Upinzani mkubali ukweli, Wananchi wamewachapa bakora kwa kutokukaa bungeni na kupinga kila kitu

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Ni kama nilivyowahi kusema na ntaendelea kusema kwamba upinzani nchini Tanzania ni kiinimacho na upo kwa ajili ya kula ruzuku.

Mimi ni mmoja wa watu ambao bila kutetereka nimemuunga mkono raisi John Magufuli na serikali yake kwa miaka mitano ilopita na ntaendelea kumuunga mkono kwa yale yote mema anayoyatendea nchi hii.

Tuwe wakweli hata wewe ukiwa na mipango yako wataka uifanye na waona kabisa kuna "obstacles" au vipingamizi ambavyo vipo kwa ajili ya kukukatisha tamaa na kuvuruga ni hatua zipi utachukua?

Ndio, hii yaitwa "obstacles to progress" yaani mtu kwa makusudi kabisa apingaaa kila kitu!

Upinzani watakiwa kuwa objective yaani uwe wapinga lakini hapohapo kwenye masuala ya kuhusu maslahi ya taifa waonekana waunga mkono asilimia 100.

Nchi zote zilizoendelea na zinazoendela wanafanya hivyo na tumeziona hata katika suala la COVID-19 wapinzani wameunga mkono jitihada za serikali na penye kupinga wamepinga na kutaka ufafanuzi.

Lengo lao la kupinga ni kuitaka serikali ifanye marekebisho ya sheria zake kuhusiana na ugonjwa huo na mengine yanayobaki kama kuunga mkono "lockdown" wameunga mkono serikali zao.

Lakini upinzani wa Tanzania ni kupinga kila lililo jema na kibaya zaidi kuzungumzia upingaji huo mitandaoni kwa kukejeli na kukashifu vitendo ambavyo wananchi wameona na wamesikitishwa sana.

Kutohudhuria vikao vya bunge na kuendelea kulipwa fedha za vikao mmeliingizia hasara Bunge na taifa kwa ujumla maana fedha hizo ni bora zingeenda kushughulikia maendeleo ya huko vijijini na huduma zingine muhimu kwa nchi yetu.

Pia kutohudhuria vikao vya bunge mmewanyima wananchi haki yao ya kufikishiwa shida zao bungeni na badala yake mkampa kazi raisi Magufuli kuzunguka nchi nzima akishughulikia matatizo ya wananchi papo kwa hapo.

Matatizo ya wananchi kama kukosa huduma ya vyoo ni jukumu ya mbunge na jimbo jimbo lake kuhakikisha kuna vyoo vya umma katika maeneo kama masoko na vituo vya mabasi.

Sasa kibaya zaidi ni kitendo cha kuwashirikisha wageni kutaka kuvuruga amani ya nchi yetu na hata kufikia baadhi yao wageni hao khasa bwana Robert Amsterdam kuandika barua za vitisho na dhihaka kwa kiongozi wa Tanzania akidhani yeye ndie mahakama ya dunia!

Wananchi wa Tanzania si wajinga ni watu waelewa sana na wapinzani wasidharau kauli hii.

Nilisema pia humu kuwa wananchi hawa walojitokeza kwenye mikutano yenu hawakufanya hivyo bila sababu, walitaka kusikia mnachosema majukwaani.

Mlichofanya mkaishia kumzungumzia raisi Magufuli na serikali yake badala ya kunadi sera zenu na ilani za vyama vyenu.

Niliwakumbusha hapa ndani kabisa ya kampeni baada ya kuona mnapotea lakini hamkusikia mkazidisha kuchukua picha za nyomi la watu na kutupa mtandaoni.


Sasa hivi wanawachapa bakora khasa na kuwakumbusha kuwa upinzani ni kuwa objective unampinga mtu na hapohapo waonyesha unamsaidia katika baadhi ya mambo ambayo ni positive.

Kiukweli mnahitaji kujipanga uzuri na kuja kivingine mkipinga yanayostahiki na kuisaidia serikali kufanya shughuli zake bungeni na majimboni kwa ufanisi na huko ndiko kula na kipofu.

Sasa hata yule anefahamu kula na kipofu anawashindaaa!!

Hiyo ni kwasababu upinzani kuja kutawala nchi hii itachukua miaka mingi sana na sababu ni haohao wananchi mnaowadharau kwa kuwaita wajinga.

Lakini ni kheri mjinga asiefahamu na anaengojea kuelimishwa kuhusu sera mbadala, kuliko yule mpumbafu anaejiona afahamu kila kitu na hata kutumia mabeberu kutaka kuiuza nchi yake.

Tuendelee kushuhudia kichapo kutoka kwa wananchi na poleni wapinzani, poleni sana.
 
Watz wanaipenda sana ccm ndio maana wapo majumbani wanafurahia ushindi wa ccm kwa amani. Kinyume na hapo wangekuwa mabarabarani wanaandamana.
Wanaipenda CCM kwa yale ambayo ndani yamiaka mitani imeyafanya na ushahidi wa wazi upo.

Wanaipenda CCM kwa kuonyesha imebadilika.

Isitoshe wapizani pia ni wanafiki kwani hivyo wanavyovipinga vingine wavitumia.
 
Wanaipenda CCM kwa yale ambayo ndani yamiaka mitani imeyafanya na ushahidi wa wazi upo.

Wanaipenda CCM kwa kuonyesha imebadilika.

Isitoshe wapizani pia ni wanafiki kwani hivyo wanavyovipinga vingine wavitumia.

Watz wanaipenda sana CCM ndio maana wapo majumbani wanafurahia ushindi wa CCM kwa amani. Kinyume na hapo wangekuwa mabarabarani wanaandamana.
 
