UPEPO WA USIKU

UPEPO WA USIKU

FANANI MTENZI

Senior Member
Joined
Jul 4, 2017
Posts
106
Reaction score
95
UPEPO WA USIKU-18

BONIFACE BIRAGE

Mama Shully alijishauri sana kati ya kutopiga simu au kupiga kituo cha polisi.Tiyari ameshakuwa mshirika namba moja katikati ya mauaji makuu matano nyumbani kwa Laredo.Kukaa kimya ni ikuruhusu kuuunga mkono jambo hilo ambalo lilihitaji nguvu ya dola kulitatua.Na pili ana uhakika gani kwamba Laredo hatamgeuka?Kama aliweza kwa mama mkwe bila sahaka na kwake litakuwa kitu rahisi sana kumfutilia mbali!Halmashauri ya ubongo wake ilizidi kukinzana.

Akaichukua simu nakuamua kupiga sasa.Ilibidi ampigie polisi anayemjua kupitia watu wake wa karibu.Hilo lilitosha kabisa kuondoa uhusika wake nakuepuka maswali mengi uyasiyo na majibu!Alijishauri kama atafanikisha jambo hilo hatakuwa na wakati mgumu kuwekwa katika maswali.

Alipiga namba.

“Habari mama Shully?”sauti ya upande wa pili ilipokea.Mama Shully alitafuta maneno ya kusema akayapata.

“Salama afande Rajabu.”

“Familia haijambo.”afande rajabu alizungulza kwa utulivu wa hali ya juu.

“Afande hawajambo.Tuache kwanza mambo ya familia.Kuna tukio zito limetokea.”alizungumza Laredo kumteka msikilizaji wake nakuchukua umakini wake.

Msikilizaji alimtilia maanani sana,”Kuna nini tena?”

“Mauaji ya kutisha yamefanyika nyumbani kwa Yule shoga yangu Laredo siunamjua?”

Afande Rajabu ilibidi kwanza aka echini maana alikuwa kituoni kasimama akipiga zogo na maswaiba wenzake lakini kwa mshtuko wa taaarifa ilibidi awe makini.

“Yamefanyika muda gani?”

“Mimi nimegundua dakika kama kumi na tano zilizopita.Kuna vifo vya watu wa tano mpaka muda huu.Na baada ya kujua shoga yangu anataka nimfichie siri!”

“Eti unasemaji kwani polisi hawajui hadi muda huu?”

“Kwani kuna taarifa yoyote mmepokea au umesikia yah ii ninayokupa?”ikawa zamu ya Laredo kuuliza.

“Hapana.Umenishtua sana.Nina pajua.”
“Nataka mje haraka iwezekanavyo maana Yule shoga yangu amegoma kutoa taarifa.Kwa inaonekana anajua vizuri mazingira ya mauaji hayo.”hakutaka kusema kama anaelewa kisa kizima.

“Mmm ni ngumu sana.”

“Ila naomba isjulikane kama ni mimi nilitoa taarifa please.”

“Kwanini?”

“She is my bestfriend.Sitaki ajue kama nimemsaliti.”

“Nakuelewa you only did what needed to be donel.Infact umeisaidia jeshi la polisi.”

Mama Shully alisema akiwa anahisi hatia moyoni mwake.Nusu alihisi yupo sawa na nusu alihisi hayupo sawa.


“Nilienda kwake kumsalimia nikamkuta chumbani akiwa analia halafu kuna maiti tano zipo sakafuni!Na hao watu ni Bario mume wa Laredo,Hamza shemji yake,Masua mpangaji mwenzake,mtoto wake Laredo pamoja na maiti ya mama mkwe wake.”alisema Laredo kwa kubabaika.Sauti yake ilikuwa na mawimbi sana.

Akaendelea kuchuja nakupembua,”Huyu mama mkwe ali…”akagoma hakutaka kusema kwamba mama mkwe alikuwa mgeni nay eye alimuhifadhi kwake siku ile kabla ya Laredo kurejea kutoka alipoenda.Na kwamba mama mkwe alikuwa amezungumza naye mudas mchache uliopita.Kumbe maskini mama Yule anaiendea kufa yake.Kufika hapo mama Shully alishtukia machozi yakimtoka kwa huruma na woga uliochanganyikana na kihoro.

