Uchaguzi 2020 Upinzani wasizuie wabunge wao kwenda kuapa na kuhudhuria Bunge

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,313
12,607
Wacha wabunge wa wapinzani washiriki vikao vya bunge lijalo, na ikiwezekana wapeleke majina ya watu wa ubunge wa viti maalumu. Maana kuhudhuria au kutokuhudhuria hakusaidii kuimarisha demokrasia wala vyama vya upinzani wala kubadilisha siasa za Tanzania.

CUF walifanya hivyo mara nyingi bila kuzaa matunda yoyote. Wabunge wa upinzani wamekuwa wakisusia vikao vya bunge mara kadhaa lakini sikuona walichofanikisha sanasana kujinufaisha wao wenyewe kiuchumi.

Itakuwa ni kuwanyima fursa wabunge wa upinzani waliochaguliwa kama tutasema wasihuhudhurie pia bunge. Hata wakisusia hawana uzito wowote wa kubalidisha mambo zaidi ya kuwakosesha fursa yao ya kiuchumi, kisiana na kijamii.

Vyama vijipange upya kwa 2025 kwa kufanya yafuatayo:
1. Kueneza vyama vyao hadi vitongojini.

2. Kuhakikisha kuwa wanachama wao na wapenzi wanajiandikisha kwa wingi kwenye daftari la kupiga kura wakati utakapowadia.

3. Kuhakikisha kuwa wanachama wao na wapenzi wanakwenda kupiga kura wote siku ya kupiga kura.

4. Wahakikishe kuwa wakati wa kujaza fomu za kugombea kuna watu maalumu wanaohakiki ujazaji na urudishwaji wa fomu hizo kwa usahihi.

5. Hakikisheni kuwa kuanzia sasa na kabla ya 2025 mnapata muafaka kuhusu Tume Huru ya uchaguzi na wasimamizi wake. Kama mkishindwa kuipata Tume huru ya uchaguzi tafadhali sana msiwasumbue na kuwarubuni wananchi kwa kuwapa matumaini ya uongo. Tunafahamu kuwa wanasiasa wanawatumia wananchi kama mtaji wao wa kuichumi wa kuwafikisha kwenye posho, mshahara, magari makubwa na kiinua mgongo bungeni na wapenzi wao wa viti maalum na kujipatia ruzuku. Na hii ndiyo maana walikuwa wakishiriki chaguzi za vyama vingi bila kujali Tume imekaakaaje.

Wanasema Tume ni mbaya kila siku lakini Tume hiyohiyo ilikuwa ikiwatangaza kushinda Ubunge. Naishukuru sana Tume safari hii kwa kuacha kuwatangaza hawa jamaa ili waufahamu ukubwa wa shughuli.

Tuwaache waliotangazwa kushinda nao wakafaidi kama vile nyie mlivyofaidi kwa miaka 10 kwa kutumia Tume ya aina hiihii.

Nitawashangaa wale walioshinda kama watasikiliza porojo za kuwaambia wasiende kupata mpunga bungeni, hata 2015 malalamiko yalikuwa hayohayo kwa Tume lakini walikwenda bunge kilafi pamoja na malalamiko ya Lowassa kuibiwa kura.

Kwakuwa wao safari hii wametemwa basi wanataka walioshinda wasiende bungeni. Huu ni utoto.
 
Mabadiliko yoyote yale hayaletwi na viongozi pekee. Sisi wananchi wa kawaida tuna nafasi pia. Tujiulize (ukiwemo wewe mtoa hoja), tumefanya nini katika kuchochea mabadiliko zaidi ya kupiga kura na kulalamikia viongozi wa upinzani?

Hata hivyo, napendekeza wabunge hawa wa upinzani waende bungeni wakale hela hizo na ikiwezekana wasichangie chochote ili wasionekane wakwamishaji wa maendeleo.
 
Kuwapeleka maanake umekubali UHUNI uliyofanya lazima wa protest. Hao wabinge wa Upinzani hawakupatikana kwa kura bali walichofanya CCM ni gelesha kuhalalisha WIZI waliofanya. Wameona aibu kuwa 100% Ushindani kama ule mpk mzee baba alipiga magoti ndo fake zile kama vile. Watu wanavinyongo japo wako kimya.
 
Kuwapeleka maanake umekubali UHUNI uliyofanya lazima wa protest. Hao wabinge wa Upinzani hawakupatikana kwa kura bali walichofanya CCM ni gelesha kuhalalisha WIZI waliofanya. Wameona aibu kuwa 100% Ushindani kama ule mpk mzee baba alipiga magoti ndo fake zile kama vile. Watu wanavinyongo japo wako kimya
Kama wangechaguliwa Mbowe, Sugu na Msigwa bado wangekatazwa kwenda bungeni?
 