Tusubiri bunge lenu may be litaondoa umaskini ujinga na maradhi nchi nzima na kupandisha mishahara wafanyakazi baada ya upinzani kutokuwepo bungeni
Kupambana na ujinga na maradhi ni jambo endelevu.

Hivyo angalau safari hii CCM imepewa dhamana ya asilima 100 kuhakikisha inapigana na matatizo hayo.

Na kama ulimsikia kiongozi wetu aliiongelea hilo la kupandija mishahara.

Ila, bila juhudi na kujituma kazini sahau kupandishiwa mishahara.

Kumbuka kupandishiwa mishahara si haki ni matokeo ya vipimo vya ufanisi wa kazi zako.
 
Wanaipenda CCm kwa yale ambayo ndani yamiaka mitani imeyafanya na ushahidi wa wazi upo.

Isitoshe wapizani pia ni wanafiki kwani hivyo wanavyovipinga vingine wavitumia.
Mimi binafsi nimeitetea sana CCM hapa kwa kuwa maisha yangu na familia yameboreka zaidi kwa sera za JPM

Gharama zimeshuka sana sana za maisha

Kwa miaka 4 tangu 2016 watoto wangu wawili nimeweza kuwasomesha University of Oxford kwa msaada wa serikali na mimi nimegharamia vitu vidogo vidogo tu

Watoto wamemaliza shule mwaka jana na sasa wameajiriwa serikalini kwenye taasisi zenye uhuru wa interview, sio kama zamani mwenye akili anapata taabu

Ni furaha kubwa sana ukiwa CCM na kwa ushindi huu wa JPM hakika nitaendelea kula bata zaidi

Zamani hizo nafasi waligawana baadhi ya watu na familia zao

Maisha yangu yameboreka mara 1000

CHADEMA kwisha kwisha kabisa habari zao kwenda zao

Sasa nategemea sera mpya ambazo zitanifanya nisafiri duniani kama miaka 5 iliyopita

Ni miaka mitano ya JPM nimezunguka nchi nyingi sana zaidi ya 20 duniani ukilinganisha na nchi 10 tu wakati wa JK

Wakati wa JK mafisadi wali enjoy na kusafiri kwa kodi zetu

Wakati wa JPM tunasafiri kwa kuwa tuna sababu na pesa ipo
 
Kupambana na ujinga na maradhi ni jambo endelevu.

Hivyo angalau safari hii CCM imepewa dhamana ya asilima 100 kuhakikisha inapigana na matatizo hayo...
Miaka 40 ujinga maradhi na umaskini tangia CCM ipo madarakani hayajawahi kuondoka ila yataondoka awamu hii ?kisa upinzani haupo?Miaka 40 au kuanzia 1990 iliyopita upinzani ulikuwepo?you are talking total fukin shit
 
Miaka 40 ujinga maradhi na umaskini tangia CCM ipo madarakani hayajawahi kuondoka ila yataondoka awamu hii ?kisa upinzani haupo?Miaka 40 au kuanzia 1990 iliyopita upinzani ulikuwepo?you are talking total fukin shit
Ndo maana nimesema hilo suala la kupambana na umaskini na maradhi ni endelevu.

Hakuna nchi yoyote duniani ambayo inafuta hivyo vitu viwili kwa asilimia 100.
 
Miaka 40 ujinga maradhi na umaskini tangia CCM ipo madarakani hayajawahi kuondoka ila yataondoka awamu hii ?kisa upinzani haupo?Miaka 40 au kuanzia 1990 iliyopita upinzani ulikuwepo?you are talking total fukin shit

Total fucken shit indeed...mvua imenyesha kidogo tu kila mahali ni bwawa, wanafurahia ma flyover kama mazuzu vile hawaoni ni haki yao kutokaa kwenye mazingira hatarishi
 
ZERO BRAIN mwingine huyu! Kajisemea Askofu Bagonza tulipokuwa na chuo kikuu kimoja idadi ya wajinga ilikuwa ndogo, lakini sasa tuna vyuo vikuu vingi idadi ya wajinga imeongezeka kwa kasi ya kutisha.
Poleni sana mkuu.

Utatukana sana lakini ukweli ndo huo.

Kwanini hamuamini kuwa wananchi wamewakataa?
 
Poleni sana mkuu.


Utatukana sana lakini ukweli ndo huo.

Kwanini hamuamini kuwa wananchi wamewakataa?
 
UZWAZWA unakusumbua baada ya kuamua kujitoa ufahamu. Ulikuwa huandiki upuuzi kama huu miaka ya nyuma. Eti poleni! Kama vile yanayojiri Nchini wewe hayakugusi kwa namna yoyote ile! 😳

Poleni sana mkuu.

Utatukana sana lakini ukweli ndo huo.

Kwanini hamuamini kuwa wananchi wamewakataa?
 
Poleni sana mkuu.


Utatukana sana lakini ukweli ndo huo.

Kwanini hamuamini kuwa wananchi wamewakataa?
 
Wanaipenda CCM kwa yale ambayo ndani yamiaka mitani imeyafanya na ushahidi wa wazi upo.

Wanaipenda CCM kwa kuonyesha imebadilika.

Isitoshe wapizani pia ni wanafiki kwani hivyo wanavyovipinga vingine wavitumia.
Mbona mimi siipendi au mimi sio mwananchi?
 
Kwa Afrika ubadhilifu na uchotaji wa rasilimali za umma au chama ni vitu vinavyotokea.

Lakini hata huko Ulaya na marekani kwenye vyama vya siasa upo wizi wa kughushi na kujipatia viposho kwa njia za udanganyifu.
 
Back
Top Bottom