazo, hata hivyo sijui kama wameangalia kwa marefu na mapana juu ya mahakama hizo!
  (a) Tumesikia kwamba Mahakama za Kadhi zitahusu Ndoa, Talaka na Mirathi tu. Ukiangalia kwa haraka haraka ni kama vitu vyenyewe si vizito sana kuingizwa kwenye Sheria zetu za kawaida na kushughulikiwa na Majaji wetu kama zilivyoingizwa Sheria nyinginezo. Hata hivyo katika kuonesha kwamba hii ni sehemu ya Ibada ya Kiislamu hawataki suala hili kushughulikiwa na watu wasiokuwa Waislamu! Kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba waislamu wanataka kufanya mambo yao bila kuingiliwa na Serikali.
  (b) Hata hivyo, inavyoonekana mambo sivyo yalivyo. Ukiangalia Mahakama za Kadhi kwa Zanzibar, Chief Kadhi huteuliwa na Rais wa Zanzibar. Kwa Zanzibar sina neno sana kwa kuwa 99% ya Wazanzibari ni Waislamu, kwa hiyo probability ya kuwa na Rais mwislamu ni kubwa. Hata hivyo akitokea Rais ambaye ni Mkristo itabidi amteue huyo CK bila kupenda!
  (c) Kwa upande wa uendeshaji wa Mahakama hizo kwa upande wa gharama, Waislamu wanataka Serikali ndiyo igharamie Mahakama hizo! Hapo ndio matatizo yanapoanzia! Kama nilivyosema kwamba Mambo ya Mahakama za Kadhi ni Ibada ya Waislamu. Ibara ya 19 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inasema kwamba "Kazi ya kutangaza dini, kufanya Ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi." Kwa hiyo Serikali itakapotia mguu kugharamia Mahakama za Kadhi itakuwa imejiingiza kutangaza dini ya Kiislamu ambapo itakuwa ni kuvunja Katiba!
  (d) Pamoja na kwamba Mahakama za Kadhi zitajihusisha na ndoa kama nilivyosema hapo mwanzo, suala la ndoa ni pana. Ndio maana tumeona kwamba kuna Sheria za Kiislamu za KUPIGA WATU MAWE hadi kufa kwa kosa la uzinzi! Yapo pia makosa ambayo yanasema kwamba ni kosa kwa wanaume kuchanganyika na wanawake (haya yapo kwenye nchi za kiislamu, lakini msingi wake ndio huo). Suala la kujiuliza ni kwamba kama Mahakama za Kadhi zinaweza kuachiwa BAADHI YA MAMBO tu na mengine kushughulikiwa na Serikali (eg adhabu za kupiga mawe zisiwepo), Je, Mahakama hizo kwa nini ziwepo? Wasio Waislamu wanaona kwamba haya mambo ya Mahakama ya Kadhi ni NJIA YA KUISILIMISHA nchi baadaye!

  4. Wasio Waislamu wanachotaka ni kwamba Waislamu waachiwe mambo yao wenyewe na Serikali isijiingize kwa namna yoyote ile katika kumteua Kadhi Mkuu (KM) au kuyagharamia!
  5. Nchi za Nigeria, Somalia, Sudan na nyinginezo zimeingia katika migogoro ya kidini na hata kufikiria kuzigawanya baadhi ya nchi hizo ili Wakristo wakae peke yao, pia Waislamu wawe hivyo hivyo peke yao. Mauaji yasiyokoma, uchomaji Misikiti na Makanisa umetokea ili mradi tu kuonesha hasira walizonazo baadhi ya watu wa dini moja dhidi ya dini nyingine.
  6. Zipo hoja ambazo zimetolewa kwamba baadhi ya nchi zina Mahakama za Kadhi lakini hakuna fujo za aina yoyote! Kwa mwenye macho ya kutazama na masikio ya kusikia hawezi kubishana na mimi kwamba kama Serikali itaamua kuibeba dini moja kwa maslahi ya dini hiyo tunao mgogoro mkubwa wa kidini katika siku za mbeleni, kwa sababu dalili zote zipo. Kila iitwapo leo amani ya nchi yetu inazidi kutoweka taratibu! Tutazame nchi yetu mambo yanavyokwenda badala ya ku-copy n' paste mambo ya nchi nyingine! Tukilazimisha mambo tutakuja kulia siku moja na hakuna pa kukimbilia maana kwa majirani zetu si wakarimu kama sisi, wanachukia mno wageni!
  7. Amani yetu ni kama barafu, tusiiruhusu ikaanza kupigwa na jua itaanza kuyeyuka taratibu na mwisho wa siku tutakuwa na maji ya moto badala ya barafu!
  8. Wasio Waislamu wanawatakia mema Waislamu, ndio maana wanataka Waislamu washughulikie mambo yao ya kiibada bila kuingiliwa na Serikali kiuendeshaji au kwa gharama kwa manufaa yao na bila kuvunja Sheria za Nchi, ikiwemo Sheria mama, Katiba!


