Upole unawagharimu wanaume wengi

Upole unawagharimu wanaume wengi

Majaribu2013

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
952
Reaction score
1,050
Nimemhurumia sana jamaa yangu.Ni jamaa ambaye tumekua naye, tumesoma naye ni mpole sana na mcha Mungu sana. Kanisani kwao ni mtu mkubwa tu sijui anacheo gani, lakini ni mtu mkubwa tu.

Huyu mshikaji alioa mwaka jana mwanamke mrembo sana lakini alionekana kama mtukutumtukutu. Mshikaji kamuombea mpaka mwanamke kawa mtu mzuri tu na kanisani naye kapewa cheo fulani hivi ni Kanisa kubwa tu hapa Dar es salam.

Sasa mwanamke amekuwa akitumia sana upole wa mwanaume kumdrive kama anavyopenda. Anaweza kumnunia tu hata wiki nzima, huku mshikaji anachanginyikiwa sana na kukonda mno, hapendi kabisa wagombane na mke wake.Yaani jamaa anavyopelekwa mpaka unamuonea huruma.

Jana nimemwambia dawa ya hawa wanawake watafutie papi, akileta nyoro kale maini. Mbona atanyooka mwenyewe tu bila hata kuchapwa.Hapa mshikaji nimemtafutia msichana na vile mshikaji anapesa demu kakubali, na huyu msichana ni wa ushwahilini mshikaji atakipata cha moto mpaka atasahau mateso.

Wanaume wapole msifikiri ni sifa ni uzombi.
 
mkuu wanawake wengien akikununia ndio anakupenda zaidi.... hivyo jama inabidi amsome mwenzie yukoje kiitikad za mapenzi.
 
Yaaani unafundisha kuwa na nyumba ndogo ndio upole unaisha vipi ? na huyo akianza mapepe ina maana jamaa atakawa na nyumba ndogo ngapi sasa.
 
We unamuongezea mwenzio shida tu. Sasa na huo mchepuko ukianza kumpelekesha itakuwaje? au itabidi aongeze mchepuko mwingine??!!!
 
Akichepuka ndio upole utaisha???!
 
Mchepuko nao ukileta shida unaongeza mwingine
 
Mambo ya Ngoswe, muachie Ngoswe mwenyewe.

Unaweza kumshauri amdhibiti mkewe, kumbe jamaa anapenda kudhibitiwa.
 
Yani jeuri anafanyiwa rafiki yako,lakini roho inakuuma wewe? hivi unahisi umefanya jambo zuri kweli na ndani ya nafsi yako una amani? unakua kuadi kwa jambo lisilo kuhusu?

hukuona njia nyengine yakumsaidia? na kama huyo rafiki yako kakubali huo ushauri wako na yeye pia sie.Usimshauri mwenzio kufanya mabaya huyo mke wa rafiki angekua dadako ungemkuwadia mumewe eeh?
 
Tatizo wewe hujui nini maana ya ndoa ndio maana umemshawishi mwenzio na kumtafutia mwanamke mwingine. Wewe sio rafiki wa manufaa kwake bali ni rafiki maslai. Wewe ungekuwa rafiki yangu ukanipa ushauri wa kipuuzi kama huo nadhani huo ndio utakuwa mwisho wa urafiki yetu.

Hivi mke wake akigundua wewe utamsaidiaje, hivi wewe unaishi nao ndani au una lala nao kitandani kujua hasa ya moyoni mwao? Nyinyi ndio mnaokatisha tamaa ya watu wanaotaka kuingia kwenye ndoa kwa kutoa mitazamo hasi
 
bora umemwambia maana mm ningemshushia kombora la aina yake angesahau kuingia tena humu ndani sijui nimshushie hilo kombora au sijui nimwache tu yaani amenikerajee?
Tatizo wewe hujui nini maana ya ndoa ndio maana umemshawishi mwenzio na kumtafutia mwanamke mwingine. Wewe sio rafiki wa manufaa kwake bali ni rafiki maslai. Wewe ungekuwa rafiki yangu ukanipa ushauri wa kipuuzi kama huo nadhani huo ndio utakuwa mwisho wa urafiki yetu. Hivi mke wake akigundua wewe utamsaidiaje, hivi wewe unaishi nao ndani au una lala nao kitandani kujua hasa ya moyoni mwao? Nyinyi ndio mnaokatisha tamaa ya watu wanaotaka kuingia kwenye ndoa kwa kutoa mitazamo hasi
 
Mkuu Majaribu2013 muwahi kabla hajafanya ile kitu,huyo jamaa na huo upole unauelezea atahamia jumla.
 
Last edited by a moderator:
sio vizuri jamani, umesema rafiki yako mcha Mungu halafu unamfundisha kuchepuka!looh! marafiki hawa wa kuangalia sana. mwambie aombe tena kama alivyomwobea akaacha utukutu, hataacha tu na hiyo tabia.

kama michepuko kanunue peke yako, mwache mwenzio ebo.
 
Back
Top Bottom