Aaah, unataka kujua kwa nini Kassim Hanga alirudishwa Zanzibar? Na Ritz kakusifia kuwa hilo swali zuri. Ni kweli Kassim alisetiriwa mainland na Nyerere. Na kabla ya kumkabidhi kwa maafisa wa Karume, Nyerere alimwita Kassim mpumbavu.
Kassim, akiwa mainland, aliendelea kula njama na Kambona kumpindua Nyerere. Hawa wangefanikiwa Kassim angechukua uongozi Zanzibar wakati Kambona akichukua uongozi wa mainland. Hivi ingekuwa wewe, ungeendelea kumpa hifadhi mtu ambaye anafanya mipango ya kuhujumu utawala wako?