Mkuu Jasusi, sijui kama umeligundua kuwa hawa wapenzi na watetezi wa CCM ya sasa ndio wenye chuki kubwa na Mwalimu Nyerere wakati hicho chama wakiteteacho yeye ndio mwanzilishi wake.
Ila ukiangalia kwa darubini kali, CCM hii ya Kikwete sio ile ya Nyerere ila inatumia usajili wa CCM ya Nyerere ambayo ilishakufa pamoja na mwanzilishi wake.
Hii ni kweli kabisa wala haina marekebisho kuna kina Chipaka,Zuberi Mtemvu kina Chifu Mareale kina Fundikira,Abdulrahman Babu,wengine wengi walikimbia nchi kama kina Kambona wengine walifukuzwa jeshini na kuzuiwa nyumbani kama kina Bob Nasser(Nasari).Mahfudhi wengine wakapewa kazi nyingine uraiani lakini kwa masharti kama kina Capt.Mushi huyu mwenye malori mengi mfadhili wa Simba jina simkumbuki alikuwa meneja kampuni ya KAMATA na wengine wengi sana siwakumbuki majina yao,wako waliofia gerezani kwa mateso,lakini hayo hayazungumzwi,hiyo ndiyo taswira ya Mwl.Nyerere kwa upande wa pili,tusipende kuongelea mazuri tu,hata mabaya yapo mengi tena ya kutisha.
Akutukanae hakuchagulii tusi
Mhh! afadhali hawa mafisadi wetu wa sasa hivi wengi wao pesa nyingine wanazibakisha na kuwekeza vitega uchumi hapahapa hivyo pesa inazunguka hapahapa nchini na wananchi wengine wanaambulia kazi katika miradi ya mafisadi, lakini FISADI Nyerere yeye kazi yake alikuwa akichota tu na kuwapelekea Wakristo wenzake nje ya nchi mfano Biafra.
Ushahidi upo. Fuatilia ile kesi ya Bibi Titi Mohammed na ndugu zake Kambona, uone Hanga alikuwa na role gani katika njama zile. Tena bahati nzuri kama ulikuwepo nyakati zile kesi nzima iliandikwa magazetini. Yet still, tafuta kitabu cha Godfrey Mwakikagile. Nyerere hakuwa controversial hata kidogo. Kwa sisi tuliomfahamu, he was very predictable.Mkuu! tunazungumzia watu ambao wako tayari kuuwa raia zao ili kufikia malengo yao achalia mbali "kuvunja" mahusiano ya kibalozi.
Halafu na Nyerere naye kwa nini amkubali "personal assistant" ambaye ni mtumishi wa Serikali ambayo ni "hasimu" yake kama alivyokuwa akidai?...Nyerere was a controversial figure throughout most of his life, if not entirely!
Mkuu una ushahidi wowote? au na wewe umekuwa ni muhanga wa propaganda za Nyerere.
Kwamba Nyerere alikuwa havumilii upinzani hilo tunalikubali. Hao uliowataja wengine walimpinga akawaweka detention, wengine kama akina Chipaka walihukumiwa na mahakama kuwa ni wahaini wakafungwa, na wengine walikuwa wamefanya makosa sehmu zao za kazi akwahamishia kwingine.
Lakini Nyerere hakumuua mtu hata moja. Taja jina la mtu moja tu aliyefia gerezani kwa mateso.
Halafu CK Tumbo amekuwepo hadi mfumo wa vyama vingi unaanza. Hawakuhangaika kumuuliza yaliyomsibu wakati ule. Kuiweka pamoja TANZANIA wakati ule wa Mwalimu haikuwa kazi ndogo kama wanavyoibomoa sasa.
Nyerere alipaishwa jina lake na Waingereza.Jasusi nimecheka sana...watu walimdharau Nyerere akiwa hai wakaishia kwenye kona. Sasa hivi wanamdharau amekufa wanafikiri watamuua tena mara ya pili. Wanalijenga jina lake maana kadri wanavyoshindwa kuonyesha wana uwezo kuliko yeye ndio jina lake linavyopaa juu juu.
Saini yake ndio iliyomnyonga MWAMWINDI!! Je, hapo hakuua? Nionavyo mimi kama kuua ni kutoa uhai wa binadamu kwa kutumia mamlaka yako then hata wale walioliwa na simba wakati wa "villagization" waliuawa na muasisis wa sera ile !!
Ndahani,Hawana uwezo wa kuongoza. Changamoto zilizopo zimewazidi kimo na zinaweka weaknesses zote wazi wazi. Ndio maana tunaona sasa watu wanajitahidi kuleta mada ambazo wanafikiri zitaweza kuziba mapungufu yao kirahisi kama ukabila na udini. Hoja za sasa hivi ziangalie zilivyokaa kaa. Ni kujaribu kuzima maswali yoyote kwenye weakness za wazi wazi za uongozi tulizonazo. Utaachaje kuhangaika na mafisadi na kuhangaika na watu wadogo wadogo wasio na tija wala impact yoyote kwa uwepo na ustawi wetu? Maana ufisadi ndio ule ulioitwa uhujumu uchumi...siku hizi ukiufanya vizuri unaitwa kigogo.
