Upinzani chutameni, mpo Uchi

Kali _D

Senior Member
Feb 10, 2019
126
250
Kabla hamjaanza kushutumu kuwa serikali ya awamu ya Tano inadhamira ya kuua na kuufuta upinzani nchini ni vema mkajiaangalia mienendo yenu na kisha mkajitathmini ni nani hasa ambae anataka kuutokomeza upinzani Nchini, ni serikali au Upinzani wenyewe?

Miaka ya 2005 ,2010 na 2015 upinzani ulijizolea umaarufu sana kwa wananchi kwa kuwa na sera bora ambazo zilijipambanua vyema kwa wananchi na wananchi walizielewa kwa urahisi kiasi cha kuwakubali na hivyo kujenga imani kwao.

Sera kama ya kupambana na mafisadi ambayo Dr. Slaa aliisimamia kwa nguvu zote au utawala wa kimajimbo ambayo Mbowe kamanda wa anga alikuwa akisimamia unaona kabisa zilikuwa zikivuta hisia kwa wananchi walio wengi. nakumbuka pia namna Dr. Slaa alivyokuwa anaweza kujenga hoja zenye ushahidi wa kutosha bungeni na nchi nzima Dr. Slaa na akina Zitto Kabwe walijipatia umaarufu kwa hoja kali Bungeni.

Hali imekuwa tofauti sasa upinzani leo hii ukiwaambia wawaeleze wananchi ajenda yao wanayo isimamia kama chama pinzani sina shaka kabisa kuwa hawana na kama wanayo basi hawana nguvu ya kuisimaimia mbele ya wananchi. mbaya zaidi hoja ambazo zilikuwa zinawapambanua na kuwatofautisha na chama tawala ndizo ambazo serikali au chama tawala ndio wanazitekeleza kwa nguvu zote na hivyo kuwafanya wakose hoja za kusimamia.

Ninachokiona kwa upinzani kwa sasa ni hoja za kudandia au bendela fuata upepo, leo ikija hoja ya korosho basi wapinzani wote watahamia katika mitandao ya kijamii na wataishupalia na kuonyesha umahili na ujuaji wao kuhusu suala husika, kesho lijitokeza suala la maduka ya kubadilishia fedha basi wanasahau korosho wanahamia maduka ya kubadilishia fedha.

Mwisho wa siku 2020 hii hapa. Magufuli atawaambia wananchi Mnaziona Barabara, Hospitali,Reli,Elimu bure, Upatikanaji wa umeme, madawa, maji nk.... sasa sijui nyie mtaonyesha nini?

Ninachokiona ni kuwa upinzani wamekosa watu wenye maono na uwezo mkubwa wa kuandaa sera na ajenda za kitaifa kama walivyokuwa enzi za kina Dr. Slaa na kundi lake hivyo kabla hawajaaza kumtafuta anaeua upinzani wajitafakali wenyewe na kuona wanaanguka wapi?

Magufuli Anachapa kazi na wananchi wanaona na vile vizuri anavyovifanya na nyie mnavipinga kwa kudai mnataka maendeleo ya watu badala ya vitu wananchi wanawashangaa pia.
 

mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,169
2,000
Yeah atuambie pia waliomtoa uhai alphonce mawazo ni kina nani.

Atumbie na waliomshambulia lisu ni kina Nani.

Atuambie pia waliomteka Mo , Roma, ni kina nani.

Atuambie faida ya kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa chato.

Atuambie alitumia fedha kununulia ndege kwa utaratibu gani.

Atuambie pia ametumia Sheria gani kusitisha mikutano ya vyama vya siasa.

Atuambie pia kwa Nini anaingia na mbwa wa kumlinda wakati anakwenda kusali kumuomba Mungu amlinde.
 

Kali _D

Senior Member
Feb 10, 2019
126
250
Yeah atuambie pia waliomtoa uhai alphonce mawazo ni kina nani.
Atumbie na waliomshambulia lisu ni kina Nani.
Atuambie pia waliomteka Mo , Roma, ni kina nani.
Atuambie faida ya kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa chato.
Atuambie alitumia fedha kununulia ndege kwa utaratibu gani.
Atuambie pia ametumia Sheria gani kusitisha mikutano ya vyama vya siasa.
Atuambie pia kwa Nini anaingia na mbwa wa kumlinda wakati anakwenda kusali kumuomba Mungu amlinde.
bado sijaona sera yenu hapo? naona tuhuma tuu ambazo anaetakiwa kujibu sio Magufuli
 

mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,169
2,000
bado sijaona sera yenu hapo? naona tuhuma tuu ambazo anaetakiwa kujibu sio Magufuli
Wewe ni mjinga kweli, kwa hiyo sifa apewe magufuli,
Ila tuhuma asipewe.?
Kha yaani huo ni uzezeta uliopitiliza.
Kama kweli magufuli anachapa kazi kama unavyomsidia basi hizo tuhuma zisingetakiwa kuwepo.
Namkumbuka baba wa taifa alipata kusema kwa kiongozi yeyote mzuri kituhumiwa tu kunapaswa kumuwajibisha,.
Kiongozi yeyote mzuri hastahili hizo ulizoziita tuhuma.
Unatakiwa kufahamu kwamba rais ndio mwenyekiti wa baraza la usalama wa taifa, rais ndio amir jeshi mkuu, rais ndiye mkuu wa serikali
 

Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
23,390
2,000
Wao wamekalia oh mikutano ya hadhara sijui nini. Halafu wanapenda sana kujidanganya na mitandao ya kijamii huku chama tawala kinapambana kujizatiti kwa mikakati endelevu. Kwa mfano haya machadema hata kufanya tu ukarabati wa makao yao makuu imekuwa shida tupu. Hawa kweli wakipewa dola sijui itakuwaje Mungu wangu.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
hakuna mahala nilipo waita watanzania ni wajinga? bali nimesema watanzania wanaona yanayofanywa na kila mtu chama tawala na pinzani, hivyo suala ni lenu kuchutama au kuendelea kutembea uchi 2020 inakaribia
Hata serikali ya makaburu wa enzi zile za utawala wa Afrika Kusini, ilikuwa inajenga miundo mbinu mingi tu, hii ya Magufuli cha mtoto...............

Lakini unadhani ni kitu gani kilichofanya dunia nzima iisusie serikali hiyo ya utawala wa makaburu??

Ni kutokana na Sera zao zilizokosa utu za ubaguzi wa rangi.

Vivyo hivyo kwa serikali hii ya Magu, hata afanye nini, watu tunachopigia kelele ni siasa zake za ubaguzi wa kiitakadi, kumwona mwanaccm ni "super human being" na kumwona mpinzani, hususani kutoka chama kikuu cha upinzani nchini, wa Chadema kama mhaini ndani ya nchi yake!!

Hebu wewe mpenzi wa Lumumba, tueleze ni kina nani walimpiga risasi Tundu Lissu??

Ni kina nani walimwua Alphonce Mawazo, mchana kweupe??

Ni kina nani walimteka bilionea Mo??

Na kina nani walimteka Roma Mkatoliki??

Ni kina nani wamempoteza Bensaanane na Azory Gwanda??

Hivi mtu mwenye akili timamu wawezaje kuisifu serikali inayofanya ujambazi wa kiwango hicho??
 

RUKIA MBONDE

Member
Mar 7, 2019
64
125
Yeah atuambie pia waliomtoa uhai alphonce mawazo ni kina nani.
Atumbie na waliomshambulia lisu ni kina Nani.
Atuambie pia waliomteka Mo , Roma, ni kina nani.
Atuambie faida ya kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa chato.
Atuambie alitumia fedha kununulia ndege kwa utaratibu gani.
Atuambie pia ametumia Sheria gani kusitisha mikutano ya vyama vya siasa.
Atuambie pia kwa Nini anaingia na mbwa wa kumlinda wakati anakwenda kusali kumuomba Mungu amlinde.
yani hapo hakuna hoja hata moja yani akuambie waliomteka MO,Roma na walio mshambulia lisu ye anawajuaje si ukaulize polisi ndo wanazo hizo taarifa
uwanja wandege kwani ye ndo mamlaka ya anga mbona mikoa mingi tu kuna viwanja vya ndege
mikutano ya kisiasa ipi ni jana tu tarehe 10 mbunge wako wa tarime vijijini amefanya mkutano
sasa sijui mnataka nini kila kitu kipo wazi
 

Kali _D

Senior Member
Feb 10, 2019
126
250
Wewe ni mjinga kweli, kwa hiyo sifa apewe magufuli,
Ila tuhuma asipewe.?
Kha yaani huo ni uzezeta uliopitiliza.
Kama kweli magufuli anachapa kazi kama unavyomsidia basi hizo tuhuma zisingetakiwa kuwepo.
Namkumbuka baba wa taifa alipata kusema kwa kiongozi yeyote mzuri kituhumiwa tu kunapaswa kumuwajibisha,.
Kiongozi yeyote mzuri hastahili hizo ulizoziita tuhuma.
Unatakiwa kufahamu kwamba rais ndio mwenyekiti wa baraza la usalama wa taifa, rais ndio amir jeshi mkuu, rais ndiye mkuu wa serikali
Nivema ukapima mwenyewe kati ya ww na mm nani mjinga hoja yangu nilikuwa nasubiri mnipe sera ambazo mnazisimamia na kujipambanua kwa wananchi wewe unakuja na tuhuma, anyway 2020 inakaribia iko siku utakuja nielewa tuu.. endeleeni kutembea uchi na tuhuma zenu mdomoni maana ndio sera zenu zilizobaki
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
20,442
2,000
Magufuli hachapi kazi na wananchi hawaoni chochote zaidi ya wizi wa trilion 1.5 , kuuza makinikia kimya kimya kuminya pesa peke yake kula 10% kwenye miladi ya flyover, Reli, bomba la mafuta ujenzi wa chato Airport kienyeji pasipo idhini ya Bunge, kutumia pesa nyingi za walipa kodi kuminya demokrasia kuwabambikia kesi kuwapiga Risasi Wapinzani huku akizuia mikutano ya Siasa kwa sheria za kienyeji akiogopa Wapinzani kuanika maovu yake kweupe, CCM ni ile ile hata Dr Slaa ni mwizi alichukua Dola milion mbili akawatoroka wenzake kipindi cha kampeni hana mfano wa kuigwa kwanza ni mzinzi aliwahi kufumaniwa Dodoma na mke wa mtu huku mke anayeishi nae pia alimpora mtu.
 