Mabadiliko yoyote yale hayaletwi na viongozi pekee. Sisi wananchi wa kawaida tuna nafasi pia. Tujiulize (ukiwemo wewe mtoa hoja), tumefanya nini katika kuchochea mabadiliko zaidi ya kupiga kura na kulalamikia viongozi wa upinzani? Hata hivyo, napendekeza wabunge hawa wa upinzani waende bungeni wakale hela hizo na ikiwezekana wasichangie chochote ili wasionekane wakwamishaji wa maendeleo.
Kama viongozi wa upinzani wanatoroka nchi na wengine wamejifisha ubalozini, je, ni wananchi wangapi wanaweza kufanya hivyo? Wanawadanganya wananchi walalahoi eti tutaingia barabarani, mbona wao wamesepa?
 
Mimi nimependekeza wahamie CCM na wapitishwe bila kupingwa!
 
Kama viongozi wa upinzani wanatoroka nchi na wengine wamejifisha ubalozini, je, ni wananchi wangapi wanaweza kufanya hivyo? Wanawadanganya wananchi walalahoi eti tutaingia barabarani, mbona wao wamesepa?
Kwani walikimbia kabla ya siku ya maandamano?Maandamano hayakufanikiwa so let them run for their lives!Nawaunga mkono kwa wale ambao maisha yao yako hatarini wakimbie tu nchi,its not worth it kuzipigania maiti!Wasubiri mpaka zifufuke!
 
Naombeni majina ya wabunge wa Act wazalendo
Zitto kafaidi ubunge kwa miaka 15 kwa kutumia tume hiihii, leo kwakuwa hayumo basi uchaguzi ni batili na waliochaguliwa wasiende bungeni, jamani tuache usanii. Ninamuomba Mh. Spika ajae awalinde hawa mbuzi wa kafara kwenye ubunge wao ili nao wafaidi matunda ya Tume, jitihada zao na rasilimali zao walizopoteza wakati wa kampeni.
 
Yaani vyama vya upinzani vifanye jitiada zoote za kuimarisha demokrasia alafu siku ya mwisho chama tawala kinakuja kubaka demokrasia kwa kutengeneza matokea ya chaguzi kinacho yajua chenyewe, tena kwa mitutu ya bunduki, sasa apo kuna aja gani kwa upinzani kushiriki kwenye bunge la kihuni na kizurumati kama hili kama si kuwa snitch wananchi??
 
Kwani walikimbia kabla ya siku ya maandamano?Maandamano hayakufanikiwa so let them run for their lives!Nawaunga mkono kwa wale ambao maisha yao yako hatarini wakimbie tu nchi,its not worth it kuzipigania maiti!Wasubiri mpaka zifufuke!
Je, waliripoti polisi kuhusu kutishiwa maisha, au wamesepa tu kwa kupigiwa simu na wahuni mitaani?
 
Kuwapeleka maanake umekubali UHUNI uliyofanya lazima wa protest. Hao wabinge wa Upinzani hawakupatikana kwa kura bali walichofanya CCM ni gelesha kuhalalisha WIZI waliofanya. Wameona aibu kuwa 100% Ushindani kama ule mpk mzee baba alipiga magoti ndo fake zile kama vile. Watu wanavinyongo japo wako kimya
Upo sahihi sana
 
Kamba Mbowe angefanya haya uliyoandika tokea 2015 CHADEMA isinge anguka

Na sasa hivi wanajifanya hawajui kilicho waangusha haya sisi yetu macho
 
Kama viongozi wa upinzani wanatoroka nchi na wengine wamejifisha ubalozini, je, ni wananchi wangapi wanaweza kufanya hivyo? Wanawadanganya wananchi walalahoi eti tutaingia barabarani, mbona wao wamesepa?
Unafurahia mateso wanayofanyiwa wapinzani hapa nchini?
Hii nchi tuliyo wachiwa na baba wa taifa likiwa moja lililoshikamana leo hii mnaligawa vipande vipande kisa siasa!
 
Je, waliripoti polisi kuhusu kutishiwa maisha, au wamesepa tu kwa kupigiwa simu na wahuni mitaani?
Kilichomkuta Lissu au Ben saanane haina haja ya kuhangaika na jeshi hili la kipuuz!
Halima Mdee anaenda kituo cha polisi kureport wahalifu wanaomfuatilia,anakatwa yeye na kuwekwa ndani,wala hahojiwi juu ya kile alichoenda kureport!Kuna polisi hapo wa kuwaamini?
 
Back
Top Bottom