Nilikuwa ninataka kukujibu lakini nimekumbuka maneno ya Bigaraone:Ushahidi upo. Fuatilia ile kesi ya Bibi Titi Mohammed na ndugu zake Kambona, uone Hanga alikuwa na role gani katika njama zile. Tena bahati nzuri kama ulikuwepo nyakati zile kesi nzima iliandikwa magazetini. Yet still, tafuta kitabu cha Godfrey Mwakikagile. Nyerere hakuwa controversial hata kidogo. Kwa sisi tuliomfahamu, he was very predictable.
Wala Nyerere hakutoa hukumu. Alitia sahihi kama Rais wa NCHI ili watu hawa wanyongwe. Hili ni hitaji la kisheria ambalo hata hivo alilikwepa na kuliepuka kwa watu wengi tu. Kuna watu humu wanasutwa na dhamira zao kwa uongo wanaouandika juu ya Mwalimu. Wasubiri baadhi yetu tutoweke hapa duniani.
Ni kweli kuna exaggeration katika maandiko hayo lakini ni kweli pia kulikuwa na repression ya hali ya juu wakati wa nyerere; ndio wakati huo watu wa usalama walikuwa kazi yao kubwa kuhesabu vizibo vya bia watu wanazokunywa bar na kwenda kutoa ripoti halafu makachelo wanaanza kufuatilia nyendo za muhusika; kulikuwa hakuna uhuru wa habari ukilinganisha na leo!! Cartoon anazochorwa MKWEREE sidhani kama zingeweza kuruhusiwa enzi za MCHONGA. Alikuwa ni mzalendo wa kweli lakini pia alikuwa na mapungufu ya kibinadamu, all in all he was a BENEVOLENT DESPOT.
Ndahani,
Umewasikia mashahidi wa Mramba? Yumo Chenge, John Momose Cheyo, Marehemu Balali( kama angekuwa hai), Mkapa( hajathibitisha kama atapanda kizimbani),... Siku hizi ufisadi ni sifa mama ya kugombea UONGOZI kule CCM na serikalini.
Viongozi wa DINI nao wanajiimarisha kwelikweli. Wana nguvu kuliko serikali. Hata sensa ya mwaka huu itafanyika kwa huruma yao.
Swali zuri sana.
Well said. Nyerere alikuwa na mapungufu yake. Uchumi kwa kweli hakuumudu kabisa na alikuwa hapendi upinzani wowote ule wakati wa utawala wake. Hilo aliwahi kulisema mara kadhaa.
But Nyerere was not a dummy. He was very intelligent and eloquent and well-read. Those who say everything was written fro him dont know Nyerere at all. You could read your "Risala" to Nyerere and he would write nothing however long your "Risala" but when he stood up he would deal with all points raised one by one without reading anywhere. That was Nyerere. He could explain complicated things to novices but he could confront any intelligent person in the world. Reporters who were assigned to interview Nyerere knew very well that they had to do they assignment before confronting him. Some of us remember very well how he dealt with the reporters who came with the US Foreign Minister, Henry Kissinger and how he swayed the world opinion on Cuban involvement in the war in Angola.
ukweli unauma.....
Nyelele arikuwa mtu mzuli sana, wakati wa Nyelele aliimalisha sana hari ya watu wake kierimu na rishe bola, vyakura kama mahalage
mchere, sukali, virikuwa vikipatikana kira kona ya Jamhuli ya Tanzania
Hebu check kwenye red unafanya makusudi au ndio uelewa wako wa kiswahili?.....
Chifu Fundikira alikuwa mwakilishi wetu kwenye East African community 1963. Alichukua kazi hiyo baada ya kupoteza uwaziri katika kesi ya kwanza Tanganyika ya kupokea rushwa.Huyo hakuwa Chief Fundikira?
Hawamcheki ila wanajaribu kuiandika upya historia ya Tanzania. Hawawezi. Sasa hivi ukijaribu kumgusa fisadi yeyote kwa kumpeleka mahakamani, Mkapa lazima atajwe, tena awe shahidi. Kikwete naye atakapostaafu ukimsimamisha waziri yeyote kwenye awamu yake naye ataitwa kuwa shahidi. Ndivyo wanavyoitafuna nchi hii kwa ushirikiano wa hali ya juu.Ndio hao vigogo wa CCM wanaomcheka Nyerere. Imekula kwao maana Tanzania itakuwepo hata bila ya mimi na wewe. Wanafikiri yanayoendelea yafafunikwa chini ya kapeti...kumbe ndio itakuwa vigezo vya kuwaweka kwenye mizani siku za baadae.