Upendo unaweza kuisha ghafla kiasi hiki?

Mi naamini anampenda ila tusisahau kuwa kazi nayo ni muhimu,..pia naamini amempeleka kazini kzn kwa hata asingeenda kumchukua boss wake bado angelazimika kwenda kazini kutoa taarifa ,kupata kibali cha kusafiri, kuchukua pesa za kumsaidia kwa ajili ya shyghuli zote za msimba wa mkewe, ukiwa mwajiriwa mara nyingi ni lazima uende tena kazini ili ufuate taratibu zoote za kiofisi ndipo uweze kuondoka...

Naendelea kuamini kuwa anampenda mkewe ila pia ni wajibu wake kufuata taratibu za kiofisi kabla hajasafiri kwenda msibani.
 
BLACKWOMAN, HAYO MAANDISHI YAMENIPA TAABU KIDOGO KUSOMA KUTOKANA NA UDOGO WAKE,,AU UNA JARIBU KUWAPIMA WANA JF KAMA MACHO YAO YANAONA VIZURI ,lol........
 
BW tatizo hapa liko kwa boss maana alipaswa kumuacha aende akafuatilie habari hizo za kusikitisha pamoja na kujua mipango ya mazishi na mambo mengine. boss anathamini kazi tuu hamjali anaemfanyia kazi na utu haupo..jamaa nae anachunga kibarua..utajuaje kama alishaomba ruhusa boss akamkatalia? au akamwambia nipeleke kwanza kazini halafu uende kitu ambacho sio sahihi..utu, kutokujali kwa boss ndo tatizo
Habari ya J3 wana JF
Jana jumapili nilikwenda kwa jirani yangu kumsalimia nilipofika nilimkuta yeye na dereva wake wa kazini wote wanalia kuuliza kulikoni jirani yangu akaniambia dereva wake amefiwa na mkewe mie na jirani yangu tukawa tunamfariji huyo dereva kwa msiba alioupata.
Ilibidi niulize ilikuwa vipi, jirani yangu akanieleza walikuwa njiani kutoka kazini simu ikapigwa kwamba mkewe amepata ajali Moshi wamempeleka hospital, dereva akaamua kumpeleka kwanza boss wake nyumbani ili aweze kufanya utaratibu mwingine alipofika nyumbani kwa boss wake akapigiwa simu mkewe amefariki. mwishowe yule dereva akaondoka kurudi nyumbani kwake.
Leo asubuhi nimekwenda pale kwa jirani yangu kujua maandalizi yanakwendaje tuweze kushirikishana cha ajabu nikamkuta yule dereva amekuja kumchukua boss wake kumpeleka kazini.
Nikajiuliza amepata wapi nguvu ya kuweza kufanya kazi leo baada ya msiba mkubwa kama huo kutokea?

Ninajiuliza je huyo Dereva alikuwa hampendi mkewe au baada ya kufa upendo unatoweka ghafla hata kabla ya maziko?

Sidhani kama mapenzi yamepungua bali yeye kama mtumishi kuna taratibu za kufata ofisini ruhusa na maandalizi pia ofisini kwake lazima wapate taarifa tena ya maandishi sio mdogo so ni kawaida kabisa atakwenda kuaga then atarudi kuendelea na msiba.
 
BW Tafadhali jaribu kuwa unaongeza ukubwa wa maandishi yananipa taabu kweli kweli kusoma ni ombi tu lakini
 
Habari ya J3 wana JF
Jana jumapili nilikwenda kwa jirani yangu kumsalimia nilipofika nilimkuta yeye na dereva wake wa kazini wote wanalia kuuliza kulikoni jirani yangu akaniambia dereva wake amefiwa na mkewe mie na jirani yangu tukawa tunamfariji huyo dereva kwa msiba alioupata.
Ilibidi niulize ilikuwa vipi, jirani yangu akanieleza walikuwa njiani kutoka kazini simu ikapigwa kwamba mkewe amepata ajali Moshi wamempeleka hospital, dereva akaamua kumpeleka kwanza boss wake nyumbani ili aweze kufanya utaratibu mwingine alipofika nyumbani kwa boss wake akapigiwa simu mkewe amefariki. mwishowe yule dereva akaondoka kurudi nyumbani kwake.
Leo asubuhi nimekwenda pale kwa jirani yangu kujua maandalizi yanakwendaje tuweze kushirikishana cha ajabu nikamkuta yule dereva amekuja kumchukua boss wake kumpeleka kazini.
Nikajiuliza amepata wapi nguvu ya kuweza kufanya kazi leo baada ya msiba mkubwa kama huo kutokea?

