battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,672
- 2,540
Ukimpa kibarua jembe na kumpangia kazi ya kufanya kwa malipo huwa mkataba ule umekamilika endapo atatimiza kulima.Mimi sijawahi kuwa mkabila, ila ikitokea mtu yoyote wa kabila lolote anafanya mazuri, nitamkubali na kumpongeza.
Mwalimu Nyerere alituhusia tusimchague mtu hana sifa lakini ni kabila letu, ila pia tusimkatae mtu, ana sifa zote, tatizo "mkara", kumaanisha sio kabila langu.
Mambo ambayo rais Magufuli anayafanya yanaonekana with naked eyes, hivyo tusimpongeze kwa vile tutaonekana wakabila?.
Kiukweli nimeguswa sana na uchapakazi wa Rais Magufuli!. Je, kuna uhusiano kati ya kabila la mtu, na uchapakazi wake?. Je, 2020 kuna haja ya... - JamiiForums
P
Endapo kalima sawa sawa ndo katimiza wajibu wake,na endapo kalipua ndo kashajihalalishia kutopata kibarua kingine.
Kumsifu kwa kumwambia wewe ni mkulima bora ,kuna uwezekano wa kuomba nyongeza ya malipo.
Sasa kinyume chake Mgema akisifiwa Tembo hulitia maji.
Hivi Magu anastahili sifa kwa lipi ambalo hatukumtuma ila yeye kalifanya kwa ihsani? na ndio kwa hilo tumpogeze?