“Uligundua ni maiti kweli?”
“Ndiyo kulikuwa na damu halafu watu wote walikuwa kimya hata kama ningewatingisha bado wasingeamka.Laredo mwenyewe kanithibitishia kwamba hao watu ni maiti!Isitoshe Hamza ni mfanyakazi mwenzangu.Kumkuta katika hali ile siwezi kunyamaza.”

“Ok nimekuelewa je huyo swaiba wako anabunduki?”

“Anayo ya mume wake.”

“Alikwambia hao watu wamekufaje?”

Lilikuwa swali gumu kidogo.Lakini hakuwa tayari kujibu,”Aliniambia tu wamekufa.”
“Kuna kitu hutaki kukisema najua ni shoga yako unataka kumlinda.”

“Afande Rajabu mimi sijui kitu nimekwambia kile nilichokiona mengine mtayajua mkifika kwake.Maana huyu shoga yangu nahisi kichwa kimemruka kwa kweli.”

Kilipita kimya cha sekunde kadhaa lakini Rajabu akaamua liwalo liwe ngoja aandae kikosi waende eneo la tukio.Uamuzi wowote atakaochukua lazima uwe na tahari kwa utendaji kazi wake mzuri au mbaya.

“Sawa ila usifanye lolote wala usimwambie chochote.”alitahadharisha kwa ukali kidogo.Mama Shully alimuelwa.Akakata simu.Polisi Yule alijiandaa alikusanya kikosi akitoa taarifa kwa wenzake.

Kituoni.

Alienda kwa mkuu wake wa kazi.Aliingia ofisini kwake akipiga saluti nakumwelezea kuhusu taarifa aliyoipokea kutoka kwa raia mwema.

“Ina bidi twende haraka iwezekanavyo.Jihadharini maana hatujui mtuhumiwa atakuwa ni huyo Laredo au kauna mwingine.Bebeni vijana wa kutosha pamoja muwe makini.Ukiniambia kua maiti takribani tano unani changanya sana.Hilo sio tukio dogo.”mkuu wake wa kazi alimweleza afande Rajabu aliyekuwa amekaukia kwa kusimama wima.

“Sawa mkuu.Tuna kwenda sasa hivi.”

Mkuu wa kituo alichukua simu yake akapiga nakutoa maelekezo kwa wenzake kwamba kuna tukio la kukutwa kwa maiti takribani tano nyumbani kwa mtu hivyo walipaswa kuwa makini nakikosi maalum kikiwa kimejipanga kiende kuangalia.

Maandalizi yalifanyika.

****

“Baba mimi kweli mama haja nyumbani kwangu.”
“Najua kakudanganya wewe nieleze alipo mke wangu.”sasa mzee alikosa subira nakuona kete anazochezewa na mkwewe kumficha mke wake zimezidi.Aliinuka kabisa akitaka kuanza kuangalia vyumba hadi vyumba alimuradi amkute mkewe.

“Tena siajabu yupo humu ndani akjificha kwenye vyumba.Namjua mke wangu vizuri sana ndoa ya miaka 35 si mchezio!.”

Laredo alikosa mwelekeo wa kujiteteta.Lilikuwa swala dogo lakusema alipo mama mkwe lakini tabia ya Laredo kukwepa maelezo lilisababisha sintofahamu nakuonekana kama yeye ndo mwenye makosa.Ilibidi abanwe na mzee wake aeleze alipo mkwewe.

Mzee alipiga hatua nakuingia kwenye korido.Laredo alipoona hivyo alikosa pumzi ya amani.Ikiwa ataingia chumbani mwake bila shaka atakuta jambo la siri.Mzee alipita akiwa kawaka kidog ule upole wake ukageuka kuwa chukizo.Aliingia hadi jikoni biola kumwona mkewe alikagua hadi nyuma ya mlango wa jikoni lakini kulikuwa hakuna mtu.

“Mama Bario hebu toka mke wangu.Nimekuja tuyamilize madoido wangu.”sasa alipaaza kabisa sauti.Hali hiyo ilimtia hzuni Laredo akijua tayari kesha mfutilia mbali mama mkwe.
Mzee alirudi chumba kingine huko nako hakuona mtu.Ilibidi aende chumba cha Laredo pasipokujua kuwa kuna kitu gani ile kafika mlangoni alihisi kusimamiwa kwa nyuma!Laredo mwenyewe alikuwa amesimama kwa nyuma!

Ukasikika mlio mkubwa wa bunduki!Paa!

KWA SIMULIZI ZAID TEMBELEA BLOG HII
UPEPO WA USIKU-18
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 75
Back
Top Bottom