Upinzani dhidi ya Rais Samia unazidi kupata nguvu

Upinzani dhidi ya Rais Samia unazidi kupata nguvu

Jiwe aliteua Makamu dhaifu Ili amdrive.Rais akifa turudi kwenye uchaguzi fullstop
 
Samia alipochukua madaraka ya Urais, kwa yale machache aliyoyafanya mwanzoni, yalimfanya apingwe sana na hardliners wa CCM, hasa CCM ya marehemu Magufuli.

Kwa upande mwingine, aliungwa mkono sana na wanaCCM wenye busara wa misimamo wa wastani, wapinzani walio wengi na wale wasio na vyama vya siasa.

Kwa ujumla, Rais Samia aliungwa mkono na kundi kubwa la Watanzania kiasi cha kuketa hofu hata kwa wapinzani, kwa uungwaji mkono ule, wangeenda kwenye kampeni za uchaguzi mwaka 2025 kwa agenda gani ya kum-disqualify Samia.

Baada ya Samia kuwaachilia waliobambakiwa kesi na marehemu Magufuli, na yeye Samia kuanza kutengeneza wa kwake wa kuwabambikia kesi, mambo yamebadilika ghafla. Kwanza imeonekana wazi hakuwa na dhamira ya kulinda haki, demokrasia na kuongoza kwa kufuata sheria.

Kuwaachia waliobambikiwa kesi, huenda katika kundi lile kulikuwa na watu wake aliotaka watoke lakini ili hilo lisionekane wazi, ikabidi litendeke kwa wote. Baada ya kukamilisha hilo, mara moja na yeye akaanza kuwabambikizia watu kesi za ugaidi. Sitashangaa baada ya muda si mrefu matajiri, wawekezaji nao wataanza kuonja joto la jiwe.

Wawekezaji na matajiri, waenende kwa uangalifu mkubwa kuwekeza katika nchi hii. Ukiingia kwa miguu yote, unaweza kujuta. Kama ameweza kuwazudishia maradufu tizo za kwenye miamala, itashindikana nini siku moja kuwawekea kodi maradufu wawekezaji na matajiri?

Rais Samia hataki kubadilisha mifumo wala sheria, bila shaka ili awe huru kuwafanya chochote watanzania wakati wowote akijisikia kufanya hivyo.

Sasa chuki dhidi ya Samia imewaunganisha hardliners wa CCM, wanaCCM walio wengi, Wapinzani na hata wasio na vyama.

Rais Samia yupo kwenye disadvantaged side bila ya kujitambua:

1) Mafuta, diesel na petrol, bei yake imepanda kwenye soko la Dunia, na yeye akaongezea tozo. Wananchi wanaona kuwa ongezeko limesababishwa na yeye. Na wanajiuliza kwa nini wakati wa Magufuli bei ilikuwa chini.

2) Kodi za kupindukia kwenye miamala kwa maelezo kuwa ili hela ipatikane ya kumalizia miradi ya kimkakati ya marehemu, wakati mtangulizi wake alisema hela ipo, na hakuwahi kuweka hiyo tozo, inaonekana yeye ndiye aliyesababisha hizo tozo na siyo kwamba mazingira ya hazina yamemlazimisha kufanya hivyo.

3) Covid 19 ya mwakajana haikuua kama inavyoua sasa hii delta, marehemu aliwaaminisha watu kuwa corona haifui dafu kwa sababu Mungu ameilinda Tanzania. Wale wenye akili za mahitaji ya lazima tu, wanaona corona kuanza kuua sana sasa, ni kwa sababu utawala huu hauna Mungu.

4) Kuna suala la bei ya gas, ongezeko la nauli, ongezeko la bei ya mbolea, yote, wananchi wanaona yamesababishwa na yeye.

5) Mitaani watu wanasema hali ni ngumu zaidi sasa kuliko hata ya wakati wa utawala wa marehemu Magufuli.

Laiti yeye mwenyewe Samia angekuwa mwerevu, na washauri wake wangekuwa super intelligent, angetafuta kitu cha kufanya ambacho kingefunika madhira yote yaliyopo sasa ili wakati wote kuwa na kundi kubwa linalomtetea na kumpandisha juu katika uongozi - kwa mfano angekazania sana ulinzi wa demokrasia na haki za watu, uanzishwaji wa katiba mpya, kulegeza sana taratibu za biashara na uwekezaji, kubadilisha sheria zote gandamizi, n.k. ili hata mbele ya mataifa aioneshe Dunia kuwa Tanzania sasa ni mfanobwa demokrasia, haki na uhuru wa watu. Bahati mbayabimekuwa kinyume.