  Naomba kuwasilisha, kwa mjadala zaidi, kama upo!
   
 2. m

  maarufu Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha udini wewe
   
 3. T

  Topical JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wewe na udini utakufa mkuu...dini inapeta tu..wala haijali wewe umechukia kiasi gani..
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hakuna mwenye chuki, hizi dini zipete kama unavyodai lakini tujifunze jinsi Nigeria, Somalia, nk walipofika ili tuepuke kufika huko ikiwa bado tungali na nafasi!
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Nigeria na Somalia wanapigana kwa sababu ya mahakama ya kadhi?
  Au Vyanzo vya mapigano yao ni nini?

  Umesema watu wanapotosha mambo, hapa wewe unafanya nini?

  Au umesahau tu sababu za mapigano yao?

  Anyway, Tanzania iko on the right track kuelekea huko tusikokutaka lakini sababu kubwa itakuwa ni kwa wananchi kuchoshwa na ufukara na umasikini, sauti zao kupitia kura zinapokanyagwa, ufumbiaji macho wa wala rushwa wakubwa na ufisadi wa kutisha wa rasilimali za taifa. na kukosekana a level playing field kwa vyama vya siasa.

  Siku ukondoo wa umma ukiondoka basi vurumai zitaingia kwenye "kisiwa cha amani na utulivu"
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwani mbuyu ulianza kuwa mkubwa kama unavyoonekana hapa chini? Mimi sipotoshi ila natahadharisha kwamba mambo yanavyokwenda tutakuja kulia!

  [​IMG]
   
 7. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,306
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Mkuu upo sahihi sana. Hawajui wafanyalo. Mimi ninaona ni kama aina ya kiubaguzi fulani. Na kama wanasema ni moja ya ibada za dini ya kiislam kuna haja gani ya kuhusisha serikali ili hali serikali yetu haifungamani na dini yoyote? Huko nigeria isijeonekana walianza tofauti sana na sisi. Tumshukuru mwl kwa kuliona mapema na kulifanya liwe lilivyo. Dini na serikali viwe tofauti. Kwani mbona wakristu wakikorofishana mume na mke huenda kwa padre au askofu? Kwa nini kadhi asiwepo but awe chini ya bakwata na si serikali? Kuna kitu kingine naona kinatafutwa underground ambacho hatukijui. Ningeomba watz tusicheze na hii amani iliyopo. Tukumbuke kuna watu wameoa waislam na wengine wakristu na kuolewa the same. Itakuwaje kama watakuwa wameanza kubaguliwa? Kama kuna mtu alieona sinema iitwayo sometimes in april au picha yoyote ile ya mauaji ya rwanda angejumbuka watusi walooa wahutu au the opp walivyoteseka. Kupewa panga umuue mwanao au mkeo ni kitu kigumu jamani. Na kama viongozh wetu wa serikali wanakujaga jf walifanzie kazi hili kwa haraka na bila kumuangalia mtu usoni. Hatufiki 2050 salama.
   
 8. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Hawa jamaa janja sana! Wanakupa mkono, ukiwapa, wanashika bega! Mwanzoni kabisa walianza na Mahakama ya Kadhi. Siku hazijaenda mbali wameshaongeza pia Mwaka Mpya wa Kiislamu ili uwe publis holiday. Wataenda taratibutaratibu... na hatimaye kuanza kukama watu mikono na kuwapiga mawe hadi kufa maana kwao si tatizo kufanya hivyo bali ndiyo kuishi dini yao.
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mimi sina imani na JK ambaye inaonekana alichokikimbilia Ikulu ni maslahi ya watu wa dini yake tu, as simple as that! He is surely, short sighted!
   