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,995
2,000
Binadam bora na mstarabu haangalii amefanya kipi cha kufurahisha watu bali asifanye nini cha kuumiza watu.

Baadhi ya makabila na mila Afrika ,zamani watoto wenye ulemavu walitupwa kwenye miamba mirefu na watu kwa kusgawishiwa kuwa hilo lilikua jambo bora walishangila na kuona kuwa ni kitu cha kawaida.
Hali iliendelea hivyo kwa karne nyingi na mwafrika aliyepinga aliadhibiwa vikali.
Walipinga kwa siri sana.
....Mpaka wakoloni weupe walipokuja ndipo walipoanza kupinga na kupambana na mila potofu zilizotumika kuua watu na kudhalilisha watu.

Karne 21 kuna watu bado wanafurahia kuuawa kwa binadam wenzao mfano ni Msibamsibamkuu. Huyu anatangaza na kuhamasisha kuuawa kwa watu ili iwe kafara ya maendeleo.
Haya ndiyo yaliyowafanya waafrika wapenda haki kuanzisha harakati za ukombozi na kupambana kwa nguvu zote na kuwatoa wakoloni katili weupe .
Hata hivyo kwa bahati mbaya wazungu walifanikiwa kuwaweka madarakani wakoloni weusi kwa katiba,sheria,mitizamo,mifumo na mitizamo ile ile waliyokuwa nayo.

Mpaka leo Afrika hawajapata kile babu zatu walichokidai toka kwa wakoloni ,yaani Utu ,haki na usawa.
Mareli,mabarabara na majumba hayawezi kuwa mbadala wa maisha ya ndugu zetu.

Kama kuna mzalendo kuliko wote anayependa madaraja ,Mareli,mandege,mabarabara kuliko uhai wake na wa familia yake tunaomba ajitokeze afanye jambo dogo sana ili reli zijengwe kwa jasho lake pia yaani atoe pesa zake zote na mali zake zote na mshahara wake ubaki kwa ajili ya chakula cha kubangaiza alimradi maendeleo ya vitu yawepo huku familia yake ikiishi maisha ya shida. Wafanye hivyo kwa sababu uhai sio jambo la maana kama madaraja. Wangeweza kufanya haya kwa ajili ya kulijenga taifa ningewaamini na ningewapinga wale wanaosema maendeleo yaanze kwa wote kuwa na maisha bora na kulinda uhai na maisha ya wote kwa usawa bila kujali vyama.

Naamini Mali walizonazo makada wa wa chama kikubwa na kikongwe Barani Afrka wakiziuza na kupeleka pesa zao zote hazina ili zikatumike kujenga miundo mbinu basi Tanzania ingekua paradiso kwa mabustani na miundo mbinu mizuri. Na maskini wasingeumizwa na makodi makodi kila siku.

Lakini watu hao wasiojali maisha ya binadam wenzao Pesa na mishahara minono kwao ni muhimu lakini kwa wananchi pesa sio muhimu na hawatakiwi wawe nazo bali wafunge mikanda. Wao wana maisha mazuri kwa pesa za walipa kodi. Wao wana Mali nyingi kupitia mishahara na maslahi mazuri waliojiwekea na wanagombania kupata vyeo ili wasikose maslahi halafu wanatudanganya kuwa tufunge mikanda.
Vitabu vya dini vinasema usimtendee mwenzako kile ambacho hungependa utendewe .

Ningewakubali wakoloni na mabeberu weusi kama wangejitoa muhanga kulijenga Taifa kwa kujitoa kwa moyo hata miaka kumi tu.
Wangeamua kukataa magari ya kifahari yanayoligharimu taifa na kuwaumiza walipa kodi wasio na hata baskeli. Wangekataa kukimbilia kujenga maofisi yasiyozalisha chchote badala yake wakajenga viwanda.
Wangepunguza misururu ya misafara inayotumia mafuta malaki ya lita. Mafuta yanayoagizwa kutoka nje kwa kodi za wananchi . Misafara ya kwenda kuzindu choo kimoja cha shimo.
Ningewaona wazalendo na wenye nia ya dhati kwa kutumia TV ya Taifa kuhamasisha haki na kukataa kizazi kinachonufaika na dhulma.

Ukishangilia Wizi wa kura na kunyanganya wagombea formu za kugombea ili mtoto wa chama fulani apate kwa dhulma ni kuhamasisha kizazi cha kihalifu. Kizazi kisichopenda haki,kizazi chenye ubaguzi,kizazi kisicho na usawa, kizazi chenye kuamini kuwa bila dhulma huwezi kupata mafanikio.
Ndio maana chaguzi za Afrika zimegubikwa na ushirikina.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom