"Laba nitoe mfano sasa hivi. Unajua sasa hivi hata hali ya kisiasa, kwa ninavyotazama mimi, kwa namna ambavyo naiona, hali ya kisiasa ina utofauti mkubwa sana na hali ya siasa ya kipindi kilichopita. Kwa nini? Hata upinzani wa sasa hivi una utofauti na upinzani uliopita."
Mhoji (Mwanaume):
"Mmmh."
Mhojiwa:
"Kwa nini sasa nasema hivyo? Upinzani wa kipindi cha nyuma, japo nilikuwa na umri wangu mdogo, lakini nilikuwa nikiona watu wakijibizana wanajibu hoja. Yaani kukiwa na ajenda, ajenda zinajibiwa kwa hoja. Lakini njoo sasa hivi, yaani watu hawashambuliani kwa hoja, wanashambuliana zile... yaani mtu anamshambulia mtu binafsi.
Ndio maana unakuta hata mimi ninayezungumza hapa, ukija baadaye mkaposti hata kwenye... nini... kwenye Instagram, yes, unakuta matusi kibao kwenye comment. Nini maana yake? Kwamba kuna... yaani kuna namna fulani watu wameondoka katika the reality ya kujibu hoja, wameingia sasa kushambulia watu binafsi. Mtu atakuangalia tu... ah huyu tayari ni hivi.
Yaani wamishatoka kwenye ile upinzani sasa ule ambao tunautamani—upinzani wa kina Mrema. Sio upinzani wa sasa hivi... unamsikiliza labda kiongozi wa BAVICHA muda wote yeye ni matusi, kufoka tu. Hafoki kufokia hoja ile yaani kwa maana anajibu ile hoja, anafoka kumfokia mtu binafsi. Sasa hiyo unaona kwamba kuna mazingira pia bado yana... yana utofauti.
Sasa kwa kiongozi mwingine ambaye yeye sio mtu wa hekaheka, yaani kwa maana hapendi kelele, unakuta anaweza akaona kwamba ku-control zile emotions anaweza akatoka nazo yeye kaaribu, kaamua kukaa kimya asiende kujibizana kwa matusi ama kwa namna ambavyo yule aliye... aliyekuja wa upinzani amezungumza vipi. Kwa hiyo kuna hali hiyo pia ya utofauti pia wa upinzani. Kwa hiyo..."
Mhoji:
"Kwa hiyo nyinyi vipi sisi? Kwani mnajibu hoja nyinyi? Ata kama mnajibu..."
Mhojiwa:
"Unamjibu hoja nani? Yaani unajibu hoja zipi? Hawana hoja ya kujibiwa. Ndio maana huoni kwa sababu unaona muda mwingi unashambuliwa kwa matusi, unashambuliwa kwa vitu ambavyo havipo. Kwa sababu kama hoja, mara ngapi ambazo unakuta yale mambo ya maslahi ya taifa tayari yana clarifications zilizonyooka, umeona? Mtu anazungumzia labda swala la Katiba kama kitu binafsi. Lakini Katiba ni ajenda ya Chama cha Mapinduzi ambayo ilani ya CCM imeeleza kabisa na Rais ameahidi, si unanielewa? Lakini anapokuja mtu mwingine anataka kutuchukulia kama hiyo ni ya kwake na chama chake na kikundi chake inakuwa sio..."
Mhojiwa: > "...hiyo ya kwake na chama chake na kikundi chake inakuwa sio sawa, kwa maana..."
Mhoji: > "Mwenyekiti, kumradhi kidogo, samahani. Kwani mnahisi sasa hivi mnajibizana na CHADEMA au mnajibizana na raia ambao wamechoka?"
Mhojiwa: > "Raia waliochoka sisi..."
Mhoji: > "Hapana, no no no. Yaani kwa unavyoona wale watu mtandaoni wanaobishana, ama nyinyi mkiweka... wanakutukana. Umesema mkiweka posti unakuta unatukana unafanyaje. Unahisi wale wote ni CHADEMA ama wengine tu ni raia wa kawaida ambao wengine pia hawana hata uanachama wa vyama vya siasa? Ila tu wanaona vitu haviendi, mambo hayaendi, alafu wanaona kama... wanaona kama—tutumie kwa sababu ni mwenyekiti wa vijana—tutumie lugha ya vijana, wanaona kama kuna miyeyusho miyeyusho tu. Wao wanaona hivyo. Unahisi wote ni CHADEMA au wengine ni raia tu ambao wanaona kabisa vitu haviendi na nyinyi mnazungumza vitu ambavyo havipo?"
Mhojiwa: > "Kumejengeka upotoshaji mkubwa sana na vijana wameshindwa kufungua akili pia. Kwa sababu ya... nikwambie kitu kimoja, sisi tuna utofauti wa namna ya kuchambua mambo. Vijana wengi sasa hivi wanaamini hata katiba ndio solution ya matatizo yao. Kumbe, ukiniambia mimi leo, hata leo tukaingiza sera mpya, tukatengeneza katiba... kama watu hawajawajibika ipasavyo, bado tutarudi kwenye swala la malalamiko kwa wananchi."
Mhoji: > "Watawajibikaje? Kwa sababu Msahafu ama Biblia ya nchi si ndio Katiba? Ambayo inajenga misingi yote ambayo tunaiona. Sasa kama unasema Katiba... hata tukiwa na Katiba kama watu hawatawajibika, watawajibika kupitia nini kama sio Katiba?"
Mhojiwa: > "Tuna changamoto kubwa sana baadhi ya..."