ulichokiongea ni kweli kwa asilimia zote,
kuna kisa kimoja kiliwah kumtokea
kumtokea mama mkubwa wangu
mnamo mwaka 2008
yeye alikufa kwa mda,
kisha akafufuka na baada ya kufufuka alielezea yaliyomkuta pindi amekufa.
Yeye alifarik dodoma mjini,
na nyumban ni kijijini, hivo uliandaliwa utaratibu wa kusafilisha mwili wa marehemu hadi kufika nyumbn ni mwendo wa masaa mawili
walifika nyumban na mwili wa marehemu,
Walikaa masaa mawili
yule bi mkubwa akaamka watu waliokuwa hapo walishangaa sana na hata wengne kukimbia
yeye bi mkubwa akawaambia naomba maji ya kunywa maana nmechoka sana,
nmetembea kwa mda mlefu na nmetoka mbali sana,
basi wakampatia maji na kisha akawaeleza kisa alichokutana nacho,
nanukuu kama nilivyosikia kutoka kwake
anasema alikuwa anatembea kwa mda mlefu huko alikokuwa alikuwa akipita kwenye milima na mabonde bila kuelewa anaelekea wapi alitembea kwa mda mlefu mwisho alikuta kuna mlango mkubwa wa kuingia basi alibisha hodi na mlango ukafunguliwa
baada ya mlango kufunguliwa aliona ile sehemu ina mwanga mweupe na unaong'aa sana tofauti na wadunian
hakuna jua ila mwanga umetapakaa sehemu yote,
kifupi ni kama wana dunia yao tofaut na sisi,
alipoingia ndani alikutana na ndugu zake wa zamani waliokuwa wamekufa dunian akawakuta kule
anasema kuna watu wengi sana kule
hata hivyo anasema wale watu hawakumpokea maana walikuwa wameinamisha vichwa chini
yeye aliendelea mbele akakuta babu yake mzaa baba ake amekaa kwenye kiti na yule babu yake pia hakumtazama uso ila alikuwa kainamisha kichwa
alipofika yule babu yake akamuuliza
wewe nani?
akajitaja jina
akaulizwa umekuja kufanyaje,
akawaambia nmekuja kama nyinyi mlivyo kuja,
babu akamwambia umekuja kabla ya mda wako chukua haya maji unywe upate nguvu ugeuke uludi ulikotoka
mda wako wa kuja huku ulikuwa bdo haujafika bali kuna mtu alikuroga hivo sisi hatukupokei,
mda wako wa kuja ukifika tutakupokea,
baada ya hapo alianza kurudi alitembea umbali kidogo baada ya kuvuka mlango wa kule
ndo akastuka akiwa kitandani.
na akasimulia kama nilivowaelekeza hapo juu,
Tokea cku hyo nilijifunza mambo meng kupitia hii story ya kweli kabisa
kwamba kuna dunia baada ya kufa
na ukifa unaenda kuungana na ndugu zako waliokutangulia kabla
ambao sisi ndo tunawaita mizimu.
hata hivyo huyo mamkubwa ameshafariki kwa sasa.
lakin aliniachia somo kwamba nijitambue kuwa baada ya kufa kuna maisha,
na maisha yenyewe ni kuungana na ndugu zako waliokutangulia,