Kwa bahati mbaya, anakoelekea ni kutaka kuharibu kotekote, atajishikilia wapi? Nani watamshikilia?
Ameamua kuwa na shingo ngumu na ukaidi kama ule wa Farao. Sio muda mrefu Mungu ataanza kushughulika naye.
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Unajaribu kuunganisha visivyo na uwezo wa kuunganishwa. Unaweza kufanya hivyo kama huna akili ya kutosha kuona kuwa kuna vitu havihusiani kabisa, na hapo hapo akili hiyo ikakutuma kwamba nawe unaweza kuhadaa wengine walio na akili kukuzidi wewe!
 
Huo upinzani unatoka wapi? Aliyewaaminisha corona haipo yeye na safu yake yote ya Juu corona iliwafanya nini? Mbona hatuwaoni tena na nyungu?
 
Alipoanza tu kumteua mkwe nilijua tu ni falsafa zile zile za jiwe na m7.
Uongozi ni ajira ya kutatua shida za ndugu.
 
2726156_PSX_20210328_141214.jpg
Huyu mwanzoni alifanikiwa kuiteka mioyo ya walioonewa japo sikuwa mtu wa pupa kumpa credit sabab CCMhl haibadiliki..

Nilichoshauri ni yeye kuanza kuwafyatisha mikia sukuma gang kama inavyoonekana pichani! Njia pekee ilikua ni yeye kupangua safu nzima na kukata mizizi ya jiwe iliyojikita chini kabisa!

Suprisngly alishindwa kufanya hivyo sasa allies wa jiwe wanamfamyia mgomo wa chini chini kumpima soon hili genge linarudi kivingine!

NB:Kuwa Sukuma gang sio lazima uwe msukuma bali ni wafuasi tiifu wa Jiwe
2726156_PSX_20210328_141214.jpg
 
Chuma kilikuwa kinacollapse miradi mingi pesa Hakuna hadi kuanza kuwapora watu account zao.
Hao walioporwa PESA zao walikuwa hawana Maelezo hizo pesa walipataje, hizo hazikuporwa zilirudishwa kwa wenyewe.
 
View attachment 1887875Huyu mwanzoni alifanikiwa kuiteka mioyo ya walioonewa japo sikuwa mtu wa pupa kumpa credit sabab CCMhl haibadiliki..

Nilichoshauri ni yeye kuanza kuwafyatisha mikia sukuma gang kama inavyoonekana pichani! Njia pekee ilikua ni yeye kupangua safu nzima na kukata mizizi ya jiwe iliyojikita chini kabisa!

Suprisngly alishindwa kufanya hivyo sasa allies wa jiwe wanamfamyia mgomo wa chini chini kumpima soon hili genge linarudi kivingine!

NB:Kuwa Sukuma gang sio lazima uwe msukuma bali ni wafuasi tiifu wa JiweView attachment 1887875
Kama siyo lzm uwe msukuma basi genge hili litafutiwe jina jingine majina si yapo mengi tu.
 
Kawatoa mashehe wa uhamsho waliobambikwa kamweka Mbowe kwa kumbambika.Karudi kule kule.

Hii inaonyesha kwamba yeye kama yeye hana maamuzi yake, anafuata sana ushauri kwa kuangalia wakati kuweza tu kujifurahisha na kupata nafuu kisiasa kwa wakati huo. Kiongozi makini hawezi kuwa hivyo.
 
Hii inaonyesha kwamba yeye kama yeye hana maamuzi yake, anafuata sana ushauri kwa kuangalia wakati kuweza tu kujifurahisha na kupata nafuu kisiasa kwa wakati huo. Kiongozi makini hawezi kuwa hivyo.
Ukiwa kiongozi yafaa uwe na washauri binafsi mentor hata kwa kuwalipa hawa watakusaidia kujua pro na cons.Ukipokea KILA kitu toka kwa wasaidizi wako huwezi jua ajenda yao ni nn.
Thus Jk na Mkapa walikuwa smart Sana.
Ishu ya Mbowe na tozo walilenga kumuharibia na washawini.
 
I tend to agree with you kalonji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom