Hawamcheki ila wanajaribu kuiandika upya historia ya Tanzania. Hawawezi. Sasa hivi ukijaribu kumgusa fisadi yeyote kwa kumpeleka mahakamani, Mkapa lazima atajwe, tena awe shahidi. Kikwete naye atakapostaafu ukimsimamisha waziri yeyote kwenye awamu yake naye ataitwa kuwa shahidi. Ndivyo wanavyoitafuna nchi hii kwa ushirikiano wa hali ya juu.
Hivi nyie mnakumbuka jinsi Usalama wa Taifa ilivyokuwa inaogopwa wakati wa Nyerere? Kwani kuna binadam gani asiye na kasoro? Kuna watu wengi sana WALIPOTEZWA/WALITOWEKA wakati wa Nyerere na hakuna aliyethubutu kusema kitu! Msiuogope ukweli kwani Historia ndiyo inayohukumu. Tenda utendalo, litaandikwa tu!
Ndio maana halisi ya kuwa kigogo siku hizi....kula na kutapanya halafu kulindana kwa gharama yoyote ile. Wengine wote tunaonekana hatujui tunalofanya mbele ya wajanja hawa wachache wenye hadhi ya kuwa vigogo. Kazi ipo.....
Chifu Fundikira alikuwa mwakilishi wetu kwenye East African community 1963. Alichukua kazi hiyo baada ya kupoteza uwaziri katika kesi ya kwanza Tanganyika ya kupokea rushwa.......
Hivi nyie mnakumbuka jinsi Usalama wa Taifa ilivyokuwa inaogopwa wakati wa Nyerere? Kwani kuna binadam gani asiye na kasoro? Kuna watu wengi sana WALIPOTEZWA/WALITOWEKA wakati wa Nyerere na hakuna aliyethubutu kusema kitu! Msiuogope ukweli kwani Historia ndiyo inayohukumu. Tenda utendalo, litaandikwa tu!
KVM,Thank you Sir, I agree. Nimekisoma kitabu hiki: Julius Nyerere and the Establishment of Sovereignty in Tanganyika by Paul K. Bjerk kinaelezea kwa undani sana habari za Christopher Kassanga Tumbo na mapambano ya Nyerere na Trade unions, racism (watu waliwakataa akina Jama na Bryceson kuwa kwenye TANU), nk. Unaweza kukipata kwenye eBook Julius Nyerere and the Establishment of Sovereignty in Tanganyika - Paul K. Bjerk - Google Books
Wawataje angalau watu wawili waliopotezwa na Nyerere
Wikipedia hii itakua imeandikwa na wale makaburu wa South Africa. Walikua hawampendi Nyerere kwa msimamo wake. Huu wote ni upumbavu. Nyerere alikua dictator ndio, lakini hajawahi kufanya mambo hayo.
Na tukichukua kitu kimoja tu ambapo Nyerere alifanikiwa sana, na hili haliwezi kusutwa na akina Njiwa, Sadeeq, na Zomba, ni kutuunganisha sisi wote na kuthamini Utanzania wetu. Ndugu zetu wa Kenya mpaka yale mauaji ya 2007, walikuwa hawajitambui kuwa ni Wakenya, ila Waluhya, Wajaluo, Wakikuyu, Wakamba, etc. etc. Na ukiangalia Afrika ya miaka 60 na 70, huo si ufanisi wa kubezwa hata kidogo. Alituwekea msingi ambao leo hata m' k were anaweza kukubalika kwa wapiga kura wa Nyegezi bila kutumia siasa za makabila kama ilivyo katika nchi jirani.KVM,
Ahsante sana. Muda mfupi baada ya kupewa Uhuru wetu Mwalimu alipata taabu sana kuwaunganisha WATANGANYIKA:
-Kuna ambao walitaka tuendelee na Majimbo na kwa maana hiyo ukabila/uchifu;
-Kuna ambao walitaka DINI zipewe umuhimu wa aina yake;
-Kuna ambao hawakuwataka Wazungu, Wahindi, kwenye TANU na serikalini;
-Kuna ambao walitaka kuanza kuitafuna NCHI mara moja;
-Kuna ambao walitaka vyama vya SIASA vyenye UDINI ndani yake.
Wote hawa kwa nyakati tofauti waligeuka wakawa maadui wakubwa wa Mwalimu kuliko hata MKOLONI. Chuki hizi ziliendelea hadi lile jaribio la mapinduzi la mwaka 1964 likatokea. Baada ya AZIMIO la ARUSHA na MIIKO ya UONGOZI maadui wa Mwalimu wakaongezeka zaidi. Jaribio la mapinduzi likawepo tena la akina Chipaka, Kambona, Bibi Titi Mohamed,...Majaribio yote haya Mwalimu hakumnyonga mtu. Chuki ziliendelea kuwepo hadi leo kwa wajukuu wengine walioko humu JF. Hawatamsamehe Mwalimu kwa kosa ambalo kimsingi halipo.
Now i know kwanini sera na fikra za Nyerere zinapingwa sana na wale ambao tulifikiri watakuwa watetezi wake kwa sababu ni watetezi wakubwa wa sera za chama alichokianzisha.Wengi sana tu kwa maelfu kama sio malaki, mbona humuhumu JF zimeshaandikwa habari za maovu yake mengi tu:
Soma hapa mfungwa wake mmoja: https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=5657&d=1250867389
Halo umenena. Asante.Na tukichukua kitu kimoja tu ambapo Nyerere alifanikiwa sana, na hili haliwezi kusutwa na akina Njiwa, Sadeeq, na Zomba, ni kutuunganisha sisi wote na kuthamini Utanzania wetu. Ndugu zetu wa Kenya mpaka yale mauaji ya 2007, walikuwa hawajitambui kuwa ni Wakenya, ila Waluhya, Wajaluo, Wakikuyu, Wakamba, etc. etc. Na ukiangalia Afrika ya miaka 60 na 70, huo si ufanisi wa kubezwa hata kidogo. Alituwekea msingi ambao leo hata m' k were anaweza kukubalika kwa wapiga kura wa Nyegezi bila kutumia siasa za makabila kama ilivyo katika nchi jirani.
ukweli unauma.....
Nyelele arikuwa mtu mzuli sana, wakati wa Nyelele aliimalisha sana hari ya watu wake kierimu na rishe bola, vyakura kama mahalage
mchere, sukali, virikuwa vikipatikana kira kona ya Jamhuli ya Tanzania