Upole unawagharimu wanaume wengi

Upole unawagharimu wanaume wengi

hapo nakupongeza ila siku na yeye mke wake akitafutia njemba sijui mtafanyaje?
 
Pole sana mleta maada, hujamsaidia katika upole wake. Utamuweka kwenye tatizo ambalo huzaa kifo, kama unampenda badili strategy mkuu.
 
Acheni kudeal na mambo ya watu kiasi hiki mnajifanya mnaona sana,mnajua sana,MNA huruma sana ...kama ni Mungu aliwapa hiyo ndoa no yeye tu anajua namna ya kuilinda as no one knows
 
Angalia asije akahamia airtel jumla sijui utafanyeje kumrudisha na huyo umesema ni mtumishi wa kondoo wa bwana
 
Nimemhurumia sana jamaa yangu.Ni jamaa ambaye tumekua naye, tumesoma naye ni mpole sana na mcha Mungu sana. Kanisani kwao ni mtu mkubwa tu sijui anacheo gani, lakini ni mtu mkubwa tu.

Huyu mshikaji alioa mwaka jana mwanamke mrembo sana lakini alionekana kama mtukutumtukutu. Mshikaji kamuombea mpaka mwanamke kawa mtu mzuri tu na kanisani naye kapewa cheo fulani hivi ni Kanisa kubwa tu hapa Dar es salam.

Sasa mwanamke amekuwa akitumia sana upole wa mwanaume kumdrive kama anavyopenda. Anaweza kumnunia tu hata wiki nzima, huku mshikaji anachanginyikiwa sana na kukonda mno, hapendi kabisa wagombane na mke wake.Yaani jamaa anavyopelekwa mpaka unamuonea huruma.

Jana nimemwambia dawa ya hawa wanawake watafutie papi, akileta nyoro kale maini. Mbona atanyooka mwenyewe tu bila hata kuchapwa.Hapa mshikaji nimemtafutia msichana na vile mshikaji anapesa demu kakubali, na huyu msichana ni wa ushwahilini mshikaji atakipata cha moto mpaka atasahau mateso.

Wanaume wapole msifikiri ni sifa ni uzombi.
Ndo unajiona mjanja sasa?

Mbona wewe na ukali wako bado unagongewa na yule mwenyekiti wa mtaa wenu?
 
wewe unataka watumishi wa mungu wawe wahuni
 
Back
Top Bottom