Upi uhalali wa Muungano wetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upi uhalali wa Muungano wetu.

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Bado nipo nipo, Nov 20, 2011.

 1. B

  Bado nipo nipo Member

  #1
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hali ya kawaida kabisa, inajulikana kuwa Muungano baina ya nchi ni maafikiano kati ya nchi na nchi. Na mnapoungana mmeridhia kuwa pamoja kwa mambo yote, sasa mimi nahoji juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Zanzibar ina rais wake, na Jamhuri ya Muungano ina Rais wake. Sasa huyu rais wa jamhuri ya Muungano ana nguvu ipi dhidi ya Zanzibar? Na kama hana mamlaka yoyote juu ya Zanzibar uhalali wa Muungano uko wapi? Katiba ijayo ibadilishe hiki kitu maana sikielewi elewi vile!
   
 2. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,071
  Trophy Points: 280
  hapa kuna maswali mengi na wengi wetu wanayajua lakini kwa vile waliounda muungano huu walikuwa na interests zao zingine ambazo either zimepitwa na wakati au wanajua kuwa unaficha udhaifu wa walio wengi.

  Binafsi nadhani Kisiwa cha Pemba, Zanzibar, Mafia nk wakazi wake wengi wako na uhusiano wa moja kwa moja na upande wa bara. Aliyevitenganisha ni hao wageni ambao walikuja kufanya shughuli zao na wakaamua kulowea. Nimeangalia Channel 10 juzi wakielezea historia ya Kilwa Kisiwani jinsi kilivyowahi kununuliwa na mfanyabiashara mmoja wa Kishiraz karne ya 7-9 kwa kipande cha nguo, lakini leo hakina mgogoro wa umiliki. Ni sehemu ya Tanzania!

  Ukiangalia vizuri historia ya Zanzibar ukiihusisha na Tanganyika inaleta jambo jipya (wengi tunalijua) ambalo ni Kilomita 10 za mwambao (kutokea mwambao wa Mombasa mpaka sehemu za Msumbiji) ambazo tukiendelea na mawazo tuliyonayo sasa huenda zikaanza 'kudaiwa' nazo! Pia kuna baadhi wanaodai kuwa Pemba haikuwahi kuungana na Unguja!

  Kwa ujumla ukianza kuongelea haya mambo utasikia wengine wanasema mara "oh, wewe haya mambo ya Muungano huyajui, ...oh! hujui historia" nk. Yaani haina tofauti na 'siasa (uswahili) za simba na yanga'!!

  Lakini matokeo ya haya yote ni kuwa nchi hii (ikijumlisha pande zote mbili) pamoja na kuwa na utitiri wa rasilimali zimekosa kuendelea kwa aidha kuchelewesha maamuzi au kwa kutokuwa na maamuzi kabisa sabau ya 'MUUNGANO'!
   
 3. B

  Bado nipo nipo Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimekupata asante kwa kuona hilo!
   
Loading...