Samia alipochukua madaraka ya Urais, kwa yale machache aliyoyafanya mwanzoni, yalimfanya apingwe sana na hardliners wa CCM, hasa CCM ya marehemu Magufuli.
Kwa upande mwingine, aliungwa mkono sana na wanaCCM wenye busara na misimamo ya wastani, wapinzani walio wengi na wale wasio na vyama vya siasa.
Kwa ujumla, Rais Samia aliungwa mkono na kundi kubwa la Watanzania kiasi cha kuleta hofu hata kwa wapinzani, kwa uungwaji mkono ule, wangeenda kwenye kampeni za uchaguzi mwaka 2025 kwa agenda gani ya kum-disqualify Samia.
Baada ya Samia kuwaachilia waliobambakiwa kesi na marehemu Magufuli, na yeye Samia kuanza kutengeneza wa kwake wa kuwabambikia kesi, mambo yamebadilika ghafla. Kwanza imeonekana wazi hakuwa na dhamira ya kulinda haki, demokrasia na kuongoza kwa kufuata sheria.
Kuwaachia waliobambikiwa kesi, huenda katika kundi lile kulikuwa na watu wake aliotaka watoke lakini ili hilo lisionekane wazi, ikabidi litendeke kwa wote. Baada ya kukamilisha hilo, mara moja na yeye akaanza kuwabambikizia watu kesi za ugaidi. Sitashangaa baada ya muda si mrefu, matajiri na wawekezaji nao wataanza kuonja joto la jiwe.
Wawekezaji na matajiri, waenende kwa uangalifu mkubwa kuwekeza katika nchi hii. Ukiingia kwa miguu yote, unaweza kujutia. Kama ameweza kuwazidishia maradufu tozo za kwenye miamala, itashindikana nini siku moja kuwawekea kodi maradufu wawekezaji na matajiri?
Rais Samia hataki kubadilisha mifumo wala sheria, bila shaka ili awe huru kuwafanya chochote watanzania wakati wowote akijisikia kufanya hivyo.
Sasa chuki dhidi ya Samia imewaunganisha hardliners wa CCM, wanaCCM walio wengi, Wapinzani na hata wasio na vyama.
Rais Samia yupo kwenye disadvantaged side bila ya kujitambua:
1) Mafuta, diesel na petrol, bei yake imepanda kwenye soko la Dunia, na yeye akaongezea tozo. Wananchi wanaona kuwa ongezeko limesababishwa na yeye. Na wanajiuliza kwa nini wakati wa Magufuli bei ilikuwa chini?
2) Kodi za kupindukia kwenye miamala kwa maelezo kuwa ili hela ipatikane ya kumalizia miradi ya kimkakati ya marehemu, wakati mtangulizi wake alisema hela ipo, na hakuwahi kuweka hiyo tozo, inaonekana yeye ndiye aliyesababisha hizo tozo na siyo kwamba mazingira ya hazina yamemlazimisha kufanya hivyo.
3) Covid 19 ya mwakajana haikuua kama inavyoua sasa hii delta, marehemu aliwaaminisha watu kuwa corona haifui dafu kwa sababu Mungu ameilinda Tanzania. Wale wenye akili za mahitaji ya lazima tu, wanaona corona kuanza kuua sana sasa, ni kwa sababu utawala huu hauna Mungu.
4) Kuna suala la bei ya gas, ongezeko la nauli, ongezeko la bei ya mbolea, yote, wananchi wanaona yamesababishwa na yeye.
5) Mitaani watu wanasema hali ni ngumu zaidi sasa kuliko hata ya wakati wa utawala wa marehemu Magufuli.
Laiti yeye mwenyewe Samia angekuwa mwerevu, na washauri wake wangekuwa super intelligent, angetafuta kitu cha kufanya ambacho kingefunika madhira yote yaliyopo sasa ili wakati wote kuwa na kundi kubwa linalomtetea na kumpandisha juu katika uongozi - kwa mfano angekazania sana ulinzi wa demokrasia na haki za watu, uanzishwaji wa katiba mpya, kulegeza sana taratibu za biashara na uwekezaji, kubadilisha sheria zote gandamizi, n.k. ili hata mbele ya mataifa aioneshe Dunia kuwa Tanzania sasa ni mfano wa demokrasia, haki na uhuru wa watu. Bahati mbaya imekuwa kinyume.
Kwa bahati mbaya, anakoelekea ni kutaka kuharibu kotekote, atajishikilia wapi? Nani watamshikilia?