Upinzani tafuteni majadiliano na CCM, wanaogopa madudu waliyoyafanya upinzani ukiwa madarakani yataanikwa wazi

Ni kweli alifanya yote hayo lakini alichimbua makaburi na wakuwashughulikia (kinyama) watangulizi wake. Kulindana kukaisha. Si advocate mtu afanye kwa style hiyo lakini kuna muda nawaza tu je kulindana kutaisha lini?
Kulindana ndiyo kunafanya wastaafu wakae kimya katika haya yanayoendelea.
 
Wanaomchukia magufuli pia ni wale waliozowea short cut to successful.

Waliozowa kuishi DARESALAAM kiujanja ujanja,.
Wajasilasiasa na wengineo kama wewe.

Wengi tusiompenda ni wale tusikubaliana na viongozi madhalimu.
 
Huku juu ulitiririka viziri ila huku chini ndo sijaelewa
CCM si chama chenye uadilifu katika matumizi ya pesa.
Nani anafahamu budget iliyotumika katika vita ya Kagera,
Tuliwahi kuhoji katika ukombozi wa bara la Afrika? Yote yalikuwa ni maamuzi ya mtu mmoja. Hata Chama kushika hatamu haikuwa ridhaa ya wananchi.

Afadhali ya Nyerere yalikuwa ni maamuzi ya kwa manufaa ya wengi. Ethics hapa inamuona hana hatia.

Awamu ya pili chini ya Mzee Ruksa Waarabu walipewa mbuga ya Loliondo bila kupitishwa na bunge. Mrema alikamata dhahabu Airport ikiwa inakwenda Arabuni, alipohoji vizuri ndipo alipoambiwa cheo chake ni Waziri wa Ulinzi na hakuna cheo cha Makamu wa Waziri Mkuu kama alivyoaminishwa mwanzo.

Ya Mkapa yanajulikana kubinaifsisha miradi yote ya nchi na kuuziana na wazee wenzake.

Ya Kikwete ni mengi, kwa uchache ni GSM ndiyo washirika wake wakuu. Mzee anapesa chafu lakini uchumi aliyosomea pamoja na unafiki wa Waswahili wa Pwani vinamsaidia mumuone ni mtu wa kawaida. Yeye ndiye mfadhili wa Yanga kama hamfahamu hili.

Magufuli amewazidi wenzake wote. Wengi waliiba awamu ya pili ili wapate pesa ya cha juu ya pensheni lakini Rais Magufuli ameanza kuchota tangu mwaka wa kwanza wa kuwa madarakani.

Hawa na wanufaikaji wengine hawawezi kukubali CCM itoke madarakani. Watu kama Mzee Makamba, Lowasa, Rostam Aziz na wengineo.

Kibaya zaidi wakiwa madarakani hawazalishi ajira. Vijana wasio na ajira, wa wasomi na bodaboda ndiyo kete itakayotumiwa na wapinzani kuanzisha mabadiliko. CCM kubalini kukaa mezani na upinzani mfikie muafaka. Mabadiliko hayaepukiki.
 
Wanaompimga Rais Magufuli Ni mafisadi na wauza madawa ya kulevya na wenye vyeti feki

Sisi Watanzania tunampenda Magufuli nyie wachache mnajiangaisha
Siku mirija ulaji ya shemeji ikikatwa ndo akili zitarudi ungekuwa unajitegemea ungejua hali halisi
 
Kwa mara nyingine wale wanaoitwa mabeberu wanatupigania watanzania kuzuia wizi. Magufuli ni mwizi na mshamba.

WanaCCM Waliotulazimishia rada walijiita wazalendo, wakatupiga, wakagawana matunda na bado wanafurahia.

WanaCCM Walionunua ndege ya rais, walijiita wazalendo, wakatupiga na bado wanakula raha za wizi.

WanaCCM Wakaja na EPA, wakajitambulisha watetezi wa wanyonge, wakapiga pesa ndefu, na wamejistaafia kwa amani na wanaendelea kujichana.

WanaCCM haohao, wakaja na mambo ya vivuko, kupitia kwa Magufuli, wakaiba pesa zote, wakaleta screpa. Wakaikabidhi jeshi na haijulikani inaogelea ziwa au bahari ipi huko jeshini.

Leo haohao CCM kwa kivuli cha propaganda za uzalendo wa Magufuli, wanaiba mchana kweupe kwa manunizi yasiyokaguliwa.

Miradi yote inalazimishiwa kuingia mikataba na mtu mmoja anayejiita kichaa jiwe.

Bila kuitoa CCM madarakani, ni vilio mpaka Yesu atakaporudi kukata hukumu ya mwisho kwa kizazi hiki.
 
Magufuli allies ni zamu yao ya mavuno kwenye shamba la bibi.
 
Back
Top Bottom