Upepo mkali unaovuma usiku huu 31.07.2021 kulikoni?

Bunju sokoni unavuma hatari, miti iliyokauka na majani ni kudondoka tu, nimetazama weather report, wanadai bunjub kwetu, mvua yaweza nyesha saa kumi na moja na kumi na kumi na mbili asubuhi, probability ni 50%..
Hawa TMA chance labda iwe 98% ndio inatokea.
 
Wanaume wa Dar bhana, upepo kidogo tuu na manyunyu imeshakuwa habari kubwa
Tulio nchi kavu tukiona hali kama hii hatujifikirii zaidi sisi bali tunawaza kwa ndugu na jamaa wanaofanya shughuli majini(baharini) & pamoja waishio karibu na fukwe itakuwaje.

Si mpaka madhara makubwa yatokee ndio uanze kuona ni jambo kubwa.
 
huku njombe hua unaanza sakumi aise unapuliza balaa changanya na baridi kali la huku linalochoma na nyasi
 
Iringa town hapa kitung'u(baridi kali +upepo unaovuma kwa kasi ) bado kinakunguta vibaya , hapa napiga hesabu jinsi ya kunawa huo uso .
 
Wapendwa Jf haitumiwi na wana dar pekeake, unapoandika weka maelezo yanayojitosheleza.

Yani umeandika kana kwamba wote humu tunaishi mtaa mmoja.
 
Nilikuwa Kigamboni imebidi niamke nishangae maana si kwa upepo ule.Nilifikiri ni TSUNAMI
 
Umenistua saa nane na nusu hivi, nikadhani ni mvua kubwa inanyesha nikaenda kutoa viatu nje kumbe ni upepo tu. Nikawa nahofia miashoki iliyo jirani na nyumba nayoishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…