Ninajiuliza je huyo Dereva alikuwa hampendi mkewe au baada ya kufa upendo unatoweka ghafla hata kabla ya maziko?
Mhm hii ikotofauti kwangu!Kila mtu na maono yake na inategemea waliishi vipi!lakini hatakama!Mke ni kila kitu!
 
inawezekana alikuwa aende kwanza kazini aweke mambo sawa ndo aendelee na msiba. pia boss wake ndo angeweza mpa mwongozo kuwa kesho bana usije shughulikia mambo ya msiba. shida mdau unauliza swali ambalo majibu yapo ndani ya moyo wa dreva na boss!
 
wanaume wana roho ngumu we acha tu! angetulia zake tu home, utafikiri analipwa mshahara kwa siku!
 
^^
Alichobeba kifuani mwake ndicho kimemfanya awe alivyo.
Hard to understand
^^
 
Habari ya J3 wana JF
Jana jumapili nilikwenda kwa jirani yangu kumsalimia nilipofika nilimkuta yeye na dereva wake wa kazini wote wanalia kuuliza kulikoni jirani yangu akaniambia dereva wake amefiwa na mkewe mie na jirani yangu tukawa tunamfariji huyo dereva kwa msiba alioupata.
Ilibidi niulize ilikuwa vipi, jirani yangu akanieleza walikuwa njiani kutoka kazini simu ikapigwa kwamba mkewe amepata ajali Moshi wamempeleka hospital, dereva akaamua kumpeleka kwanza boss wake nyumbani ili aweze kufanya utaratibu mwingine alipofika nyumbani kwa boss wake akapigiwa simu mkewe amefariki. mwishowe yule dereva akaondoka kurudi nyumbani kwake.
Leo asubuhi nimekwenda pale kwa jirani yangu kujua maandalizi yanakwendaje tuweze kushirikishana cha ajabu nikamkuta yule dereva amekuja kumchukua boss wake kumpeleka kazini.
Nikajiuliza amepata wapi nguvu ya kuweza kufanya kazi leo baada ya msiba mkubwa kama huo kutokea?

Ninajiuliza je huyo Dereva alikuwa hampendi mkewe au baada ya kufa upendo unatoweka ghafla hata kabla ya maziko?
There are different ways of handling and tackling pain and grieve.Some prefer to work more so as not to feel much pain through past memories and the loss they have. So I can understand why he might be working,because when we keep ourselves busy we avoid thinking alot,I believe that´s his way of grieving,DONT JUDGE A BOOK BY ITS COVER,He is the only one who knows what he feels inside,thereby we/you cannot judge him,some people don't like to show when they are hurt,they would rather eat themselves inside! SOME PEOPLE LIKE TO SHOW THEIR STRENGTH AND NOT THEIR WEAKNESS!!
There is two sides for everything so there might be some other reasons too behind the whole scenario.
 
Pengine walielewana na boss kwamba asubuh amchukue waende kazini akamfanyie mipango ya ruhusa na chochote kwa ajili ya mazishi,,,japo boss alikuwa na uwezo wa kumsaidia tu usiku ule ili yule bwana asubuhi aende tu zake kwao..
 
kwani anafanya kazi kwenye kampuni ya boss ama kuna ma boss juu ya boss? Koz kama ni kampuni ya boss anaweza ruhusiwa papohapo lakini kama kuna ma boss wa boss wake lazima kutakuwa na kautaratbu karef anakotakiwa kukaptia.
 
Back
Top Bottom