 10. Y

  Yusuph Salehe Member

  #10
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha unafiki unauhakika kuwa JK anahucka kwa lolote kuhusu mahakama ya kadhi? Ongea na facts
   
 11. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2011
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Udini ndani ya jf acheni hizo leteni hoja zisizo za kidini heee!
   
 12. CPU

  CPU JF Gold Member

  #12
  Jan 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nimefikiria kwa kina sana kuhusu hiyo Kadhi. Achilia mbali kugharamiwa na Serikali, inaweza ikasambaratisha waislamu wenyewe kwa wenyewe badala ya kuwaweka pamoja. Na isitoshe inaweza kusababisha ndoa nyingi za waislamu na wakristo zikavunjika.
  Na hii inaweza kuwafanya hata kwa baadhi ya walio waislamu kwa sasa wakakimbia dini yao wakiona hiyo mahakama inawanyima uhuru wa baadhi ya vitu walivyokuwa wanafanya hapo awali bila bughudha.

  Kwa kuhitimisha ni kwamba hii Mahakama inafaa kwa nchi ambazo wakazi wake wengi ni Waislamu, ndo itafanya kazi vizuri. Lakin kwa hapa Bongo, mtu akichoshwa na masharti ya Kadhi, ana hamia Ukristo, anaendelea kupata uhuru wake wa awali
   
 13. s

  shadhuly Senior Member

  #13
  Jan 16, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  mtoa mada tumekusoma.katika hilo la kupingana na katiba nadhani hata hii memorundum of understanding kati ya kanisa na serikali ambapo kodi za wananchi zinachotwa pale hazina na kupewa nalo ni tatizo.so kwanini msiivumilie katika hilo kama wanavyovumilia waisilamu.
   
 14. CPU

  CPU JF Gold Member

  #14
  Jan 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nadhani hii inahitaji maelezo zaidi
   
 15. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #15
  Jan 16, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Afrik kusini kuna mahakama ya kadhi, kuna madhara yoyote yameripotiwa kutokea. Tanganyika orderin council iliruhusu mahakama ya kadhi. Independence Constitution na Republi, zote ziliruhusu niambie wapi madhara ya mahakama ya kadhi yaliripotiwa? Thanks Buchanan kwa kuanzisha mada
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Jan 16, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hata Nigeria nako zilipoanzishwa kulikuwa na amani! Historia inaonyesha kuwa waislamu wakiwa wachache hawana vurugu, wakiongezeka wanaanza kulalamika wanaonewa, wakiwa wengi ndio balaa zinapoanza! RSA is not an exception!
   
 17. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #17
  Sep 30, 2014
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ...........kumbe wewe jamaa ni mpuuzi hivi ! Buchanan. Kwa hiyo Somalia na Nigeria ni kisa "Mahakama ya Kadhi !?" Mbona wewe hujajifunza Hiroshima na Nagasaki au Palestine wanavyodhulumiwa !?
   
 18. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #18
  Sep 30, 2014
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ...........sikutegemea kuwa ni mjinga kiasi hiki !:peep:
   
 19. H

  Haika JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2014
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mimi swali langu ni moja ni moja tu, nimeelewa kiasi umuhimu wa mahakama ya kadhi:
  kama mtu aliwahi kuwa muislamu, atafanya vipi kama hataki kuhukumiwa na hio sheria, mfano ameamua kuacha dini hio na kubadili dini au kuwa mpagani.
  Je familia zenye mchanganyiko wa dini mojawapo ikiwa ya kiislamu, zinahusishwa vipi na hii mahakama

  A kama ninaa mzazi mmoja muislamu, mwingine mpagani, ninahusika na hii mahakama?
  Yani kwa maneno mengine nauliza hii mahakama inachaguaje watu wa kupokea kesi zao? je hata ndugu, marafiki, maadui wanaweza kuamua kunishtaki katika hii mahakama simply tu kwa kuwa nilishawahi kuwa na historia ya kiislamu? Yani mahakama itafanyaje kazi katika nchi hii ambako tumejichanganya na wengi tumeacha dini zetu?
   
 20. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #20
  Sep 30, 2014
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  .........wewe unaona kiasi cha urefu wa pua yako !
   
Loading...